Uliwahi kusikia story gani kuhusu Said Salim Awadh Bakhresa?

Ana gari nyingi mpaka hajui idadi yake,nilikuwa nakataa kabisa kipindi naambiwa kwenye story kule kijijini,maana kusikia mtu ana magari ilikuwa ni habari achia kua na magari usiyofahamu idadi yake.

Baada ya kuja mjini ndipo nikajua kumbe sio uongo,na si yeye tu mabosi wengi wanapishana na gari za kampuni zao ambazo hawajui zimenunuliwa lini.
 
Usiseme Muongo, sema naamini tofauti na unavyoamini..!

Weka uthibitisho wako Mezani na mimi ntaweka wangu Ubaoni.
Ni kwamba wewe umehitimisha kuwa usipofanya biashara za magendo na kukwepa kodi hauwezi kutoboa ndio maana nakuambia wewe ni muongo
 
Wanasema 50% ya huo utajiri ni wa mzee arijojo yule watoto wake sasahivi ni namba moja wetu.
 
Pembe za ndovu, kutakatisha,ukwepaji Kodi ...

Ukideal na wakuu huta lala njaa!
 
Ni kwamba wewe umehitimisha kuwa usipofanya biashara za magendo na kukwepa kodi hauwezi kutoboa ndio maana nakuambia wewe ni muongo
Ndo nikasema hivyo ndo ninaamini, na ninao Uthibitisho wa Watu wengi tu waliofanikiwa kwa njia hizo 3 nilizozitaja!

Sasa wewe kama unayo hoja tofauti weka Mezani hapa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…