Uliwahi kuonesha jeuri ya pesa hata kama huna, ili kulinda heshima?

Uliwahi kuonesha jeuri ya pesa hata kama huna, ili kulinda heshima?

2015 iliwahi kunitokea kwenye msiba wa babu.
Babu yetu alikua na wake watatu hivyo kufanya wajukuu tuwe wengi sana kwa haraka haraka si chini ya 60.sasa ujinga wetu ni tunashirikiana kipindi cha misiba tu.

Pia tunamatabaka ya urafiki,wale ambao wapo fresh kiuchumi ndio marafiki,na wale wa kawaida ivo ivo hata kutembeleaba

Sasa mimi na dogo langu mmoja hivi(mtoto wa mana mdogo kwa bibi mwingine) tupo kivyetu tu,sio uchumi wala kielimu yani tunajijua wenyewe na ndio angalau tumeishi kule bush kwa babu hivyo kutufanya tuwe maarufu kuliko wengini huko kwa upande wa wanaume.

Ujinga ukanzia kwenye kunyonyoa kuku na kusaidia kazi msibani,ndugu zetu wanajifanya wa mjini et hata kunyonyoa kuku hawawezi,wanachofanya ni kutusifia tu mimi na hyo dogo et tunanyonyoa kuku vizuri.

Tukawa tunajiuliza na dogo je kunyonyoa kuku kuna utalamu gani,tukaona hapa ni ujinga,wao ni kufata vitu dukani na gari basi.tena kuna mgari fulan hivi mbovu ikifika time ya kuni,dogo anambiwa aliendeshe yeye.

Tukagundua kuwa hawa wanatuchukulia poa,tena enzi hizo hata hatuna ajira ila harakati zetu tunakula na kuvaa fresh bila kusumbua mtu na totozi tunahudumia.

Siku tunamaliza msiba ndio yalinikuta mazito.wakati wa kikao

Kuna dada yetu mtoto wake alikua anasomeshwa na babu,na sisita huyu aliishi pale baada ya kufeli life huko zambia,yani kifupi alikua ni mtu anaehitaji msaada na bila hivyo dogo asingefanya pepa.

Kutokana na matabaka yetu watu wakawa wazito kukunjua nafsi kumchangia dada hata ada dogo amalize shule mana alikua form four na pesa iliyobakia ni 1M tu.

Ili kuweka heshima nikanyosha mkono baada ya kuona ukimya,nikasema hili jambo si la mjadala kwakua huyu alikua anasomeshwa na babu,na babu kafariki na tumekuja kumzika,hatuwezi kuwa tumemsindikiza kwa aman kama vitu alivyoanzisha vinaishia pabaya na madume yote haya tupo,dada zetu wapo.

Nikatoa laki2 pale pale ,nikasema mimi naanzia,na wengine muendelee,

Wakashtuka hao,basi mchango ukaendelea pale na kunae mwamba huyo akasema hizo pesa mpen dada yeye atamsomesha.

Badae wakanza kuulizia siku hizi nipo wapi na nafanya nn,mara ooh chuo ulimaliza basi najibu kimwamba fulani.

Ila badae nilijuta sana mana pale pesa yangu ilikua 70k tu,zingine zilikua za boss wake dogo alimuagiza mchele tunaporudui dar.na hiyo 70 ilikua ya nauli ya kurudi dar.ilibidi tuombe mchele kwa ndugu na kudandia fuso wakati wa kurudi dar

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Aisee sio poaa...!!
 
Mimi ilikuwa sio kuleta heshima ila ilikuwa sifa.iko hivi nilienda dodoma kwenye harusi ya sista nilikaa meza moja na pisi kali 2 ukafika muda wa kuchangia bibi harusi kulikuwa na phase mbili,phase ya kwanza ilikuwa kikapu kinapita kwenye kila meza yoyote anaweka alichonacho'muda ule nilikuwa nipo tungi balaa kutaka kuonyesha sifa mfukoni nilikuwa na laki 8 nikawa naweka narusha rusha elfu 10 kwenye kapu mpaka laki 8 yote ikaisha.
Baadae wale wadada wakaniambia weee kaka pesa zote umetoa wapi mbona umechangia hela nyingi hivyo!! Nikawaambia kawaida kisha nikawapotezea.
Ikaja phase 2 kwenda kumtunza bibi harusi pale mbele ili kuonesha sifa nikaenda ATM nikatoa mil 1.5 pisi kali moja ikanishauri sana nisiende kuchangia tena pesa nilizotoa awali zinatosha.
Baada ya harusi kuisha asubuhi nikajikuta nipo room yenye muonekano kama hostel kumbe yule sista nilivyozima alinikokota mpaka chuoni kwao alikuwa ni mwanafunzi wa udaktari md5 akanikabidhi pesa yangu 1.5mil alizitunza coz nilikuwa tungi sana..kifupi huyo dada ndio mke wangu hivi sasa..sifa zilinisaidia kupata mke bora aliyekuwa yupo sealed
Kaka uongo sio kitu kizuri
 
Wakati fulani mwaka juzi nikawa na safari ya kikazi Musoma. Sikuwahi kufika Musoma kabla kwa hiyo sikuwa mwenyeji wa maeneo nilitegemea boda.

Nikashuka stend nikamwambia boda nipeleke lodge nzuri nzuri. Baadae nikaona nisichemke ngoja nimshirikishe mwenyeji wangu. Mwenyeji wangu sikuwa nafahamiana naye wala kuonana. Kwa vile alijua ile kazi ni ya kibosi sana akaamini natakiwa kulala hotel yenye hadhi. Akamwelekeza boda pa kunipeleka.

Kufika daaah, nakuta hotel kali ghorofq kadhaa nje napokelewa na mabendera ya nchi mbalimbali.

Nikamwambia bodaboda mmenileta cha kike. Muhudumu mrembo kabisa akaja kunipokea nikiwa mchavu vumbi na kabegi mgongoni kama nimetoka kuchimba mitaro.

Nikamwambia boda usiondoke lolote linaweza kutokea. Tayari muhudumu akawa amenihukumu kwamba sina uwezo wa kulala pale. Akaniambia lakini kaka hata chumba ni kuanzia elfu 50!

Nikamwambia mimi sijauliza bei nimeuliza chumba. Kufika reception kila mtu anaonyesha wasiwasi huyu mteja kapotea. Basi nikamwambia nataka chumba cha juu.

Akanijibu tuangalie tu vya chini kule juu ni kuanzia elfu 70. Nikaona aaaahhhh japo nilitaka chumba cha 20 ila hapa inabidi niweke heshima tu bila kujali chochote.

Nikachukue chumba cha 70. Nikarudi mapokezi kwenye watu wengi walionitilia mashaka. Nikaanza kulipa bills kwa sauti.

Nikawaambia sikilizeni, ninakaa siku 2 nitalipa 140,000 yote, halafu dada chukua buku 10, mlipe boda buku ya nauli na buku 4 ya kunisubiri. Halafu elfu 5 baki nayo umenipokea vizuri, lakini mwambie boda naomba namba yake.

Ndugu msomaji yote hayo niliyafanya kulinda heshima dhidi ya wajinga wachache ambao walinihukumu kwa mwonekano.

Lakini pia kujitabiria mambo makubwa mbeleni kwamba ipo siku nitakaa meza moja na wakuu, nitakula na wakuu na nitalala lodge moja na wakuu.

Je, ulishawahi kufanya jeuri ya pesa hata kama huna kingi, ili kulinda heshima yako au kujitabiria ukuu?!!
Hapo usikute ulienda kusambaza kinywaji chenu cha Mo xtra, au kutafuta wateja wa zile pikipiki zenu za boxer! Nahisi ulirudi mjini ukiwa huna hata 100!
 
Back
Top Bottom