Umeona nini kwenye maziko ya yule tajiri wa Kibaniani, Patel tokea mwanzo hadi mwisho?

Hapo uliposema sisi weusi ni rangi ya kiza.

Hivi ni lini tutajikubali rangi yetu na kuona fahari?
 
ficha ujinga sio wote wanakufa wakipata korona ,ila ugonjwa upo

Ugonjwa gani ambao haupo? Mjinga wewe ambaye unajitutumua kwenye keyboard kulazimisha watu wawe waoga na maisha. Kama veep, jifiche ndani usituchoshe
 
Uongo
 
Unataka tuchukue hatua zipi?.
Unadhani hao wenzio wanaokufa na Corona hizo HATUA HAWAZIONI?
Au unadhani wanaokufa na Corona Ni wajinga na wewe ndo mjanja?.
ikiwa marekani na ulaya nzima wanachezea kichapo cha Corona wewe kunguni kuwa mzima unadhani ni UJANJA WAKO?.
hao WAHINDI mnaowasifu wamevaa barakoa hapa Tanzania mkidai wanajikinga na Corona KWANINI WASIWAPIGIE SIMU NDUGU ZAO HUKO INDIA WAWAAMBIE WAVAE BARAKOA WAEPUKANE NA CORONA?.

Punguza ujinga basi mjinga . ugonjwa upo. Mie ndo ntaachiwa hospital punde. Chukueni hatua nimepigania uhai for 3 weeks
 
Wamarekani,waingereza wamewekeza billions of money kununua dawa ya corona. Ivi kwanini wasingetumia njia hii yakwako kutibu corona alaf hizo hela wafanyie mambo mengine ?
 
Endelea kuwaamini wanasiasa

Waliwaahidi millioni 50 kila kijiji hamkuziona; wakawaambia watawanunulia NOAH kila mmoja wenu wakilipwa hela za makinikia nazo HOLAAAA!!! Bado mnawaamini tu!!! Mtakuwa mataahira.
 
Hivi kuna mtu anaamini kuwa hakuna corona tZ?
 
Hapo uliposema sisi weusi ni rangi ya kiza.

Hivi ni lini tutajikubali rangi yetu na kuona fahari?
Sasa ulitaka nione aibu kujiita rangi ya kiza ??? Au ningesema Ni tunda langu lile lenye rangi ya chungwa , Na usitulazimishe tuseme rangi yetu nyeusi mbona tupo waTanzania wa kila rangi ,ila sisi tuliokoza buluu tunaonekana kufaa kwenye kazi ya jeshi tu.
 
Barakoa haizuii harufu
Na barakoa pia haizuii Corona na kama inazuai ni kwa % ndogo sana. Kama ingekuwa inazuia corona ulaya, china, na marekani wasingekufa kwa maelfu maana huko ndiko barakoa zinakotengenezwa! Na je huku mtaani hao mabaniani wanavaa hizo barakoa?
 
Unavyoviandija vibafanana na jina lako . kweli we jinga
 
Reactions: BAK
Hivi kuna mtu anaamini kuwa hakuna corona tZ?
Tatizo wapo wanaoamini hakuna corona na wapo wanaoamini corona ipo,limekuwa ni suala la kuamini tu sasa kila mtu anachagua mwenyewe anachotaka kuamini.
 
Nani alikwambia katika Nchi hizo kila mtu anavaa barakoa? Kuna kundi kubwa la watu katika Nchi zote hizo ambao wanapinga kuvaa barakoa wakidai uhuru wao wa kuamua na wengi wameupata ugonjwa na wengi wao wamekufa.

Tusibishe kitu ambacho kimefanyiwa utafiti na wataalamu na kuonyesha kinasaidia kupunguza maambukizi ya COVID19 kama kikivaliwa vile inavyotakiwa.
Kama mask ingekuwa ndo dawa ya Corona , basi ujerumani na marekani WANGEPONA.

hivi unadhani hyo barakoa yako ndo ITAKULINDA NA CORONA?

hao wanaokufa na Corona HAWAZIJUI HIZO BARAKOA WAVAE WAEPUKANE NA CORONA?

AKILI SIO PAMBO ZITUMIE.
 
Kwenye msiba wa baba yake joketi kuna ndoo za kunawa maji lakini unaambiwa hakuna Corona.

Juzi nilienda Muhimbili kumuona mgonjwa, madaktari wanasisitiza kuvaa barakoa na wanakataza msongamano lakini unaambiwa hakuna Corona.
Wapi uliambiwa hakuna corona?

Corona ipo na tunaishi nayo kama ambavyo tunaishi na malaria. Ukijichnganya inakuondoa.

Unavyochukua tahadhari kwa malaria....chukua tahadhari hivyo hivyo kwa corona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…