Uliwahi kuwaza kuua mtu? Hii ndiyo mara yangu ya kwanza kupata wazo la kuua mtu

Uliwahi kuwaza kuua mtu? Hii ndiyo mara yangu ya kwanza kupata wazo la kuua mtu

Mimi nimesoma Kemibos Bukoba ada mwaka 2011-2014 ilikuwa kwa mwaka Mil3. Sasa wewe unafikiri mchezo Mkuu???

Na one ya digits
Na ukaamua kuwa Mwalimu?

Hizo hela si bora ungeendelea kununua migomba
 
Nilipanga kumgonga na gari mtesi wangu, yaani nilikua namvizia njia ya mtaa kabisaa huku nimekunja ndita, ila Mungu si athumani kila nilivyokua nafanya hivyo kile kiumbe kilikua hakikatishi njia ile.
😅😅😅🧢
 
Kuna mzee mmoja niligombana nae kisa tulibishana kwenye ukumbi wa mpira ilikuwa Real Madrid na Barcelona (El Classico). Na mie nikiwa ni Team Ronaldo.

Mie nilikaa kimya ila yule mzee akawa anaongea shit sana, kuwa najifanya mjuaji mara ooh najifanya nina pesa na maneno kibao ya kukera.

Kiuhalisia mie huwa sio muongeaji sana, huwa naamuaga kukaa kimya maana nikiwa na hasira nakuwa na kigugumizi ghafla na kuanza kutetemeka. Sasa yule mzee ndio ikawa point kwake maneno kibao mie namchora tu.

Mpira ukaisha ile tunatoka yule mzee akawa anasema huyu mtoto lazima nimkomeshe tu na shit kutosha.

Alivyosema hvo nikajawa na gesi sio kawaida sikuongea na mtu nikaenda moja kwa moja hadi Gas station (sheli) nikanunua petrol lita 5 nikarudi hadi mtaani nikavizia kwenye saa 8 usiku nikaenda hadi kwake na nikaanza kuimwaga ile petrol kuizunguka nyumba ya yule mzee lengo langu niwateketeze yeye na familia yake.

Ile nakaribia kumaliza kumwaga ile petrol kidogo jamaa angu huyu hapa kumbe alikuwa ananifatilia tokea muda.

Jamaa kafika pale akanirukia kapiga kidumu kule akaanza kunisihi niache kufanya maamuzi kama yale. Hapo mie nimejaa sio kawaida.

Kiukwel ikabidi niache lakini ndio ikawa pona yake yule mzee na family yake.
Lakini sikuishia hapo maana nilikuja kumvunja mguu baada ya miezi kama mi3 mbele hivi.
Duuh wewe una hasira sana
 
Sio tu kuwahi kuwaza,nipo ndani ya hilo wazo kutaka kulifanya tena kwa ustadi.

(1) ni mkate viganja viwili vya mikono na kumkata vidole vya miguu hasa mguu moja tu wa kulia. Kimy kimy

(2) nimteke na kumuweka katk roba nimni’ginize nikimfanyia mazoez (punch bag) mpaka kifo.
Nachuku petroleum nachoma mwil porin.

Rest In Peace
IMG_2297.jpg

17/3/2023 inaniuma sana simalizi wik nalia[emoji24]
 
Nadhiri gani [emoji28][emoji28][emoji28]
Ndugu yangu ni mwaka wa tatu sasa toka fundi huyo akimbie na 4.5m ambazo nilizilipa kwa maumivu ya riba,nilipata kibarua sehemu ndo kilichoniokoa kumaliza deni na kubahatika kuweka madirisha mengine ila likizo yangu nilienda dodoma nilikaa wiki tatu namsaka mdogomdogo,nilimkosa ila naona roho inaniambia ipo siku nitamwona,aisee nitamtafuna,maumivu yangu hayajawahi kuisha

Sent from my SM-G531H using JamiiForums mobile app
 
Mimi nimesoma Kemibos Bukoba ada mwaka 2011-2014 ilikuwa kwa mwaka Mil3. Sasa wewe unafikiri mchezo Mkuu???

Na one ya digits
Kumbe umemaliza form four 2014, ukikua utaacha kufikiria mambo ya hicho cheti
 
Waovu hawazaliwi wakiwa hivyo bali ni matokeo ya uminywaji wa haki na Uonevu katika Jamii. Hata magaidi au wanaotekeleza mauaji ya kinyama, lazima Kuna sababu nyuma yao.

Miaka ya nyuma nilienda shuleni kuchukua cheti Cha O-level. Nilfunga bahasha kwenye baiskeli nikawa nikiendesha speed. Kuna wazee niliwakuta tunafahamiana, Kati yao kulikuwa na mmoja ana mgogoro wa shamba na familia yetu, alikuwa anang'ang'ania shamba letu na anakiri wazi kuwa anafanya hivyo kwa sababu hayupo tayari kuona mjane akiwa na ardhi kubwa Kuliko yake.

Nikaona hakuna haja ya kusalimia, nikawapita kwa kasi kufika mbele nikagundua nimedondosha bahasha yenye cheti! Nikaanza safari ya kurudi taratibu kwa mguu huku nikiangalia barabarani kwa umakini kama nitaona bahasha.

Ghafla nikakutana wa wale wazee halafu lile zee lililokuwa lina mgogoro wa shamba na familia yetu ndilo limeshika cheti changu anakisoma huku anawaambia wenzake "watoto wote wa huyu mwanamke (mama yangu) Wana akili Sana darasani.

Nikaanza kwa kuwasalimia na kuwabembeleza wanipe Ile bahasha. Lile zee likakazana kusema "ulitupita pale bila kutusalimia hivyo hatukupi hii bahasha, kwanza nachana hichi cheti" Hapo ndipo Wazo La Kuua liliponijia kwa Mara ya kwanza katikati maisha yangu. Yaani mtu anataka kutunyang'anya shamba na Cheti changu akichane kweli?

Wenzake ndiyo wakawa wanamzuia asikichane, baadae sana akanipa ila kwa mbinde sana cheti kikiwa kimekunjika-kunjika kama mchicha wakati muda mfupi uliopita kilikuwa kipya.

Ana bahati, angechana Cheti changu, ningetafuta mbinu yoyote anitambue.

Je, Umewahi kuwaza kuua mtu? Chanzo kilikuwa nini?
Kuua ni kiwango cha juu cha ushirika wako na shetani, na ukiona Hali ya kuua inakujia kimbia kaini aliambiwa dhambi inakuotea na unatakiwa kuishinda
 
Kuna jamaa aliniuzia bidhaa iliyo chini ya kiwango nikaenda nayo mpaka nyumbani bila kujua nilipofika nyumbani nakuta mambo tofauti nikarudisha mzigo dukani akaukataa yaani aliniudhi nafikiria nikamchomee TRA lakini sina ninaemjua TRA ndo ikawa pona yake
 
Aisee pole Sana mkuu
 
Waovu hawazaliwi wakiwa hivyo bali ni matokeo ya uminywaji wa haki na Uonevu katika Jamii. Hata magaidi au wanaotekeleza mauaji ya kinyama, lazima Kuna sababu nyuma yao.

Miaka ya nyuma nilienda shuleni kuchukua cheti Cha O-level. Nilfunga bahasha kwenye baiskeli nikawa nikiendesha speed. Kuna wazee niliwakuta tunafahamiana, Kati yao kulikuwa na mmoja ana mgogoro wa shamba na familia yetu, alikuwa anang'ang'ania shamba letu na anakiri wazi kuwa anafanya hivyo kwa sababu hayupo tayari kuona mjane akiwa na ardhi kubwa Kuliko yake.

Nikaona hakuna haja ya kusalimia, nikawapita kwa kasi kufika mbele nikagundua nimedondosha bahasha yenye cheti! Nikaanza safari ya kurudi taratibu kwa mguu huku nikiangalia barabarani kwa umakini kama nitaona bahasha.

Ghafla nikakutana wa wale wazee halafu lile zee lililokuwa lina mgogoro wa shamba na familia yetu ndilo limeshika cheti changu anakisoma huku anawaambia wenzake "watoto wote wa huyu mwanamke (mama yangu) Wana akili Sana darasani.

Nikaanza kwa kuwasalimia na kuwabembeleza wanipe Ile bahasha. Lile zee likakazana kusema "ulitupita pale bila kutusalimia hivyo hatukupi hii bahasha, kwanza nachana hichi cheti" Hapo ndipo Wazo La Kuua liliponijia kwa Mara ya kwanza katikati maisha yangu. Yaani mtu anataka kutunyang'anya shamba na Cheti changu akichane kweli?

Wenzake ndiyo wakawa wanamzuia asikichane, baadae sana akanipa ila kwa mbinde sana cheti kikiwa kimekunjika-kunjika kama mchicha wakati muda mfupi uliopita kilikuwa kipya.

Ana bahati, angechana Cheti changu, ningetafuta mbinu yoyote anitambue.

Je, Umewahi kuwaza kuua mtu? Chanzo kilikuwa nini?
Bila ya shaka huyo mzee hakuwa miongoni wa wenye busara
 
Nilitapeliwa simu kariakoo na kijana mmoja hivi,..hatua za mwisho kabisa za kumfanya yule kijana awe chizi mama yangu alinisihi sana nisimfanyie ukatili binadamu mwenzangu kwa kitu kama simu ila mimi niliambiwa nichague kati ya kumtoa roho au nimfanyie uchizi...
Mkuu Njoo Dm tujadili jambo la muhimu [emoji120]
 
Nikikumbuka Jinsi Walimu wa O-level walivyokuwa wakali, na nilivyohimili adhabu mbalimbali, kuacha usingizi na kutembea kwenye baridi kwa miaka mingi alafu mtu aje achane cheti changu kirahisi. Aisee [emoji34]
Huyo ungepiga kisu tu
 
Back
Top Bottom