Umaskini ni laana; nimeamini pia maskini ana roho mbaya sana

Umaskini ni laana; nimeamini pia maskini ana roho mbaya sana

Ila yote kwa yote majitu majizi nayachukia sana sijui sababu sina kitu

Hivi kila mtu akiiba hivyo tutafika? Halafu tunalalamika kwanini hatutoboi
 
Mimi huwa nasema mtu akitaka sehemu ya mwili wangu mfano nywele au kucha aje Mimi nitaenda nae Saluni nitanyoa nywele namkabidhi akafanye anachotaka au kama ni boxer basi aje nimpe dazani. Tusitishiane na upuuzi ebo! Ila jamaa una hela duuuuh huko itakuwa Airport au Bandarini.
Comment bora kabisa. Haina hata chembe ya husuda! Mungu akufanyie wepesi mkuu.
 
Mjomba hakuna tajiri anajigamba mtandaoni Mo, Bakhresa, Bill Gates, Jeff Besoz na wengine ushawahi kuwasikia wakijitamba mtandaoni kua wana Pesa n bla bla bla sijui ndugu kufanya nini tena Bakhresa ndio huna details zake kabisa zaidi ya kujua asset zake tu, na ikakupwoteka kalipambilile maana yake ikikuuma nenda kajinyonge
Acha njaa na wivi bro![emoji38]
 
Acha njaa na wivi bro![emoji38]
Sina njaa Sina wivu Mzee maisha ya mtandaoni kila mtu Bill Lugano we understand that, Bei Elekezi naongopa ? Hutaki muulize Chizi Maarifa

Naweza nikakwambia hapa nachat Jf nikiwa nipo ndani ya Submarine chini ya maji na ukajaa ulivyo jinga, ninaenda kesho kutembelea ujenzi wa mabangaloo yangu hapo masaki ambayo nimetumia almost Trillion 200 nikikwambia hivyo unajaa tena pumbavu, pokea Kofi la uso utoe wenge hilo
 
Pole sana mkuu, nimegundua wewe ni mtu mwema na pesa inakutesa sana...😎
Sasa ebu fanya hivi.....
Kama itawezekana naomba ufanye mpango unitumie 20k ili walau nikanunue debe la mahindi na kilo moja ya dagaa, kuni nitajisumbukia...😔
Fanya wepesi kwa
Tigo wakala ni 537797 Ashraf Abdallah...😊
M-pesa wakala ni 876134 Ashraf Abdallah....😋
By the way, umebarikiwa kabla sinakuombea...😎
akituma nitag mkuu na mimi nikae kwenye foleni ya kupokea fedha
 
Hiki niandikacho ni kisa cha kweli na ndicho ninachopitia.

Nikiri kwamba nimezaliwa kwenye umaskini na nimesomeshwa kwenye umaskini mpaka namaliza elimu yangu

Nilisota kidogo tu kitaa baada ya kumaliza elimu nikapata kazi sehemu nikaajiriwa, baada ya mda kutokana na Tabia yangu ya ukimya na usiri mkuu wangu wa kazi akanihamishia idara ambayo baadae nilikuja kujua ni sehemu yenye michongo mingi ya pesa.

Nikafundishwa kazi, nikaiva. Hela zipo idara hii bwana, kwa Siku nilikuwa nikitoka kazini mfukoni kuna 3+m kama hamna hamna sana nina 1+m.

Ndani ya miezi 3 nikiwa pale nikawa niko vizuri nikanunua uwanja sehemu yenye hadhi kidogo heka 3 nikaweka mansion yangu ikiwa na uwanja wa basebal na netbal ikiwemo sehemu za kucheza watoto na mabwawa ya kuogelea.

Mpaka huu mjengo unakamilika nilitumia zaidi ya 400+m, siku nawapeleka wazazi na ndugu hawakuamini kutokana na mazingira niliyotoka na namna nilivo mkimya. Sikuishia hapo wadogo zangu tumbo moja wote nilianza mchakato wa kuwajengea nyumba kila mmoja yake na nikafanikisha nyumba nzuri za kisasa ambazo wastani nilitumia 120+m

Ndugu zangu wote nilitoa msaada kwao bila kubagua, watoto ambao walikuwa wamefeli shule niliwapa uchaguzi wanachotaka wanawafanyia, nimetoa mitaji nimepeleka vyuo vya ufundi natimiza mahitaji yao kila kitu maana hela ninayo na sioni fahari ya kuabudiwa.

Sasa baada ya miaka 6 kuona nazidi kuwekeza kwa kasi ileile tu, mashangazi wakaanza za chinichini huyu jamaa ni Freemason mimi nikiwa sijui chochote. Kuna kipindi msiba ulitokea, Mke wa mtoto wa shangazi alifariki kulingana na majukumu yangu ule msiba sikufika ila nilibeba gharama zote za msiba.

Bwana kama miezi 6 hivi za msiba kupita, napata habari k kumbe watu wanachukuzwa na mafanikio, mashangazi wanapanga mipango ya kunidhuru kwa mda mrefu na mmoja aliyepewa majukumu ya kuchukua baadhi ya vitu kwenye mwili ikawa mlopokaji akanipa mchongo wote, wala sikuvumilia nikawawashia Moto mashangazi kufatilia kumbe baba zangu baadhi wanazo habari za hii mipango na wakanyamaza. Imenitia hasira sana.

Wanasema nimemuua yule mke wa binamu yangu na moja ya masharti niliyopewa ni kuwa na roho nzuri ya kuwasadia kwa hiyo nao wanataka kulipa kisasi kwa kunidhuru. Nina hasira na hawa watu Moto niliowawashia nimejikuta nawatukana mpaka matusi ya nguoni.

Natamani siku zirudi nyuma nisingefanya huu ujinga wa kusaidia hawa wanaoitwa ndugu, huku tunakoelekea naona kabisa kuna dalili mbaya kisa mafanikio yangu

Nimeongeza nguvu zaidi upande wa mama, huko nawajengea majumba ya maana.. Sasa naona wivu waziwazi mpaka watoto wao niliowasaidia kwa hali na mali.
Wewe ni muhaya?


Chai.
 
Hii chai sema ina ujumbe mzuri. 3m kwa siku kihalali nje ya mshahara ni kitu kigumu hapo ni upiga dili 100%. Cha muhimu wakati unaendelea kulaumu maskini jitahidi kutunza hela sehemu isiyojulikana ili likitokea la kutokea uwe na hela ya kumlipa wakili.
 
Nimekwambia haina haja ya kujieleza nafanya nini mkuu. Amini unachoamini ila nilichoandika ndio ukweli wangu
Wewe ni mwongo. Au unadhani watu humu ni wajinga wajinga hawajui mifumo? 3m kwa siku ni ngumu na kama ni upigaji iwe serikalini au nje ya serikalini jua ni suala la muda tu kabla ya kudakwa.
 
Kitu kidogoo sana hicho.. endelea kula maisha. Una thawabu nyumbani.

Ila kawaombe msamaha hayo matusi nao wakuombe msamaha... Mpeane mikono muachane kwa amani.
Kupeana mkono na mchawi ni hatari zaidi. Hapo waachane juu kwa juu. Kuomba suluhu watu wanaojihusisha na uchawi ndo watakumaliza kirahisi. Hiyo mbinu ya kuwakoromea ni sahihi kwa wachawi
 
Kupeana mkono na mchawi ni hatari zaidi. Hapo waachane juu kwa juu. Kuomba suluhu watu wanaojihusisha na uchawi ndo watakumaliza kirahisi. Hiyo mbinu ya kuwakoromea ni sahihi kwa wachawi
Hakuna uchawi...
 
Back
Top Bottom