Umepitia/Unapitia changamoto gani tangu umalize chuo mpaka sasa?

Umepitia/Unapitia changamoto gani tangu umalize chuo mpaka sasa?

Kuhusu ajira ilikuwa kipengele kidogo , nilisota kiaina mtaani, andika sana barua cha kushangaza nilikuwa hata sijibiwi japo kimaisha sikusota sana sababu nilikuwa nina sapoti ya ndugu hivyo ilisaidia kubalance stress

Niliomba sana Mungu naye akanibariki na Internship, baada ya muda akanifungulia njia zaidi nikapata ajira na kuanza kula mshahara huku life linasonga, sijajipata kivile ila nashukuru nilipo ni kwema na-pay bills na kusaidia wengine.

Kuhusu mapenzi nilisota kiaina, ilinibidi nirudi kwenye makoloni yangu ya chuo hata baada ya kumaliza maana mtaani vilikuwa vipengele vingi😁 bora wale niliowaacha school walionijua jobless hivyo kiaina walini-bless bila vizinga vya kijinga

Mengineyo, wakati wa Mungu ndio wakati sahihi ukimtumainia atakupigania, cha msingi weka nia na bidii bila kuhofia.
Waoe haohao wa chuo waliokua hawakupigi vizinga
 
Mkuu !Pole sana kwa unayopitia kwa sasa.

Kwanza, naomba nikwambie jambo moja USIKATE TAMAA, maisha hayana kuchelewa wala kuwahi, nakwambia siku yako ikifika basi na mambo yako yatanyooka vizuri tu.

SIKILIZA KISA CHANGU

Mwaka 2018 nilikua na miaka 27 kama wewe, na nilikua nimejitolea katika shirika moja na posho yangu kwa mwezi nilikua napewa 42,000/= ( Elfu Arobaini na Mbili tu). Na hii nilikua napewa kama pesa ya sabuni tu lakini uhalisia nilikua ninafanya kazi bure.

Kiukweli kama binadamu na pia kijana wa kiume nilikua napitia wakati mgumu sana, nilikua naona kila kitu kiko against na mm, nilikua na stress sana..ilifika kipindi hata mademu walikua hawanitaki bro[emoji1][emoji1], nilijiona ni mtu mwenye mikosi kwani nilikua nikijaribu kujilinganisha na wana niliosoma nao, nilikua naona wameniacha mbali sana kiuchumi na hata kifamilia(Kosa kubwa sana kujilinganisha na watu).

Lakini broo huwezi amini ilipofika mwaka 2020 milango yangu ya kiuchumi ilifunguka, nikapata kazi ambayo iliniwezesha kuendesha maisha yangu na nikawa na uhakika wa kuingiza 4M kila mwezi, wale niliokua najilinganisha nao nikagundua sikuwa sahihi kwani hata maisha yao ni yakawaida sana, lakini pianilikua najiona nimechelewa kimaisha lakin kumbe nilikua pazuri tu na wala sijachelewa.

Bro USIKATE TAMAA....MAISHA NI KUPAMBANA NA MUDA WAKO UTAFIKA ONE DAY

KUWA STRONG MZEE
Hongera!
 
Acha tu nimeanza masters yangu MBA since 2021 changamoto za ada,ujana na majukumu ya watoto wawili mpaka sasa sijamaliza,ada Sasa semester ya mwisho ndo imekuwa ngumu mikopo nadaiwa kuanzia garage mpaka dukani mpaka najuta kusoma MBA....ooh God please hii MBA ije inilipe maana inanitesa sana familia inakula wali kama wanafunzi waa boarding
Mungu akufanyie wepesi
 
Nilikosa kibarua nkawa sina hata geto naishi porini, baadae kwa ugumu sana nkaja kupata kichumba yaan kijistoo cealing board hakuna upande wa pili choo. Watu wana sifa akiwa anakunya unamsikia anahema na kujamba kana kwamba amekula mbigili, alafu harufu kali kichizi. Nilkua nakereka sana. Alhamdulillah nilivuka.
Duh! Pole Sana mkuu
 
Ahsante Sana mkuu kwa kutuhamasisha
Kuhusu ajira ilikuwa kipengele kidogo , nilisota kiaina mtaani, andika sana barua cha kushangaza nilikuwa hata sijibiwi japo kimaisha sikusota sana sababu nilikuwa nina sapoti ya ndugu hivyo ilisaidia kubalance stress

Niliomba sana Mungu naye akanibariki na Internship, baada ya muda akanifungulia njia zaidi nikapata ajira na kuanza kula mshahara huku life linasonga, sijajipata kivile ila nashukuru nilipo ni kwema na-pay bills na kusaidia wengine.

Kuhusu mapenzi nilisota kiaina, ilinibidi nirudi kwenye makoloni yangu ya chuo hata baada ya kumaliza maana mtaani vilikuwa vipengele vingi😁 bora wale niliowaacha school walionijua jobless hivyo kiaina walini-bless bila vizinga vya kijinga

Mengineyo, wakati wa Mungu ndio wakati sahihi ukimtumainia atakupigania, cha msingi weka nia na bidii bila kuhofia.
 
Kama binadaamu kuna wakati mtu unapitia magumu mpaka hujui nani wa kukusaidia hata kimawazo.

Leo nimeanzisha thread hii ili tushare mambo au changamoto mbalimbali ambazo tunapitia sisi viumbe wa Mungu.

Orodhesha changamoto na jinsi ulivofanikiwa kutatua ili umsaidie mtu mwingine huko aliko.
1. Changamoto ya ajira.

2. Changamoto ya mapenzi.

3. Changamoto ya biashara au maisha kiujumla
Mimi nimepitia changamoto ya ajira need liajiriwa serikalini nikaondolewa kwenye payroll kimajungu baada ya kwenda masomoni kusoma fani tofauti na ajira.
Nilianza kurudi kazini 2018 mpaka Sasa Nina barua toka utumishi yenye check namba ikinitaka niombe ajira mamlaka yoyote ya ajira pindi tangazo litakapotoka ili nipangiwe kazi kulingana na uhitaji uliopo ndivyo barua inavyosema.
Kumbuka barua zangu zimecheza utumishi ikulu na wizara ya elimu.

Shida au changamoto nipitie wapi? Ili nifanikishe hatua ya mwisho. Niliwaza nimwandikie mama Samia changamoto je barua ataipata na kama ataipata je ni nini niandike mpaka aridhie kuniajiri? My no 0786601598
 
Ndugu mtanzania hapo sio majungu yaliyotumika kukuondoa kwenye ajira. Uliondolewa kisheria kwani mtu anapoenda kusoma akiwa kazini anatakiwa akasomee kilekile anachotumikia kwenye ajira ili kuongeza ufanisi.

Sasa ww unalipwa sekta A, umeenda kusomea Sekta B, maana yake umependa sekta B na ww unatakiwa uajiriwe huko huko ulikoenda kusomea, na inapaswa atafutwe mtu haraka ambae atakua na ufanisi kama wako endapo ungeenda kusomea kilekile.

Ndo maana ukapewa batua officially ya kukuruhusu kuomba ajira pinfi zitakapotangazwa.
 
Changamoto lililolikumba taifa kwa Sasa Ni huu mkataba ovu wa CCM na DP W.
 
Nina mashaka na afya yako ya akili
Kuna muda saa mbovu husema ukweli, sali sala ya toba kijana.

Tatizo lako unataka kuonyesha hukufanya hivyo ulivyoandika ila ndo ulifanya sasa.
Unataka kwa Mungu uwepo na jf pia ikuone rijali.
 
Miaka Mi4 kukaa porini huku nikisubiria Michongo itiki
Mpenzi Wangu alikosa uvumilie akaamua kuolewa Kwa kuisingizia familia yake kuwa imemshinikiza sana na kimtishia kumtenga.
Ila MUNGU ni kila kitu kilikuja kutimia baada ya muda alioupanga Mungu Mwenyewe.
 
Pia changamoto nyingine kwa sasa nina 27 years ninaona nmechelewa wenzangu wana kazi nzuri wana magari wanapost wanaenda sehem nzuri wanavaa nguo nzuri mi narudia rudia tu nguo
Relax..fanya kile ambacho kinaboresha maisha yako kila siku.Ipo siku itajibu
 
Back
Top Bottom