Uliwahi kutamkiwa neno gani baya na Mwalimu wako?

Baadhi ya walimu kuanzia Shule ya Awali na Msingi,Sekondari na hadi Chuo wamekuwa na tabia ya kutamkia watoto maneno makali na yenye kukatisha tamaa.

Mojawapo ya Maneno hayo ni kama “Hutaweza kufanikiwa hata siku moja”.

Wakati mwingine maneno hayo huwafanya wanafunzi kujiona wanyonge na kukata tamaa katika masomo yao na kusababisha baadhi yao kushindwa kutimiza ndoto zao.

Lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida wanafunzi wengi wakimaliza masomo baadhi yao hufanikiwa na kuajiriwa katika Taasisi, idara, Mashirika na sehemu nyingine kama hizo.

Walimu hufika kuhitaji msaada na kuwakuta wanafunzi wao waliowatamkia maneno makali wakitoa huduma katika sehemu hizo.

Wakati mwingine husaidiwa lakini pia wakati mwingine hukutana na Vikwazo kutokana na yale waliyoyatenda nyuma.

Walimu tujifunze tuache kuwa wakatili na kutoa kauli kali kwa Mtoto ili kesho yenu iwe Bora zaidi.
Usiwaamini waalimu, ni waongowaongo sana.
Walikuwa wananiita eti mimi ni kichwa nitafika mbali, matokeo yake nauza mabungo. Labda kama walimaanisha kufika mbali kiumri yaani kuishi miaka mingi yenye msoto duniani.
 
Teacher Mary wa English form 1 alinisusua mbele ya wanafunzi wenzangu ati nimepaka shadow wakati ni mishipa ile ya green kwa sababu ya weupe wangu inaonekana waziwazi. Mwishowe aliniambia nisipoacha kujipodoa nnapoenda shule ntaishia majutooo. Ntakuja kulia kama mbwa mdomo juuu 🤣. Ila katika mtu asiejua kukasirika wala kununa mmoja mie. Yule mwalim wala sikumuwekea kinyongo badala yake alikuja kuwa rafiki yangu na alijua kuwa sikuwa najipodoa kumbe na ubyuti nature tu
 
Baadhi ya walimu kuanzia Shule ya Awali na Msingi,Sekondari na hadi Chuo wamekuwa na tabia ya kutamkia watoto maneno makali na yenye kukatisha tamaa.

Mojawapo ya Maneno hayo ni kama “Hutaweza kufanikiwa hata siku moja”.

Wakati mwingine maneno hayo huwafanya wanafunzi kujiona wanyonge na kukata tamaa katika masomo yao na kusababisha baadhi yao kushindwa kutimiza ndoto zao.

Lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida wanafunzi wengi wakimaliza masomo baadhi yao hufanikiwa na kuajiriwa katika Taasisi, idara, Mashirika na sehemu nyingine kama hizo.

Walimu hufika kuhitaji msaada na kuwakuta wanafunzi wao waliowatamkia maneno makali wakitoa huduma katika sehemu hizo.

Wakati mwingine husaidiwa lakini pia wakati mwingine hukutana na Vikwazo kutokana na yale waliyoyatenda nyuma.

Walimu tujifunze tuache kuwa wakatili na kutoa kauli kali kwa Mtoto ili kesho yenu iwe Bora zaidi.
Eti aliniambia nitakuwa mwenyekiti wa CCM kijijini kwetu. Nikawaza huyu mwl ananionaje aiseee kiasi cha kunihusiha na chama cha majizi na mafisadi duniani.
 
Teacher Mary wa English form 1 alinisusua mbele ya wanafunzi wenzangu ati nimepaka shadow wakati ni mishipa ile ya green kwa sababu ya weupe wangu inaonekana waziwazi. Mwishowe aliniambia nisipoacha kujipodoa nnapoenda shule ntaishia majutooo. Ntakuja kulia kama mbwa mdomo juuu 🤣. Ila katika mtu asiejua kukasirika wala kununa mmoja mie. Yule mwalim wala sikumuwekea kinyongo badala yake alikuja kuwa rafiki yangu na alijua kuwa sikuwa najipodoa kumbe na ubyuti nature tu
Awww 😅😅😅😅ulikua ni wivu tu 😅
 
Usiwaamini waalimu, ni waongowaongo sana.
Walikiwa wananiita eti mimi ni kichwa nitafika mbali, matokeo yake nauza mabungo. Landa kama walimaanisha kufika mbali kiumri yaani kuishi miaka mingi yenye msoto duniani.
😅😅😅😅😅
 
I'm not perfect ila nafanya kazi katika ufanisi mkubwa ninaowaudumia wanasema wenyewe, ila point ni kwamba usimuhukumu mtu mapema mpe muda unaweza kukataa jiwe walilolikataa waashi likawa jiwe kuu la pembeni.
👏🏻👏🏻
 
Mwl wa physics alinitoa darasa la wanafunzi wanaosoma masomo ya science kwasababu sikuwa napaform vizuri somo lake, bahati mwalimu wa chemistry alipita akauliza huyo vipi Tena?
Baada ya maelezo akatoa maoni kuwa nafanya vizuri sana kwenye somo lake kwaiyo tusimpoteze huyu mtoto tumsaidie tu kidogo.
Kwasasa Mimi ni daktari nauliza hapa ni wapi??
😅👏🏻👏🏻
 
Back
Top Bottom