Umeshawahi kusaidiwa nini na mganga ukaona kabisa mganga wako fundi?

Umefanya vyema mm niliibiwa vitu vya gari. Stata na vitu vingien vya miklioni2 h ila nikatulia tu nilitaka kwenda lkn naaziawapi na mm sijui hbr hzo

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Baada ya kuona biashara yangu imekwama nikaongea na wenyeji wa mji, nikapelekwa kwa mganga mwanamke,

Kwanza mganga huyo akikaa anaogea kama anapokea simu au anapokea maelekezo kutoka sehemu,

Nilikutana na watu wa hadhi tofauti wanamiliki mabasi mapya na magari mengine mapya wamepeleka yakafanyiwe uchawi,

Zoezi la kwanza baada ya kujieleza akanituma nikachote maji kwenye kisima chake, hiki kisima ni maalum kwa kazi hiyo ya kiganga, kipo umbali kama wa kilometer moja kutoka mji ulipo,

Hivyo nilipewa mashariti nisigeuke hadi nikifika nyumbani kwa mganga kupeleka maji na endapo nikigeuka napaswa kurudia zoezi upya.... ila nikajikuta nimegeuka nikiwa nakaribia kufika... niling'atwa na nyuki kwelikweli,

Nikaona uvivu kurudi tena kisimani nikaamua kwenda kwa mganga na maji yale yale .. nilipofika tu akaniamba usikae wewe umegeuka (umekosea mashariti) rudia zoezi, ikanibidi nirudie[emoji23]

Tulishindwana alipoanza kuniuliza
Kabila langu, Wazazi wangu kama wapo hai, idadi ya watoto na mke, pia nichague nani nataka afahamu ninachokifanya endapo nakufa ataendeleza mali.

Nikamwambia nimegailisha zoezi kwa leo ngoja nikajitafakari upya, akanigundua namkimbia akanipa adhabu kabla sijaondoka nikanunue jogoo mkubwa zaidi ya wote nitakaemkuta kwenye cage ya wauzaji sokoni nimpelekee,

Kufika sokoni nikakuta bei mbaya nika bargain nikachukua mdogo kati ya yule mkubwa zaidi, ile kurudi kwa mganga akasema sio huyo, kamlete yule mweupe uliyemuacha[emoji23] tulisumbuana zoezi hilo mara 3 ikabidi nikubali kumnunua na kumpelekea.

Nikatoka nduki hata nyuma sikutazama tena.
 
Na msadaa hukupata

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Mmmh kuna harufu ya chai SAS uendelezi unataka kuombwaa

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
oyaa letaa uzi huu...usitukatiri
 
Noma sana!
 
Hao ndio wa kweli. Ukiona lina taka hela mapema lipe kisogo usepe kabla hajakupa msiba wa pili.
 
Hiyo ni mizimu. Ila siku hiz haina tena nguv mana mambo mengi yamebadilika. Mifugo inavishwa hereni watoto wanasoma mbali nk..
 
Miaka hiyo ndio bodaboda zinaingia ingia kuna mwanangu wa haswa haswa,alipewa moja awe analeta hesabu.Shida ya mwanangu mtu wa kilaji sana na kamti pombe.Kwa kifupi alipoteza boda ya watu.Mwenyewe hakukubali akadai chombo yake haipotei kifala so sijui digala alienda kwa mtaaalamu.Mwana akawa analalamika anahisi ametwishwa boda mabegani hawezi kuamka wala kutembea ilikua ni kamzozo.Kila nikikumbuka haingii akilini nahisi kama kulikua mipango mingi hapo kati ambayo hatukuijua.
 
Nyingine kuna jamaa yetu anajikuta mtu wa mifugo sana,kila mtu na mambo anayoyapenda bwana.Siku hiyo kaniambia nimsindikize sehemu eti anafata dawa ya kupata njiwa weusi kwani ni deal sana.Kufika kwa mtaalamu akapewa kimjiti awe anaweka kwenye maji ,aisee njiwa walitotoa watoto weusi balaaa kila wakitotoa ni black tu mpaka akakatupa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…