Uliwahi kupata mikasa gani kwa kuishi kwa ndugu?

Uliwahi kupata mikasa gani kwa kuishi kwa ndugu?

Sijui kama umenielewa, huyu wifi yangu katoka kwa mume wake kaja hapa kwa kaka yake kuishi.ishu inayokuja kwa mfano hapa kwangu nina ratiba ya chakula asubuhi mchana na jioni,asa utakuta ratiba yangu jioni ni kupika hiki yeye atapika kile,hafu maagizo yote hela huwa namuachia binti wa kazi lakini ukirudi ulicho tegemea kukuta sicho kuuliza ooh aunt kasema tupike hiki. Kwahiyo ni kama anataka niishi apendavyo yeye.na sio kama hivyo vingine yeye hatumii hapana anatumia ila fujo tu.hapo bado atapika sufuria kubwa la chakula kesho unakikuta kwenye dustbin.haya asubuhi ataamka atapika chai ya rangi hapa kwangu kuna bili ya maziwa bado atapika na uji[emoji849] sio kama anamtoto wala hanyonyeshi siku mbili kilo ya sukari kwisha. hapo sijazungumzia mafuta,huwa nanunua viazi kwaajili ya chai lakini yeye kila siku asubuhi atapika chips anywe na chai,asa nakuta mafuta hayakai vile nlivyokusudia kumuuliza dada mnatumiaje mafuta aunt anapika chips kila mara asubuhi.na sio mjamzito .sawa kwake alikuwa yeye pekeyake na mume wake huenda alikuwa anaishi hivyo lakini mimi ninafamilia na sio kama tumetusua maisha jamani mimi na mume wangu wote ni wahanga wa ajira tuko mtaani tunaunga unga tu na tumepanga bado kwanini haelewi? Kila pesa tunayoipata tunaipangilia sana
Pole ila hapo unatakiwa uwe mkali vinginevyo ndoa itakushinda hakuna mafahali wawil we ndo unatakiwa uwe na maamuzi ya Nini kinapikwa kulingana na budget Yako na ratiba ifatwe ilo jiko ni lako lake ameliacha kwa mume wake sasa asikuingilie na usiongee na house girl ongea nae mwambie wifi naomba nikipanga ratiba ya chakula ifatwe Bora lawama kuliko fedheha na hivyo ndo atakuheshimu na ukipata mgeni wa hivyo siku nyingine siku ya kwanza tu akibadilisha ratiba unamuwahi unamuweka sawa ila kama hivyo akishazoea kujipangia ni changamoto
 
Duh ila ndugu wa mume jamani kuishi nao yataka moyo.nimekuja kugundua kwanini watu wengi wanaishi na ndugu zao kuliko ndugu wa mume.nikiishi na mdogo wangu namtuma nitakavyo hata nguo zangu nampa anifulie hutomsikia kunung'unika, ndugu wa mume mtume hata mara moja ukoo wao mzima watajua . Nako hapa naishi na wifi yangu kaachika kwa mume wake yaani ni kero jamani nyumba imekuwa kama na wanawake wawili mimi napanga kipikwe hiki yeye anapika kile mavyakula anapika mengi anaishia kumwaga yaani ilimradi fujo.hapa napanga na mimi niondoke niende kuishi kwa kakaangu
ila na wewe ukalete fujo kwa mke wake sio?
 
Ni uchoyo tu wa mtu hasa wanawake. Katika vitu ambayo sina uchoyo navyo ni vyakula
Naishi na ndugu zangu wa 5 ( watoto wa dada 3 ,wa kaka 1 na mjukui wa dada 1) . Huwa nanunua kila kitu ,kama siku hiyo hamna mboga naacha 10k. Huwa sipangii mtu muda wa kula, chakula kikipikwa kila mtu ana uhuru wa kula muda anaotaka. Na kwa muda wote huo tunaishi kwa furaha kabisa. Nilishawahi ishi na jamaa wa rafiki kwangu na sikuwahi kupangia mtu kazi etc. Utajiongeza mwenyewe ukiwa kwangu. Kwa uhuru ninaowapa, ukifika home kila kitu kipo safi. TV hata wakeshe wanaangalia watajijua wenyewe na usingizi wao. Sitaki stress ambazo hazina mashiko.
KONGOLE kwako! 👊🏾👍🏾

Mwenyezi mungu azidi na aendelee kukufungulia rizq na moyo swafi, mwema na tulivu vivo hivyo!
 
Wamama wa kipare shikamoo.
Kuna jamaa walikuja Dar kwa baba Yao mdogo ambaye ameoa mpare. Sasa huyo mama alikua hapiki mpaka mume wake arudi jioni kabisa. Vijana wakajiongeza wakamwambia baba mdogo kwamba wanashinda njaa, kula Ni mpaka baba arudi.
Baba mdogo akawaambia, hapa Ni kwenu, sio msubiri mpaka mama apike. Ukiona mama Yuko bize, ingia jikoni pika, kula OSHA vyombo.
Dogo wakawa wanatanya Kama walivyoagizwa. Siku mbili nyingi, mpare akawa anahifadhi vitu muhimu vya kupika chumbani kwake akijua kabisa Mila haimruhusu kijana wa kiume kuingia chumba Cha mzazi.
Huyo alikuwa kiboko, yaani sipati picha dah!
 
Kiufupi kama mzazi una uwezo wa kutunza mtoto wako basi Kaa naye umtunze usimpeleke kwa ndugu unless kuwepo na sababu maalumu ya kumpeleka mtoto kwa ndugu,
Vinginevyo kinachotokea n chuki baina ya huyo mtoto na ndugu.
Kukaa kwa ndugu ni Kero sana hasa upande wa wanawake Wana roho mbaya sana sitaki kusema ila yote nasemehe maisha mengine yaendelee
 
Kuishi kwa ndugu jau sana nakumbuka nilikuwa kwa uncle maisha yalikuwa mazuri skatai ila kuishi na mkewe ndo kazi picha linaanza asubuhi kuoga sabuni anakuwa kaifungia chumban kwake ili kuhepusha usumbufu muda mwingne unanunua yakwako unaoga akijua una yakwako kelele zinakuwa nyingi

Bas kwakuwa ofcn na hm sio mbali sana anasema kamavp ukiwa unafka muda wa msos unakuja unakula then unarud muda ukifika ukienda anasema mbn mapema sana hata hatujapka hapo ni saa 9 kumbe washakula na watoto wake na ndugu zake siku ukisema nisiende anamwambia uncle mbn siendi kula mchana dooh kazi kweli

Wakija wageni wa nyumbani anajifanya malaika hapo ndo utaona ana-care sana mara hv mara vile kujionesha ni mwema wakiondoka mwendo ni ule ule

Siku zingne unatoka ofcn usiku unakuta wanakula let say ugal utasikia mke wa mjomba anasema dah umechelewa kdg tulikuwa tunamalizia kula msos wako uko kwenye sahan hapo yale mabaki yake na watoto wake ndo nile had now nilitoka [emoji19]!!
We mwanamke popote ulipo asante ntakuletea zawadi
Wanawake washamba ndio wana tabia hizo 🤣
 
Chanzo Cha yote hayo ni njaa hukosefu wa chakula .

Mimi Nina kilo miatano za mchele na gunia mbili za maharage na Nina pesa za Mboga Sasa ukija kwangu kunitembelea huwezi kugombana na mtu .


Wanawake wana njaa Sana Mnabidi kulifahamu hilo Kama hauna chakula Cha kutosha usimlete ndugu ikiwa unakaa na Mwanamke ataishia kumnyanyasa Mimi nimejionea haya Mambo Nina ndugu yangu yeye anakaaga na vyakula magunia Mengi ya kutosha Sasa pale kwake ndugu wa mke na wa Mume wanakula na kusaza huwezi kuona ugomvi ukitokea Sasa njoo huku kwa Hawa sijui Mwalimu sijui nurse sijui nani huko pamoto Sana.
Hahahah njaa njaa ndio mbaya sana 🤣 sema pia roho ya mtu tu! Wanawake wengi ni wabinafsi by nature!
 
Back
Top Bottom