Hapa mkuu, jamaa alimaanisha mnyama ambaye endapo atakutana na simba basi simba lazima akimbie kuokoa maisha yake kulingana na hatari ambayo iko mbele yake
Na nahisi hapa mbwa mwitu ana-fit kabisa maana wale mabwana hawanogi kama ugali usio na mboga. Naskia wana rules yao ya "one touch" yani kimbiza ng'ata kisha sizi pembeni endelea kutafuna ulicho ng'ata huku wenzako wakiendelea kukimbiza kwa mtindo huo huo mpaka mnyama anayewindwa kuishiwa nguvu na kuanguka.
Yani eti hawawindi ka simba anavyofanya mpaka amuangushe mnyama chini ahakikishe amekufa kabisa ndio aanze kumla. Wao hawaepui wanalia jikoni hapo hapo kikiwa bado chamoto moto huku kikiendelea kuchemka.