Umerogwa sio bure: Unang'ang'ania Dar es miaka mingi, kula kwa shida, kulala kwa shida, unasafiri kwa shida huku kuna ardhi Tanzania haina mwenyewe

Umerogwa sio bure: Unang'ang'ania Dar es miaka mingi, kula kwa shida, kulala kwa shida, unasafiri kwa shida huku kuna ardhi Tanzania haina mwenyewe

Bila salamu nawapa ujumbe wenu enyi watu.

Mnaweza kusema kuwa najiinua au nawakashifu ila Mimi siko huko. Ni upendo tu.

Waarabu wanasema fikisha ujumbe hata kama ni mchungu.

Miaka 5 inatosha kabisa mtu kupima bahati ya maisha Dar es salaam au mahali popote.

Unaishi Dar miaka zaidi ya 5 huna nyumba, huna kiwanja, kula kwako ndo kule unatafuta leo ili ule leo, kila siku kwenye daladala wewe ukichomoa pesa kubwa basi buku 2.

Unalala store (jiko, meza, sofa, feni, kitanda, pasi, bag la nguo na vitu vingine vyote ukifungua macho tu hivi hapa.

Tanzania hii kuna mahali kama Liwale huko Lindi ukifika kijiji chochote ukiomba ardhi ya kujenga au kulima unapewa bure kabisa. Yet wewe uko dar hata hatua 4 za ardhi Chanika huna . Umerogwa shituka

Kijijini wenzako wenye bidii wanamiliki pikipiki, gari, guta, nyumba, duka nk.

Kijijini ni bidii zako tu. Mjini kuna pesa kuliko kijijini ila kama kila ukihangahika huzipati za kukukwamua ni vyema utafute chimbo kijijini.

Braza alifika kijiji fulani kuuliza ardhi ya kulima huko chobingo akapewa upana wa hekari 5 urefu ajipimie mwenyewe.

Kama akilima hekari 40 na kupanda mikorosho baada ya miaka 5 atakuwa wapi?

Nakuuliza wewe unayelipwa laki 2 na Mwindi.
Tatizo tumeshawatambia watu kijijini tupo Dar kwenye flyover,tuna maisha mazuri

tutarudi kijijini watatuelewaje?😀😄

Huoni ndugu wakitutembelea kutoka mkoani hua tunajifanya na sisi tumepata dharura hatupo Dar?au kuzima simu kabisa wakifika stand?😝😝
 
Watu wanachuki ambazo hazina logic.
Majinga tu hayo yaliyofeli Dar na kukimbia mjini hayajui kuwa asilimia kubwa ya wanaofanya kazi kwa wahindi ni wazawa maana mgeni ni ngumu ku survive kwa mshahara wa mhindi na huko shambani sijui wanaamka saa sita ndo wanaenda
 
Back
Top Bottom