ruby garnet
JF-Expert Member
- Apr 10, 2017
- 2,869
- 3,852
- Thread starter
-
- #61
1.ni vifaa gani vyenye bei nafuu ambavyo mchimbaji mdogo anaweza kuvitumia kugundua madini yaliyopo aridhini? 2.katika machimbo madogo madogo mule ndani ya mashimo kunawakati huwa kunazuka gas hatari ambayo huua na kukausha.je[a]gas hii husababishwa na nn? je kama watalaamu na watafiti hamuoni kuwa geita inapaswa kufanyiwa utafiti wa gesi kutokana na kiashiria hicho?[nipo tayari kuwapeleka ktk eneo husika] 3.katika uchenjuaji wa dhahabu wa wachimbaji wadogo,kemikali ya zebaki/mecury hutumika kukamatisha dhahabu iliyopo katika mchanga ulioragwa karashani.kwa bahati mbaya kemikali hii imeonekana kuwa na madhara ya kiafya na pia kuacha dhahabu nyingi kwenye mcianga.je, hakuna njia nyingine nzuri ya kukamatisha dahabu? 4.OMBI:HUKU GEITA ndani ndani kata ya lwamgasa kunasehemu kunamawe yenye shaba nyingi sana.yaani nyingi kweli kweli.kama kunanamna ningependa kuwakaribisha ktk utafiti wa shaba.ahsanteni.
mwenye shamba
swali
1.ni vifaa gani vyenye bei nafuu ambavyo mchimbaji mdogo anaweza kuvitumia kugundua madini yaliyopo aridhini?
jibu
kunachangamoto hiyo mwenye shamba, kwa kuwa umeuliza kutoka geita nafikiri madini unayoamanisha ni dhahabu.
kwakifupi dhahabu huwa ni vitu vigodovidogo sana kulinganisha na ukubwa wa mwamba hivyo kwa dhahabu za kwenye mwamba hakuna kifaa moja kwa moja kinaweza kukwambia kuwa kunadhahabu nyingi kiasi gani au kina gani utazipata. ila kunanjia za kuweza kutafiti kwa garama kidogo kwa wachimbaji wadogowadogo. kwa dhahabu za mwamba uliooza na kusambaa juu ya aridhi(kanda ya ziwa wanaita dhahabu za sesa) kunakifaa kinaitwa gold detector ndiyo kinaweza kungundua zilipo na zenyewe ziwe kwa wingi kwerikweri vinginevyo hata zenyewe huwezi kuzigunduz. kifaa hivi vipo vya modeli tofauti tofati vinauzwa kuanzia 5milion hadi hata 40million. hiki kifaa hakiwezi kupima dhahabu ya kwenye mwamba japokuwa sasa kunatechnolojia nyingi zinzatengenezwa lakini hakuna kifaa kinachoweza kufanya kazi kwa ufanisi kwa kuonesha mwamba ulipo kwa usahihi.
njia zinazoaminika hadi sasa kutafiti dhahabu kwa wachimbaji wadogo wadogo ni hii hapa lakini kwa miamba iliyitokeza juu ya aridhi.
kupiga sample za sesa(dhahabu za mwamba ulioza na kusambaa aridhini). hivyo ukigundua zilipo dhahabu za namna hii ujue kunamwamba karibu hivyo unaweza kufatilia kwa kupiga sample kuelekea zinakokwenda hadi zinaweza kukufikisha zilikotokea
tanzama picha hapo ukiwa na kalai lako na maji nunaweza kuutafuta mwamba uliosambaza dhahabu kutoka bondeni kuelekea mlimani kwani hii inamaana kama umekuta kuna dhahabu bondeni jaribu kuangaria kuelekea juu mlimani
hebu tazama picha hapo juu rangi nyekundu inaonesha mwamba wa dhahabu ambapo kwa juu umeoza na kuanza kusambaa
hapo juu unaweza ona mwamba huo wa dhahabu ulivyooza na kusambaza dhahabu maeneo ya karibu. hivyo ukiwa makini na karai yako unaweza tafuta mwamba wa dhahabu ulipoanzia na kugundua. hivyo hii ndiyo njia yenye garama na fuu sana kwa mchimbaji mdogomdogo. Ila lazima pia uwe na uzoefu wa madini ya dhahabu na miamba yake. na hili kwa mchimbaji mdogo mdogo ni kitu cha kawaida.
SWALI
2.katika machimbo madogo madogo mule ndani ya mashimo kunawakati huwa kunazuka gas hatari ambayo huua na kukausha.je[a]gas hii husababishwa na nn? je kama watalaamu na watafiti hamuoni kuwa geita inapaswa kufanyiwa utafiti wa gesi kutokana na kiashiria hicho?[nipo tayari kuwapeleka ktk eneo husika]
JIBU
mwenye shamba
gas unayoiona mashimoni ni gas ya ukaa (carbon monoxide) na siyo sawa na gasi inayozungumuziwa mtwara na lindi
kama umewahi kusikia kuwa usilale na jiko la mkaa ndani likiwa linawaka ni hatari litakusababishia kufa kiailensa( huuwa na kukausha). hii ndiyo gas ya carbon monoxide hiyo pia kutokea wakati mkaa unaungua kwenye jiko ila hautuasili katika mazingira nyenye hewa nyingi kila siku watu wakiwa wanapika .
mwenye shamba labda nikueleze husababishwa na nini shimoni( chazo cha gas hii machimoni ni nini?)
1) huko kanda ya ziwa huwa kunamiamba inayoambatana na dhahabu huwa ina aina ya mawe ambayo yana carbonate hivyo huwa yanapata joto na kusababisha kutoa hewa ya carbon monoxide(gas ya ukaa) hasa wakati wa kulipua migodini kwani husababishia moto kutokea hata kama bila kulipua kama shimo limebana sana inaweza sumbua sana hiyo gas
2) pia kutumia mitambo inayotoa moshi humo shimoni nayo husababisha gas hiyo kujaa mgodini humo
njia ya kuepukana na tatizo hilo ili uendelea kula pesa ya dhahabu inayotoka kwenye shimo lako.
1) kuweka mashiyo ya hewa ya kutosha kwenye mgodi ili hewa iingie ya kutosha( good ventilation) hii njia hutibu kwa hewa hii kwa njia ya kikemia. yaani hewa ya ukaa +hewa ya oxjeni unapata hewa ya corbon dioxide ambayo sawasawa na hewa tunayopua binadamu.(Co + O = CO2)
2) Weka mtambo wa kuingiza hewa safi shimoni. mfano wengine wanatumia upepo wa copresa ili kuingiza hewa shimoni na pia kunamitambo mahususi kwa ajili ya kuingiza hewa shimoni.
swali
3.katika uchenjuaji wa dhahabu wa wachimbaji wadogo,kemikali ya zebaki/mecury hutumika kukamatisha dhahabu iliyopo katika mchanga ulioragwa karashani.kwa bahati mbaya kemikali hii imeonekana kuwa na madhara ya kiafya na pia kuacha dhahabu nyingi kwenye mcianga.je, hakuna njia nyingine nzuri ya kukamatisha dahabu?.
jibu
nikweri zebaki ni hatari kwa afya tena mbaya mno lakini ubaya wake hasa ni sawa na ugonjwa wa HIV kwani zebaki haiui papo kwa papo. ninaomba nikueleze kuwa zebaki hata kama ikiwagwa sehemu harafu ukapanda mchicha inaweza kuingia kwenye mchicha na ukiuchuma ukaula utaipata mwilini, pia ikiingia kwenye mkondo wa maji inaweza safiri hadi hata ziwani na samaki akiila nawe ukija kumula samaki utaipata mwilini mwako, pia ukiikamata ukiwa na kidonda inaweza kukuingia mwilini mwako. na wale wanoochoma dhahabu kwenye moto sehemu isiyo nahewa yakutosha mvuke wake utakuingia na unaharibu ubongo .
pia ni kweri mercury huacha dhahabu nyingi kwenye mchanga. lakini naomba nikukumbushe kuwa siyo mercury inayosambabisha dhahabu ibaki kwenye mchanga bali ni njia ya uoshaji wa mchanga wa dhahabu. kwani mwenye shaba mercury hutumika kukamatishia tu na hii ni hatua ya mwisho ambayo huwa umebaki na mchanga wa takilibani ndoo moja ya lita20 kutoka kwenye michanga wa viloba 300(kiloba ni mifuko ya kilo 50 iliyojazwa unga uliosangwa kalashani).
mwenye shamba huo ndio mtambo wa kuoshea dhahabu kwa wachimbai wadogowadogo (gold washing plant for small scale) kwa kingereza mtambo huu unaitwa sluice box
Hivyo dhaahabu nyingi hubaki kwenye mchanga ( marudio, senate na kwa kimombo tunaita tailling) siyo kwa sababu ya zebaki(mercury) bali kwa sababu ya mtambo wetu huu wa kuoshea siyo mzuri na umepitwa na wakati.
kutokana na hili ndiyo maana kunanjia nyingine za kuweza kupata dhahabu iliyobaki kwenye mchanga huko kanda ya ziwa tunaita kuozesha (yaani kutumia asidi iitwayo cynide) na ndiyo maana mchanga uliooshwa unanunuliwa kwa bei kubwa sana na wanaenda kuozesha na kupata dhahabu iliyobaki na njia hii kwa kilataalamu tunaiita cynide leaching. migodi mikuwa ndiyo wanatumia njia hii ila inakuwa tofauti kidogo njinsi ya mitambo yao inavyofanya kazi ( na hiki kitendo cha kuosha mchanga ili kupata zahabu ndiyo tunaita kuchenjua)
mwenye shamba mchanga unaobaki wenye madini baada ya kuosha ndiyo unaenda kukamatishwa na mercury na mchang huu ni kidogo sana hivyo huwezi kusingizia mapato yako mgodini ni kidogo kutokana na mercury bali ni kidogo kutokana na mtambo wa kuoshea wa kizamani
MWENYE shamba mitambo ya kisasa ipo ila inahitai pesa
mfano ya plant iliyojengwa busolwa huko Geita
mwenye shamba nafikili utakuwa umenielewa hapo.
swali
4.OMBI:HUKU GEITA ndani ndani kata ya lwamgasa kunasehemu kunamawe yenye shaba nyingi sana.yaani nyingi kweli kweli.kama kunanamna ningependa kuwakaribisha ktk utafiti wa shaba.ahsanteni.
Ombi lako limepokelewa ninaratiba ya kutembela huko kwani huko mimi ni nyumbani nitakutafuta nikija GEITA ili niweze kuona eneo lako hilo la shaba.
ASANTE SANA KWA MASWALI KAMA HUJAELEWA UNAWEZA NIULIZA TENA.