Uliwahi kuonesha jeuri ya pesa hata kama huna, ili kulinda heshima?

Ukiwa na uwezo wa kusema Hapana, maisha hayatakuwa magumu kamwe.

Sio lazima ujilazimishe uonekane tajiri wakati huna uwezo, utaishia kuaibika mwenyewe rohoni.

Kama kitu sina uwezo nako, naondoka kimya kimya mambo yasiwe mengi.
Mi huwa nina mtindo wa kuuliza bei ya kitu kabla sijakinunua.
Kama bei kubwa naondoka.
Kuna sehemu sitaki hata uliza bei
 
Siku nipo zangu JNIA nimetoka Istanbul, kuna dada nilimuona Airport na Transit Cairo nilimsalimia mara zote mbili ila akanyuti..

Basi tulipotimba Daslam majira ya saa tisa unusu to kumi alfajir, baada ya kuzoazoa mabegi tukafika ukaguzi belt tukaambiwa tuingie room ya TRA mmoja baada ya mwingine.

Tulijikuta tumefika wakati mmoja, yeye kaanza kaingia, baada ya muda anatoka na bill huku analalama hana pesa, ananiangalia kwa huruma.

Nikaingia, nikamsomesha afisa pale, nilishaanda mpango wa how ningeshushaba bei.

Nikatoka kiroho safi kuelekea NMB ya ndani,kufanya malipo namkuta manzi anatia huruma kama anataka kuniongelesha, nikarudi kwa afisa kukabidhi risiti, ile nataka kutoka manzi akaja kuniomba nimsaidie njuruku zimepungua, blah blah za kulalalama.

Nikamuuliza ilikuwaje, kumbe kajimwambafai pale kwa afisa, kataja mabei makubwa makubwa bila ya risiti wakati pochi ya 100$ tunasema hata 10$.

Nikamwambia tatizo hamsalmii watu, nikampa pesa ya kuongezea kama 50$,nikachukua namba nikawekeza..
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Daaahhh, nimecheka hatari, nimeisoma huku nikivuta taswira jinsi walivyokuchukulia halafu ukawageuzia kibao
 
Alaa alaa!
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Daaahhh
 
Dah... Mkuu salasala chimbo gani hilo soda aftatu Aiseee... mimi huku ndo home.. nipe code nikaweke heshima!! Au ulishuka chini kule mitaa ya lamada?
 
Nimewahi kuchoma laki nane kwa sifa za kijinga sana Mwaka juzi, roho iliniuma sana sana.. yaani iliniuma kiasi kwamba kesho yake nikaamua kutoa hela zingine nisafiri tu kuupoza moyo.
 
Ujinga mtupu.
 
Mimi ndo nipo nasumbua ndugu hapa wanikopeshe walau alfu kumi.

Hii ni baada ya kulipia bili za watu wote niliowakuta mgahawani jana
Kwa tsh 86500.

Ni stori ndefu kidogo lakini tu kiufupi dharau zinaumiza sana.
Teh teh...
 
Castle lite 20 ni Tsh elfu 30.
 
Very interesting
 
Dah mi nakumbuka kuna mwanangu alinialika kigamboni tupate bia mbili tatu nikatimba asee apo ni camp joint,nikakuta kimewaka yuko na jamaa zake kama nane wanamalizia malizia bia zao namimi nkapiga kama mbili hivi nilizozikuta tukahamia the Giant asee ile siku nikijikuta natumia laki tatu ila kuendana nao make jamaa yangu alikua ananitambulisha kama mtu mkubwa fulani hivi bas namimi sikuwaangusha ila nilipata homa kwa hasara ile.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
2016 nikiwa mtumishi wa taasisi fulani hivi,ilitokea tu nikawa sina smartphone,sasa kijiweni ninaposhinda nikawa nagongea simu,kuingia jf,twitter insta nk,mpaka kubeti.
Siku moja nadhani mwenye simu alifikwa hapa(waswahili wanasema)akaropoka[emoji28][emoji28].
Aisee wewe ni mtumishi smart imekushindaje bana??daily unagongea simu yangu inachemka[emoji28],aisee wengine njia ya kupokea taarifa mbaya za ghafla huwa tuna tabasamu.
Kinyoonge asishtuke kama nimekwazika,nikamwambia tulia namalizia ishu moja,nakupa.
Kesho yake ilibidi nivunje kibubu kwa hasira kwa mara ya kwanza nikaenda kujitwisha iphone ya kwanza kutoka shop(iphone 6plus) ikiwa bado inafuka moshi kipindi hicho 1.6mln.asubuhi nafika pale anashangaa nina simu yenye bei mara 5 ya kwake,akatoa macho tu na kuanza kujaribisha camera.

Binaadam wanatia hasira lakini tunawashukuru maana wamefanya wakati mwingine kwa kauli zao,tuondoke kwenye comfort zone zinazotulemaza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…