Uliwahi kuonesha jeuri ya pesa hata kama huna, ili kulinda heshima?

Uliwahi kuonesha jeuri ya pesa hata kama huna, ili kulinda heshima?

Yule demu aliponipa mzigo tako tatu wadhungu hao. Nikasingizia sijala ngoja nile nimpe show za WWE John cena you can't see mee. Nikala chips ndizi mishikaki. Nikampq romance kupima oil naona huyu kashaiva nikachomeka kupiga take tatu wajapan hao. Nikaona sasa hapa mbona kazi sana. Nikaona ngoja nizuge zuge kuangalia vipindi vya wanyama kwenye TV. .

Alipoamka nikaona nitumie nafasi hii kumuonyesha show ya kibabe. Kupiga tako nyingine tani aisee wazee hawajakosea siku ya kufa nyani kweli miti yote huteleza. Kupiga tako nikajikaza yani kufika tako ya tano tu tena nimejikaza nikawa na uma na meno wahindi haoo. Aisee what an embarrassing day.

Kurudi kwenye mada, ili kurudisha heshima nikamuliza demu hivi unaishi wapi? Akajibu magomeni nimepanga chumba elfu 70. Nikaanza kujiongelesha hapa inabidi upange sinza chumba laki na hamsini. Nataka nikukipie kodi ya miezi kumi. Kwanza kabla sijasahau shika hii laki. Ukifika nyumbani nakutumia hela nyingine ununue vitu vya nyumbani hiyo laki ni nauli tu. Hata samsung unayotumia sio simu ya maana nakununulia iphone.

Alipoondoka na laki yangu nikatupa line nikasajili line nyingine kwa mpita njia. Huyu dada tulikutana kwenye mwendokasi. Hata mwendokasi sipandi tena nawasiwasi naweza kukutana nae huko [emoji51][emoji51][emoji51]
Nimecheka hadi basi[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Niko na toto la Nai tunapigiana simu tu tukaahidiana tu meet easter holiday, zile skukuu zinaongozana siku kama nne hvi, sasa nikakata zangu ticket presisheni ya go pekeake ilikua kama laki saba hivi, kurudi nitarudi zangu na tahmeed sio kesi,

Basi siku ya safari imefika naenda zangu airport kwa mbwembwe huku na ma whasap video kalling na mchuchu, naye alikua ndio yuko saluni anatengeneza nywele a bling bling aje kunipokea Jomo kenyata ashawapanga na mabeshte zake,

ile kufika airport tu mda wa check inn ulishapita na milango ishafungwa, mzee baba full kupanik omba sana wakaniambia ni amend ticket nipande ndege nyingine, nikamweleza mchuchu akaniambia nisimuongeleshe ye anachojua mi nafika leo yaani alishajikoki, Mzee nikatoka kwa nje pale mpaka kaunta ya presesheni na mkuta mdada, akaangalia akaniambia ndege ipo ya saa moja ila nafasi ilikuepo ni bizness klass!
Dooh nikacheki na mchumchu akaniambia yaani nisimuongeleshe kitu chochote na atashika simu tu nikiwa kwa ndege,

Mzee baba nikamuuliza niongeze ngapi dada mhudumu akajibu laki saba Halahaulaaaa!
Kulinda heshima nikaenda palekuna magari magari ya atm nikatoa akiba yangu nilioweka inilinde nikirudi nikavurua nikakata, ikabidi niisubirie palepale imagin toka saa tisa hadi saa kumi nambili!
Nguvu ya K
 
2015 iliwahi kunitokea kwenye msiba wa babu.
Babu yetu alikua na wake watatu hivyo kufanya wajukuu tuwe wengi sana kwa haraka haraka si chini ya 60.sasa ujinga wetu ni tunashirikiana kipindi cha misiba tu.

Pia tunamatabaka ya urafiki,wale ambao wapo fresh kiuchumi ndio marafiki,na wale wa kawaida ivo ivo hata kutembeleaba

Sasa mimi na dogo langu mmoja hivi(mtoto wa mana mdogo kwa bibi mwingine) tupo kivyetu tu,sio uchumi wala kielimu yani tunajijua wenyewe na ndio angalau tumeishi kule bush kwa babu hivyo kutufanya tuwe maarufu kuliko wengini huko kwa upande wa wanaume.

Ujinga ukanzia kwenye kunyonyoa kuku na kusaidia kazi msibani,ndugu zetu wanajifanya wa mjini et hata kunyonyoa kuku hawawezi,wanachofanya ni kutusifia tu mimi na hyo dogo et tunanyonyoa kuku vizuri.

Tukawa tunajiuliza na dogo je kunyonyoa kuku kuna utalamu gani,tukaona hapa ni ujinga,wao ni kufata vitu dukani na gari basi.tena kuna mgari fulan hivi mbovu ikifika time ya kuni,dogo anambiwa aliendeshe yeye.

Tukagundua kuwa hawa wanatuchukulia poa,tena enzi hizo hata hatuna ajira ila harakati zetu tunakula na kuvaa fresh bila kusumbua mtu na totozi tunahudumia.

Siku tunamaliza msiba ndio yalinikuta mazito.wakati wa kikao

Kuna dada yetu mtoto wake alikua anasomeshwa na babu,na sisita huyu aliishi pale baada ya kufeli life huko zambia,yani kifupi alikua ni mtu anaehitaji msaada na bila hivyo dogo asingefanya pepa.

Kutokana na matabaka yetu watu wakawa wazito kukunjua nafsi kumchangia dada hata ada dogo amalize shule mana alikua form four na pesa iliyobakia ni 1M tu.

Ili kuweka heshima nikanyosha mkono baada ya kuona ukimya,nikasema hili jambo si la mjadala kwakua huyu alikua anasomeshwa na babu,na babu kafariki na tumekuja kumzika,hatuwezi kuwa tumemsindikiza kwa aman kama vitu alivyoanzisha vinaishia pabaya na madume yote haya tupo,dada zetu wapo.

Nikatoa laki2 pale pale ,nikasema mimi naanzia,na wengine muendelee,

Wakashtuka hao,basi mchango ukaendelea pale na kunae mwamba huyo akasema hizo pesa mpen dada yeye atamsomesha.

Badae wakanza kuulizia siku hizi nipo wapi na nafanya nn,mara ooh chuo ulimaliza basi najibu kimwamba fulani.

Ila badae nilijuta sana mana pale pesa yangu ilikua 70k tu,zingine zilikua za boss wake dogo alimuagiza mchele tunaporudui dar.na hiyo 70 ilikua ya nauli ya kurudi dar.ilibidi tuombe mchele kwa ndugu na kudandia fuso wakati wa kurudi dar

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahahaha sana nimecgeka night kaleee
 
Nilikuwa na elfu kumi na tano mfukoni nikasema Leo acha nisumbue dalali wa viwanja na nyumba.
Nikamcheki dalali nikamwambia nahitaji kiwanja Cha Kati ya milioni 2 Hadi 4.
Akasema anavyo viwanja vingi ila kunitembeza gharama yake ni ten nikasema poa.
Kanitembeza weee kila kiwanja nasema sijaridhika nacho baadae kanipeleka kwenye kiwanja kibaya nikasema nataka hiki hiki[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].
Tukakubaliana kesho yake anitafute tufanye malipo ilivyofika kesho nikachomoa.[emoji2957][emoji2957][emoji2957][emoji2957]

Sent using Jamii Forums mobile app
Nyie watu khaaaa! Hahahaha
 
Inaitwaje hiyo lodge mkuu nkna safari huko j4
Inaitwa Gland Victoria mkuu. Ila kuna mkendo pia bei nafuu room kali tu
20230120_072652.jpg
 
Nilikua na 2000 tu alaf dem wa chuo nlietoka kumtongoza siku km 3 nyuma akaniambia hana vocha, nikasema mmh uyu nikimuonyesha unyonge mapema itakua jau, nikamuungisha bando la 1500 uku m nikabaki nawaza ntakulaje iyo siku.
 
hapo omba ukutane na mwanamke muelewa, vinginevyo anaharibu kabisa saikolojia yako
Hata huyu aliharibu sana. Akaanza kejeli ooh kwenye simu unajifanya mandingo kumbe huna lolote. Kidume nikakauka tu. Halafu jirani kulikuwa na show inapigwa ananiambia sikia wanaume huko.
Niliumia snaa
 
Ukiwa na uwezo wa kusema Hapana, maisha hayatakuwa magumu kamwe.

Sio lazima ujilazimishe uonekane tajiri wakati huna uwezo, utaishia kuaibika mwenyewe rohoni.

Kama kitu sina uwezo nako, naondoka kimya kimya mambo yasiwe mengi.

Hakuna haja ya kujionesha kwa watu nina uwezo ilihali sina. Na mbaya zaidi watu wenyewe siwafahamu na sitakaa nionane nao milele.
Nadhani haya ni mambo ya ujanani tu mkuu,usicomplicate sana.......japo una point
 
Back
Top Bottom