Restless Hustler
JF-Expert Member
- Apr 9, 2017
- 5,150
- 20,025
Waovu hawazaliwi wakiwa hivyo bali ni matokeo ya uminywaji wa haki na Uonevu katika Jamii. Hata magaidi au wanaotekeleza mauaji ya kinyama, lazima Kuna sababu nyuma yao.
Miaka ya nyuma nilienda shuleni kuchukua cheti Cha O-level. Nilfunga bahasha kwenye baiskeli nikawa nikiendesha speed. Kuna wazee niliwakuta tunafahamiana, Kati yao kulikuwa na mmoja ana mgogoro wa shamba na familia yetu, alikuwa anang'ang'ania shamba letu na anakiri wazi kuwa anafanya hivyo kwa sababu hayupo tayari kuona mjane akiwa na ardhi kubwa Kuliko yake.
Nikaona hakuna haja ya kusalimia, nikawapita kwa kasi kufika mbele nikagundua nimedondosha bahasha yenye cheti! Nikaanza safari ya kurudi taratibu kwa mguu huku nikiangalia barabarani kwa umakini kama nitaona bahasha.
Ghafla nikakutana wa wale wazee halafu lile zee lililokuwa lina mgogoro wa shamba na familia yetu ndilo limeshika cheti changu anakisoma huku anawaambia wenzake "watoto wote wa huyu mwanamke (mama yangu) Wana akili Sana darasani.
Nikaanza kwa kuwasalimia na kuwabembeleza wanipe Ile bahasha. Lile zee likakazana kusema "ulitupita pale bila kutusalimia hivyo hatukupi hii bahasha, kwanza nachana hichi cheti" Hapo ndipo Wazo La Kuua liliponijia kwa Mara ya kwanza katikati maisha yangu. Yaani mtu anataka kutunyang'anya shamba na Cheti changu akichane kweli?
Wenzake ndiyo wakawa wanamzuia asikichane, baadae sana akanipa ila kwa mbinde sana cheti kikiwa kimekunjika-kunjika kama mchicha wakati muda mfupi uliopita kilikuwa kipya.
Ana bahati, angechana Cheti changu, ningetafuta mbinu yoyote anitambue.
Je, Umewahi kuwaza kuua mtu? Chanzo kilikuwa nini?