Uliwahi kuogopa sana kufanya nini ila baada ya muda ukaona ni kawaida tu tena ni kama vile umechelewa kuanza

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Woga na hofu miongoni mwa wangwana wengi humu duniani, vimechelewesha na kukosesha watu vitu na mambo mengi mazuri sana waliyopaswa kua nayo au kuyafikia mapema katika dunia hii.

Majasiri wengi, walioamua na waliothubutu bila kusita walifanikiwa mapema kutimiza ndoto, nia, matarajiao na matamanio yao ya maisha mapema.

Kwa upande wako hofu na woga wako vimekuchelewesha na kukukosesha vitu au mambo gani muhimu maishani mwako? Ulitokaje salama kwenye mkwamo huo, na unajutia hofu na woga wako.

Kumbuka woga wako unaweza kua ndio chanzo umaskini wako
 
Nilikuwa naogopa kutongoza siku zaenda upwiru nao ukawa unanishambulia!,nikajikaza nikaimbuisha mtoto mmoja hivi nyuma sio kabinuka ni kabenjuka! Babu nilikataliwa vibaya nikajiona mimi sio binadamu ni ng'ombe!!.

Zikapita siku upwiru ukawa unanihamasisha nitongoze tena nikatongoza kitoto chakawaida tu sema ngozi ya mtume! Na mara hii nikakataliwa! Hiyo siku nililia huku napiga kelele hadharani kwa watu nalalamika ya kwamba mi upwiru wangu niupeleke wapi sasa?

Nilikaa mwezi mmoja nikaona nyie waja msinitanie nikazama bafuni na sabuni ya unga nikaipendezesha nafsi..😂😂
 
Nilikua naogopa somo la hesabu shule ya msingi. Wakati nipo darasa la 5 kipindi cha likizo kaka angu akawa ananifundisha ndipo nikaja kugundua kumbe ulikua uoga wangu tu ila hisabati ni somo rahisi sana. Mtihani wa taifa darasa la 7 nilifaulu kwa daraja la kwanza na hesabu nilipiga 50/50 nikachaguliwa kujiunga kidato cha kwanza azania secondary
 
KULA NGURUWE a.k.a kitimoto. Zamani nilikuwa natishwa mara ooh nyama mbaya, mara Ina wadudu, mara ukilanutakufa . Nilipokuja kuoonja aisee !!! Sijui nilichelewa wapi nikiwa nadanganjwa kwa Mila za kiarabu na kilawi
 
Kuna kipindi nilikopa mitandaoni jamaa wakawa wanasema watanifuata nyumbani kesho.
Sasa kesho yake nikawa nimetoka kidogo, kurudi home nakuta Kuna gari silijui limepaki karibu kabisa na nyumbani. Duh ilibidi nirudi nyuma. Baadaye nikaja kugundua kwamba Ile gari iliharibika na dreva alikua amekwenda kununua spea Kariakoo.
 
Nilikuwa naogopa kutongoza siku zaenda upwiru nao ukawa unanishambulia!,nikajikaza nikaimbuisha mtoto mmoja hivi nyuma sio kabinuka ni kabenjuka! Babu nilikataliwa vibaya nikajiona mimi sio binadamu ni ng'ombe!!.

Zikapita siku upwiru ukawa unanihamasisha nitongoze tena nikatongoza kitoto chakawaida tu sema ngozi ya mtume! Na mara hii nikakataliwa! Hiyo siku nililia huku napiga kelele hadharani kwa watu nalalamika ya kwamba mi upwiru wangu niupeleke wapi sasa?

Nilikaa mwezi mmoja nikaona nyie waja msinitanie nikazama bafuni na sabuni ya unga nikaipendezesha nafsi..😂😂
nafurahi umeacha woga sasa :pedroP:
 
Kuna kipindi nilikopa mitandaoni jamaa wakawa wanasema watanifuata nyumbani kesho.
Sasa kesho yake nikawa nimetoka kidogo, kurudi home nakuta Kuna gari silijui limepaki karibu kabisa na nyumbani. Duh ilibidi nirudi nyuma. Baadaye nikaja kugundua kwamba Ile gari iliharibika na dreva alikua amekwenda kununua spea Kariakoo.
saivi wanasemaje au umeshalipa mkopo wao, na je bado unawakopa?:pedroP:
 
KULA NGURUWE a.k.a kitimoto. Zamani nilikuwa natishwa mara ooh nyama mbaya, mara Ina wadudu, mara ukilanutakufa . Nilipokuja kuoonja aisee !!! Sijui nilichelewa wapi nikiwa nadanganjwa kwa Mila za kiarabu na kilawi
kwahiyo saivi unazifakamia nyama za nguruwe kisawasawa right?:pedroP:
 
Back
Top Bottom