Uliwahi kupata mikasa gani kwa kuishi kwa ndugu?

Tuambie sasa ukweli ni upi?

Wewe wa kishua au choka mbaya??

Maana naonaga unatunywesha sana chai humu.

Mara utuambie una plan kufungua duka la vipodozi, mara una plan kuuza kitimoto na kufungua ki pub.
Hahahah mzee unahangaika mno halafu haitakusaidia 🤣 wanaonijua wanaelewa huu sio ubao wa matangazo
 
Mwambie mumeo ampangie chumba,
 
Watoto wao wapo kwenye Hali gani sasa?
 
Aisee,pole sana mawifi ni janga sana,kwani so aende kwao.
 
Sahihi kabisa.
 
Mmmmh wewe ni balaaa
 
Baadhi ya wanawake hawana aibu kabisa yuko radhi afiche chakula hata kama kitaoza ndani.
 
Hahahhahahahhahahah
 
Bora nyie mlinyanyaswa na mashemeji zenu...
Miaka fulani ya nyuma nilimtembelea ndugu yangu maana alikuwa analalamika sifiki kwake.

Nikapewa chumba nyumba ndogo ya nje ambayo alikuwa anakaa bro na mke wake ila chumb changu kinajitegemea tofauti kabisa na jamaa, hata choo nilikuwa namtumia cha nje ila jamaa kwake ilikuwa ni master bedroom.

Sasa huo usiku mkojo umenibana, ile natok nje tu nakutana na 2 grown Dobermanns with cropped ears na mwingine hadi mkia amekatwa[emoji15][emoji15]. I was like hee kumbe humu ndani kuna mbwa tena wakubwa hivi na hawaniambii hawa si wauwaji kabisa kwa kweli sikupenda[emoji1787][emoji1787]. Ikabidi nirud geto, nikampigia simu bro akaja akawashika mbwa nikaenda msalani.

Ilikuwa kero maana karibia kila siku nampigia jamaa anisindikize chooni kama mtoto mpaka jau, jamaa akanipanga hawana shida hao wakishakuzoea. Kesho yake nikawa nipo nao karibu tunacheza nao mixa wanapewa maelekezo wanizoee, yule mmoja alinirukia yani over nilitupiwa kakiroba cha kilo 50!! Nilipata ka upenyo nilijikuta nasepa ka upepo, yule mbwa anakuja nyuma ananikimbiza, anadhani tunacheza kumbe mwenzie ndio nasevu hivo[emoji1787][emoji1787]. Ilifika wakati ikifika kuanzia saa 9 au kumi sinywi maji mpaka kesho yake!

Sasa huo usiku nataka kwenda chooni kama kawaida, ile nafungua mlango tu yakanyanyuka masikio yamewasimama kama antenna yani kama washajiandaa kwa kitu fulani so alerted, nikasema hapana nikarud ndani pigia sana bro simu haipatikani. Mkojo unazidi kubana na ndani hakuna hata chupa. Nikachungulia tena nikawaona wako mbali kidogo nikachomoka kama mkuki mpaka chooni, yalikuja kwa kasi yakaanza kuparua mlango. Wakat nataka nirudi nkayaona yamesimama kwa mbali kidogo yapo serious sio mchezo, nikayachekiii nikaanza kuambaa ambaa na fence kuutafuta mlango wa geto, nayo yakaanza ku move kunifata. Nikajisemea hapana hii sio ishara nzuri nikarudi mbio mpaka chooni, majamaa yakaja speed mpaka pale mlangoni yanaunguruma mixa kuparua mlango.Nilienda na simu chooni, piga sana simu ya jamaa haipatikani nikajisemea leo nimeisha[emoji16]. Nikavuta ndoo ya chooni nikakaa kuanzia saa 9 hivi kuelekea 10mpaka 12 hadi nikapitiwa na usingizi na ile baridi sio poa. Nashukuru Mungu choo kilikuwa kisafi.

.......hapo sijaelezea tukio lengine la kukimbizwa na hao mbwa kidogo ning'atwe hawakuwa wamefungwa vizuri plus kukojoa mlangoni.....

Asubuhi baada ya kuyafungia namimi ndio nikajifanya natoka chooni, yule mzee akaniuliza umeingia chooni saa ngap sijakuona?! I was pissed off sikutaka hata kumwambia yaliyonikuta maana mjadala ungekuwa mrefu na sikuwa n huo mda wa kuanza kuoneana huruma, kwanza nausingiz/kichwa kinauma na hapo nafikiria kama naweza pata bus la saa mbili au la[emoji1787]. Jioni yake nikaaga kesho narud kwetu, mzee akamaind sana akapiga simu nyumbani sikubadili maamuzi. Kesho yake asubuhi nikasepa!

Zile siku chache nilizokaa pale ndani zilikuwa ni mateso, wale mbwa walinikosesha raha kabisa hasa usiku. Maana mda wote ilibidi niangalie huku na huku nijue wako wapi kabla sijafanya movement kama vile navuka barabara maana wana eneo kubwa. Na hadi leo sijawahi kwenda tena!
Japo niliwapendea ile tough and aggressive looking yao lakini haiondoi ukweli kwamba mimi na mbwa bado haziivi kivileee.

 
Nikiwa darasa la kwanza nilisingiziwa kusudi kuiba sh.400 au 200 lengo niondoke nimpunguzie mke wa mjomba mzigo wa kulea, Yule mbwa simpendi hadi Leo na anajua hata kwake sigusi napita road tu basi. Sana sana naenda nakaa kwenye kaburi la uncle kipenzi changu kama kumsamilia uncle basi nasepa
 
Sasa mkuu ulishindwa nn hata kutayarisha chupa Usiku kabla yakulala napo ulikua unazembea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ili nawewe ukavuruge ratiba ya msosi ya wifi yako hahahahaha
 
Mume anayefanya hayo sio bure atakuwa na matatizo. Au ndugu wa mke hawana nidhamu.
Hapana ni uchoyo tu, kuna ile mke akipata shida ni atajua mwenyewe yeye kaoa mke mmoja si ukoo, hivi mke anajiskia vipi kuhudumia ndugu wa mme!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…