Chui anatabia moja ya ajabu sana katika kufanya mawindo,huyu huwinda mbali na makazi yake,na hii humsaidia sana kumuweka mbali na hatari ya kushtukiwa kuwa anapatikana sehemu fulani hivyo maadui zake humkosa hupata shida kutambua alipo.
Pia mnyama huyu kama wanyama wengine wa jamii ya paka anapokua yupo vizuri tumboni huwa hana madhara makubwa sana na mara kadhaa anaweza kukuacha salama ila hali hutokea pale tu anapokuwa kashiba,anapokuwa hana mtoto au anapokua huko alipotoka hakukutana na adui yeyote,ila kama angekuwa kakutana na adui yeyote akamtibu,basi story ingebadilika.