Uliwahi kuonesha jeuri ya pesa hata kama huna, ili kulinda heshima?

Uliwahi kuonesha jeuri ya pesa hata kama huna, ili kulinda heshima?

Yule demu aliponipa mzigo tako tatu wadhungu hao. Nikasingizia sijala ngoja nile nimpe show za WWE John cena you can't see mee. Nikala chips ndizi mishikaki. Nikampq romance kupima oil naona huyu kashaiva nikachomeka kupiga take tatu wajapan hao. Nikaona sasa hapa mbona kazi sana. Nikaona ngoja nizuge zuge kuangalia vipindi vya wanyama kwenye TV. .

Alipoamka nikaona nitumie nafasi hii kumuonyesha show ya kibabe. Kupiga tako nyingine tani aisee wazee hawajakosea siku ya kufa nyani kweli miti yote huteleza. Kupiga tako nikajikaza yani kufika tako ya tano tu tena nimejikaza nikawa na uma na meno wahindi haoo. Aisee what an embarrassing day.

Kurudi kwenye mada, ili kurudisha heshima nikamuliza demu hivi unaishi wapi? Akajibu magomeni nimepanga chumba elfu 70. Nikaanza kujiongelesha hapa inabidi upange sinza chumba laki na hamsini. Nataka nikukipie kodi ya miezi kumi. Kwanza kabla sijasahau shika hii laki. Ukifika nyumbani nakutumia hela nyingine ununue vitu vya nyumbani hiyo laki ni nauli tu. Hata samsung unayotumia sio simu ya maana nakununulia iphone.

Alipoondoka na laki yangu nikatupa line nikasajili line nyingine kwa mpita njia. Huyu dada tulikutana kwenye mwendokasi. Hata mwendokasi sipandi tena nawasiwasi naweza kukutana nae huko [emoji51][emoji51][emoji51]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hii inakubalika kabisa, Mimi nilikua Kasulu, nikawa na mazoea kwenda Bar kuangalia mpira, Kila nikienda pale naagiza maji, basi wahudumu wakawa wananipotezea. Hawana mzuka wa kunihudumia.

Basi, nikarudi Tena nakumbuka ilikua game ya Simba, wakagoma kunipa hata Kiti, akanihudumia Dada mmoja hakua na makuu, kwa hasira nikaagiza Castle Light 20. Nikamwambia Kaa hapa, hizi ni za kwako na yule mwenzio aliyenihudumia Jana.
Hahahahaha [emoji2957] sometimes you got to fight to prove you're a Man (Kenny G)
[emoji23][emoji23][emoji23] kenny Rogers, huwa nawaachia tip wale walionihudumia vizuri.
 
Shida much know saaana😂😂😂😂, yaani ukiona hujawahi basi siku utawahi, na ikitokea hufanyi basi tu umekufa mapema.
Maana kujiona ipo katika maisha yetu ya kila siku. Iwe shuleni, msibani hata kwenye sherehe.

ana
Sawa...
 
Hii bwana ni Kwa hisani ya wife.

Wife hakupenda dharau toka Kwa mdada mwenzake,ilikuwa 2017 nilikuwa nimepanga kwenda shopping na wife akasema ananisindikiza na kuhakikisha napata viwalo freshi,na kama nilijua nilimpa hela akae nazo yeye Mimi kazi yangu ni kujaribu na kuchukua,ilikuwa bajeti kama 300,000.

Sasa wakati tunatoka Duka moja na kuingia lingine,yeye akawahi kutangulia Duka lingine kabla yangu,sasa kwakuwa alikuwa amevaa hijabu basi Yule sista duu WA shop akamchukulia poa kumbe hajui wife alikuwa duu hasa enzi zake Ila nilimbadilisha na kuwa mwanamke anayejistiri.

Wife akaniambia kuna mdada anamchukulia poa ngoja amuonyeshe Ila binafsi sikubariki wazo la wife lkn nikasema ngoja niwazoom nione itakuwaje,pale pamba ilikuwa bei kuanzia 15,000 mpaka 20,000.

Nikachagua kama pamba 4 ambazo nilizipenda wife akasema ongeza moja tulipe 100,000 chap basi kwakuwa nilijua wife anataka point tatu muhimu nikaona nisimwangushe,kweli ikapatikana ya tano wife akatoa 100,000 chap,mpaka hapo wife aliondoa dharau za Yule sista duu

Ni hayo Tu!
 
At least breakfast ya maana ulikuwa unafidia maumivu pia ukiwa lodge hiyo nahisi ni grand hotel jina lake ,ukipeleka pisi ukaiambia huna hela tukutane gorofani pub baadaye inakuelewa!.
Ndiyo hiyo Grand Victoria. Nilipata pisi ile night club ya kaghorofa pale junction. Ila nashukuru Mungu ilinitanguliza halafu haikutokea
 
Ilikuwa mwaka 2001 nasoma secondary nipo chalii.Nilipata zali nililamba pesa bahati na nasibu ya Coca cola (gurudu la bahati). Kama laki nane hivi..

Basi nilivaaa kikolo Sana siku hiyo. Picha linaanza nachuku tax kutoka Coca cola mikocheni mpaka kkoo. Nazama dukani kwa muarabu nataka kutungua raba mwarabu anajifanya hasikii ananiangalia kwa kuninyali. Nilipata ghadhabu.

Nauliza raba Bei gani ananiangalia huku anasomaa gazeti. Dadeki nilichukuaa pair tano laki mbili cash..
Mwarabu hakuaamini alibaki kudadisi ile pesa ajiridhishe huenda ilikuwa bandia.. Nikaitaa tax driver abebe aweke kwenye buti.... Nikasepa..
Daah dharau mwenzie jeurii[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Umenikumbusha leo wife amenipa stori ya kijijini kwao kuna ndugu anaumwa kalazwa hospitali. Anko wake akatumwa akauze ng'ombe hela ya matibabu ipatikane. Kauza laki 5 halafu akazima simu siku 3. Wakamsaka wanakuja kumkuta na laki 1 tu nne zote kapiga pombe na kuhonga
Anko ni fala sana,ujute nae aliweka heshima

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2015 iliwahi kunitokea kwenye msiba wa babu.
Babu yetu alikua na wake watatu hivyo kufanya wajukuu tuwe wengi sana kwa haraka haraka si chini ya 60.sasa ujinga wetu ni tunashirikiana kipindi cha misiba tu.

Pia tunamatabaka ya urafiki,wale ambao wapo fresh kiuchumi ndio marafiki,na wale wa kawaida ivo ivo hata kutembeleaba

Sasa mimi na dogo langu mmoja hivi(mtoto wa mana mdogo kwa bibi mwingine) tupo kivyetu tu,sio uchumi wala kielimu yani tunajijua wenyewe na ndio angalau tumeishi kule bush kwa babu hivyo kutufanya tuwe maarufu kuliko wengini huko kwa upande wa wanaume.

Ujinga ukanzia kwenye kunyonyoa kuku na kusaidia kazi msibani,ndugu zetu wanajifanya wa mjini et hata kunyonyoa kuku hawawezi,wanachofanya ni kutusifia tu mimi na hyo dogo et tunanyonyoa kuku vizuri.

Tukawa tunajiuliza na dogo je kunyonyoa kuku kuna utalamu gani,tukaona hapa ni ujinga,wao ni kufata vitu dukani na gari basi.tena kuna mgari fulan hivi mbovu ikifika time ya kuni,dogo anambiwa aliendeshe yeye.

Tukagundua kuwa hawa wanatuchukulia poa,tena enzi hizo hata hatuna ajira ila harakati zetu tunakula na kuvaa fresh bila kusumbua mtu na totozi tunahudumia.

Siku tunamaliza msiba ndio yalinikuta mazito.wakati wa kikao

Kuna dada yetu mtoto wake alikua anasomeshwa na babu,na sisita huyu aliishi pale baada ya kufeli life huko zambia,yani kifupi alikua ni mtu anaehitaji msaada na bila hivyo dogo asingefanya pepa.

Kutokana na matabaka yetu watu wakawa wazito kukunjua nafsi kumchangia dada hata ada dogo amalize shule mana alikua form four na pesa iliyobakia ni 1M tu.

Ili kuweka heshima nikanyosha mkono baada ya kuona ukimya,nikasema hili jambo si la mjadala kwakua huyu alikua anasomeshwa na babu,na babu kafariki na tumekuja kumzika,hatuwezi kuwa tumemsindikiza kwa aman kama vitu alivyoanzisha vinaishia pabaya na madume yote haya tupo,dada zetu wapo.

Nikatoa laki2 pale pale ,nikasema mimi naanzia,na wengine muendelee,

Wakashtuka hao,basi mchango ukaendelea pale na kunae mwamba huyo akasema hizo pesa mpen dada yeye atamsomesha.

Badae wakanza kuulizia siku hizi nipo wapi na nafanya nn,mara ooh chuo ulimaliza basi najibu kimwamba fulani.

Ila badae nilijuta sana mana pale pesa yangu ilikua 70k tu,zingine zilikua za boss wake dogo alimuagiza mchele tunaporudui dar.na hiyo 70 ilikua ya nauli ya kurudi dar.ilibidi tuombe mchele kwa ndugu na kudandia fuso wakati wa kurudi dar

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimechagua kucheka 🤣🤣🤣 utanisamehe kwakwel..
 
Back
Top Bottom