Uliza swali lolote kuhusu wanyamapori wetu na tabia zao utajibiwa

Uko vizuri mkuu
 
Kuna clip niliona mbwa mwitu kang'ang'ania pumbu za nyati hadi akachomoka nazo
 
Chui mara nyingi ni mwepesi kubaini uwepo wako kwenye eneo lake (territory) kabla hujamuona.

Chui ni miongoni mwa wanyama wawili akiwemo mamba ambao kuwawinda ( uwindaji wa kitalii) ni changamoto.
Chui wakati wa kumuwinda hata ukimtegea mzoga hababaiki nao mpaka ajue aliyeuweka na malengo ya kuweka hapo.
Vinginevyo wanyama karibu wote wanamuogopa binadamu mpaka atakapoona usalama wake uko hatarini
 
Mamba ndy mnyama anayeishi miaka mingi..Kama sikosei
ndio anafikia miaka 70 hadi 100.huku africa tuna NILE CROCODILE ndio common sana.uzito wa mamba hufikia hadi kg 600 na urefu wa mita 5.ni mnyama ambae anaweza kuishi mwaka mzima bila kula.katika kipindi cha ukame mamba akikosa chakula hushusha mapigo yake ya moyo kwa kila pigo 1 kwa dakika.inaitwa Hirbernated.hufanya hivyo akiwa sehem tulivu bila kujisogeza.ni mnyama pia anaemeza mawe baada ya kula nyama ili kisaidia usagaji wa chakula.kingine ndio mnyama anaeongoza kwa strongest bite.yaani akikubana na ule mdoma wake ni umeangukiwa na semi
 
kuna hoteli moja ya kitalii walizoea kumrushia nyama chui akija kula wageni wanampiga picha.akazoea hiyo tabia siku ingine kaja hamna kitu akapita na mtoto wa kizungu alikuwa anacheza mpira.ilikuwa noma sana hiyo.chui alishtukiwa akakimbia akaacha maiti ya mtoto.kesho yake wamemfata maskan kwake akawa amejificha si anajua amefanya bofu anatafutwa auliwe!!mziki aliwaamshia hapo marangers hawatausahau
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…