Uliwahi kupata mikasa gani kwa kuishi kwa ndugu?

Pole ila hapo unatakiwa uwe mkali vinginevyo ndoa itakushinda hakuna mafahali wawil we ndo unatakiwa uwe na maamuzi ya Nini kinapikwa kulingana na budget Yako na ratiba ifatwe ilo jiko ni lako lake ameliacha kwa mume wake sasa asikuingilie na usiongee na house girl ongea nae mwambie wifi naomba nikipanga ratiba ya chakula ifatwe Bora lawama kuliko fedheha na hivyo ndo atakuheshimu na ukipata mgeni wa hivyo siku nyingine siku ya kwanza tu akibadilisha ratiba unamuwahi unamuweka sawa ila kama hivyo akishazoea kujipangia ni changamoto
 
ila na wewe ukalete fujo kwa mke wake sio?
 
KONGOLE kwako! 👊🏾👍🏾

Mwenyezi mungu azidi na aendelee kukufungulia rizq na moyo swafi, mwema na tulivu vivo hivyo!
 
Huyo alikuwa kiboko, yaani sipati picha dah!
 
Kiufupi kama mzazi una uwezo wa kutunza mtoto wako basi Kaa naye umtunze usimpeleke kwa ndugu unless kuwepo na sababu maalumu ya kumpeleka mtoto kwa ndugu,
Vinginevyo kinachotokea n chuki baina ya huyo mtoto na ndugu.
Kukaa kwa ndugu ni Kero sana hasa upande wa wanawake Wana roho mbaya sana sitaki kusema ila yote nasemehe maisha mengine yaendelee
 
Wanawake washamba ndio wana tabia hizo 🤣
 
Hahahah njaa njaa ndio mbaya sana 🤣 sema pia roho ya mtu tu! Wanawake wengi ni wabinafsi by nature!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…