Uliza swali lolote kuhusu wanyamapori wetu na tabia zao utajibiwa

Nyoka wenye vichwa viwili wapo na kwetu huitwa ndumila kuwili anakichwa mbele na nyuma
 
Nyoka wenye vichwa viwili wapo na kwetu huitwa ndumila kuwili anakichwa mbele na nyuma

Kwenye tasnia ya mifugo, hiyo kitu tunaita congenital defects, na mara nying kiumbe hakiwez survive kwa muda mrefu, ila kwa nyoka vichwa viwili..nilisomaga story tu na zile movie za kichina za dragon.. Ya MUNGU mengi labda wapo, i never know.
 
Nyoka wenye vichwa viwili wapo na kwetu huitwa ndumila kuwili anakichwa mbele na nyuma
hao nyoka nakumbuka zamani sana kwenye mashamba ya mipunga nilishawaona hata ukimkata katikati anakwenda mwingine mbele kipande kingine kinaendelea nyuma.yaani anaweza kutembea vyote vyot!ngoja nifatilie kwenye kabrasha.lakini sio aina ya nyoka ile kwa jinsi nakumbuka ni kama worms au aina hiyo
 
Nyoka niliomuona ni mwenye vichwa viwili Ila upande mmoja Wana share mwili mmoja respiratory, digestion, reproduction nk na huwa hawaishi muda coz vile vichwa vyao huwa wanaumana kwenye kupiga msosi japokua akila mmoja wamekula wote

Ila sijawahi ona vichwa viwili mkia na mkia
 
inategemea wameungana kwa sehemu ipi ya mwili!kwa nyoka waliozaliwa wameungana wanaweza kuishi hata miaka 20 ila iwe kichwa kimoja ndo chenye full decisions.
 
mimi swali ninalojiulizaga na kukosa majibu ni, je mtu aliyezaliwa na upofu alalapo au anapokuwa usingizini anaweza kuota ndoto na kuona kama sisi tusio vipofu mana sisi tunapolala huwa tunafumba macho lakin tuna uwezo wa kuona taswira za watu kupitia ndoto za uongo au ukweli. mana tunapofunga macho huwa tunakuwa sawa kwa kuona giza je tunaweza wote kuota sawa?
 
Mtoa mada
Kwanini twiga hatoi sauti namaanisha kwanini hana uwezo wa kutoa sound!
Na kwanini Simba dume ana sharubu
twiga anatoa sauti lakini ni ngumu kwa binadamu kuskia.ila ni mara chache anaweza kupiga kitu kama mruzi(mbinja).wao kwa wao ndio wanaweza kuwasiliana na mara nyingi hupeana ishara kukiwa na hatari bila ya kutoa sauti.
sharubu kwa simba ni kwaajili ya display yaani kuvutia wanawake (urembo)na sio kwa ajili ya ulinzi wa shingo wakati wakigombana na dume mwenzie kama wengi wanavyooelewa.
 
ni kweli vipofu wanaota sababu wana sub conscious mind kama binadam wengine.ila wao ndoto zao zinakuwa ngumu sana kwenye uhalisia wake.
 
Nyoka ana macho na anaona vizuri, kuhusu swala la kutoa ulimi nje kila mara hii inatokana na kuwa nyoka hana masikio kama wanyama wengne kwaiyo anatumia ulimi kunasa mawimbi ya sauti.
 
Kuongezea pia ni mnyama mwenye wivu sana kwa mwenza wake na nimbabe anaweza pigana hata na simba dume wawili bila uoga
 
Kwa mamalia ni ngumu Sana dume kumvutia jike kimuonekano navyojua!
Ndege, reptilia,na insect ndio wana sexual dermophisim mfano unakuta jogoo nimzuri kuliko mtetea au dume la Weaver linapendeza kuliko majike!

Kuhusu sharubu za Simba kumkinga asipatwe majeraha shingoni ni kweli kabisa coz Simba dume akiingia territory ya mwenzake mpambano huwa ni mkali till last blood drop
 
Ila ukianzisha vita naye, nasikia huwa hana vita vya ana kwa ana kama vya Simba. Yeye huwa anapigana ile inaitwa "guerilla war", kwamba unashambulia halafu unatokomea kusikojulikana kwa kutumia njia hii, halafu unakwenda kurudi tena kisirisiri, kimya kimya na kwa kutumia njia nyingine, halafu unashambulia tena. Nasikia vita vya chui ni balaa, bora Simba!
 
mainly simba hushambulia kwenye spinal cord kuliko shingoni!hawa wakiwa kwenye fighting.unaonaje hiyo??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…