Uliwahi kupata mikasa gani kwa kuishi kwa ndugu?

Ukienda kuishi kwa kaka yako na wewe huko utakuwa ndugu wa mume, je uje kujadiliwa hapa kuwa ndugu wa mume ni mbaya au wewe utakuwa ndugu wa mume mwema?
 
Sawa ila usitoke hapo angalia njia ya kumtoa yeye
 
Duu ndoa yake imemshinda anataka kuvuruga na yakaka yake, itoshe mtu kaachika arudi kwa Baba yake sio kwa ndugu, kam wazazi hawapo lakini nyumba ipo aishi hapo sio kusumbua ndoa za watu.
 
Watu hawakatai ndugu, sema ndugu ukifika nyumba ambayo inawenyewe na serikali yao tulia na fuata ratiba zao walizojiwekea sio eti kwa kaka unaanza kujifanya mjuaji wakati yeye mwenyewe ndoa imemshinda
 
Arudi kwake asikukaushe koo, ndugu yake umejaribu kumshirikisha? Ila utaambiwa mbaya maana mawifi nao tunajijua wenyewe.
 
Roho mbaya tu, wanawake
 
daah sikuelewaa mwanzooo 😀 😀 😀
 
WANAWAKE NI MASHETANI! tusisingizie udini... nyumba yoyote ugomvi huletwa na Chakula 😔
Ni uchoyo tu wa mtu hasa wanawake. Katika vitu ambayo sina uchoyo navyo ni vyakula
Naishi na ndugu zangu wa 5 ( watoto wa dada 3 ,wa kaka 1 na mjukui wa dada 1) . Huwa nanunua kila kitu ,kama siku hiyo hamna mboga naacha 10k. Huwa sipangii mtu muda wa kula, chakula kikipikwa kila mtu ana uhuru wa kula muda anaotaka. Na kwa muda wote huo tunaishi kwa furaha kabisa. Nilishawahi ishi na jamaa wa rafiki kwangu na sikuwahi kupangia mtu kazi etc. Utajiongeza mwenyewe ukiwa kwangu. Kwa uhuru ninaowapa, ukifika home kila kitu kipo safi. TV hata wakeshe wanaangalia watajijua wenyewe na usingizi wao. Sitaki stress ambazo hazina mashiko.
 
Punguza baje kwenye manunuzi ya chakula na msiache pesa
 
Kwani huyo wifi yako yeye hana kwao kwa wazazi wake?
 
Mahusiano yenu yapoje kwa sasa mnawasioiana?
 
Kwakweli mm milipata shida sana utotoni kutokana na kitolelewa na mama mzazi kwa kipindi kirefu,shida za kunyimwa chakula nimezipitia sana tu ndo maana nimekuwa makini sana nyumbani kwangu kuhakikisha hakuna manung'uniko ya chakula,naogopa sana kusikia mtu anakaa kwangu halafu hali vzr si dada wa kazi wala ndugu,na mke wangu namwambia kila siku ukitaka tugombane basi nisikie malalamiko kuhusu chakula haijalishi nani analalamika,manung'uniko yanaondoa baraka ndani ya nyumba!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…