Umerogwa sio bure: Unang'ang'ania Dar es miaka mingi, kula kwa shida, kulala kwa shida, unasafiri kwa shida huku kuna ardhi Tanzania haina mwenyewe

Ana kitu Asipuuzwe!!lakini Tunaomba Sana usiwe Unatugombeza,,,alafu ukutute nae wa liwale anapambana kuja dar,,ni mifumo ya maisha ya kila siku ya wanadamu Kwa hiyo wala isikuudhi Sana,,,Utaghafilika bure na walimwengu na ya ulimwengu pia!!
 
Mimi niko Dar mwaka wa 8 sasa ni government employee . Sasa unataka niache kazi ya uhakika nikalime?
Nikitaka kulima huwa nalima mazao ya msimu Njombe viazi mviringo.

"Sasa unataka niache kazi ya uhakika nikalime"

Kwa hiyo mkuu kilimo ni cha second class citizens yani ukiona maisha yamekushinda ndio ukakimbilie kilimo

Ulichoongea ni kweli kwa asilimia kubwa lakini unatakiwa kujua kuwa, mtu maisha ya dar ya kimshinda haimaanishi akienda mkoa ndo atatoboa maana kuna wanaotoka mkoa na wanatobolea dar

Lastly, jiwekeze sana maana government officials wengi wakistaafu au kuondolewa kazini huchanganyikiwa kama si kufa kwa presha kwa sababu ya kuzoea comfortability.. Kwenye majibu yako nimeliona hilo kwa hiyo usidharau vipato vya watu na wakati ukitolewa kazini hata laki kuitafuta mtaani huwezi.. Kwa hiyo wekeza ili vya kutokea vikitokea, usije kuhadhirika
 
Vijiji karibu vyote Afrika vinanuka umaskini uliokithiri. Dar kwa Afrika Mashariki, kusini na kati ndo sehemu yenye unafuu kupata hela ukikomaa. Kuliko uende kijijini bora uombe ushauri kwa waliofanikiwa Dar ili na wewe ujinasue. Kuiponda Dar ni sawa na sizitaki mbichi hizi.
 
Mkuu,

Kwani ni lazima kila mtu atake unachotaka wewe?

Huelewi kwamba watu tofauti wana malengo tofauti katika maisha?

Unataka kulazimisha watu baki usiowajua waishi unavyopanga wewe?
 
Hakuna anaediss kuhusu Dar tunazungumzia wanaong'ang'ania dar na wakati wapo muda mrefu hawana cha maaana wanachofanya wakidhani maisha yapo hapo tu kumbe anaweza kujaribu sehemu zingine, we miaka 10+ bado unaoga kwenye bafu au choo hakina mlango inabidi mlangoni uweke shuka unalojifunika usiku sasa kwanini usiondoke hapo ukatafute maisha sehem nyingine?

Maana mikoani baadhi ya maeneo maendeleo na fursa zipo nyingi na watu wanaishi kwenye nyumba za hadhi ya kibinadam angalau haweki shuka kwenye mlango wa bafu
Nenda kahama,katoro,njombe na maeneo mengne katafute ukijiimarisha unaweza kurudi Dar ukiwa hata na mtaji
 
Swali la msingi. Waliopo hizo sehemu wamefanikiwa kiasi kwamba ni guarantee asilimia 100 ukienda kahama utafanikiwa??

Jibu kama ndio basi mnachosema kipo sawa jibu kama ni hapana basi hamna hoja
 
Sahivi baadhi vijana wa daslam wameanzisha tabia ya kuwasifia wanaume wenzao wenye kipato tena wanawasifia kupita kiasi ili tu wapewe chochote wanajiita machawa mwisho nao wanalilia kuolewa
Machawa wote wamezaliwa na kukulia Kigoma labda na Kagera kidogo ila sio Dar.

Walikuja Dar kwa mbio za mwenge, Gari la mkaa au Gari Moshi Tena wakijificha chini ya viti.

Mwijaku-kigoma
Baba Level-Kigoma
Aristote-Kagera
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…