Umeshawahi kutana na koboko(black mamba), uliescape vipi maana huyu sio wa mchezo

Umeshawahi kutana na koboko(black mamba), uliescape vipi maana huyu sio wa mchezo

Huyo ilikuwa nikimuona najihami kwa kukimbia huwa hataki mpishane mara mbili, huwa sio mkali kama watu wanavyosema kwamba akikuona tu anaanza kukuwinda., bali ukimchokoza au mtu alimchokoza wewe ukapita hapo. Au amekuona na bado ukaendelea kubaki eneo lake hapo ndipo huanza kuliamsha labda kama umejiandaa kupambana
Aseee
 
Hunyanyua kichwa juu kulingana na ukubwa wa anayepewa warning halafu hutanua nyama za shingo na kuwa bapa.
Kisha hufunua mdomo mweusii na kutoa mlio kama anapuliza hivi....... Hapo sasa yupo tayari kushambulia iwapo huta ondoka
Kwa mfano usipomsikia inakuaje sasa😂😂😂
 
Cha ajabu ambao hawajaishi vijijini wanamjua kiboko kwa picha ni wakwanza kuelimisha eti akikuona lazima akushambulie, waongo kweli , huyo kukushambulia labda iwe bahati mbaya kuna mtu alimchokoza eneo hilo kwa hiyo awe na hasira alafu wewe ukapita hapo utaona amekushabulia bila kumchokoza,, vinginevyo huyo huwa mpaka umchokoze
Ni kweli kabisa mkuu
Sisi zamani wakati tukiwa wadogo vijijini tunachunga tuliambiwa ukikutana na nyoka mkwepe achana naye usimshambulie

Ukikutana na nyoka aliyeshambuliwa na binadamu akajeruhiwa basi akikuona tu anajua ni hatari na anajihami kwa kushambulia mapema kabisa....... Vinginevyo nyoka ni smart sana kukwepa kukutana ana kwa ana na binadamu
 
Nyoka anaogopa binadamu kuliko unavyomuogopa wewe, black mamba ana sumu za aina mbili,inayoweza kugandisha damu na inayoweza kuharibu mishipa ya fahamu,, ukimuona achana nae, endelea na shughuli zako,, ukiamua kupambana nae ili kumuua inawezekana lakini ujue hatari ya hiyo vita uliyoanzisha.
Don't Hunt what u can't kill[emoji23][emoji23]

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Nyoka anaogopa binadamu kuliko unavyomuogopa wewe, black mamba ana sumu za aina mbili,inayoweza kugandisha damu na inayoweza kuharibu mishipa ya fahamu,, ukimuona achana nae, endelea na shughuli zako,, ukiamua kupambana nae ili kumuua inawezekana lakini ujue hatari ya hiyo vita uliyoanzisha.
Kabisa , ukimrushia hata jiwe uwe unaimudu vita,
 
Nyoka karibu wote wana hulka mmoja..... Huwa wanajitahidi sana ku avoid kukutana ana kwa ana na viumbe ambao ni wakubwa kuliko wao, ni hatari kwao na ambao sio chakula chao.

Nyoka wana sense ya hali yajuu kupitia ulimi na macho yao kubaini kiumbe kinacho wakaribia....... Hivyo akikuhisi/ona kwa mbali kabla hujamuona huwa anajificha na kutulia tuli hadi upite

Na iwapo mtakutana ghafla ana kwa ana Kwenye open space au ukambananisha labda ukatani kwakawaida Koboko huwa kwanza lazima asimamishe kichwa na kutoa onyo kwa mlio mkali wa kupuliza, na ukizidi kumsogelea anaweza kukurushia sumu usoni ili kukupa upofu wa muda ili apate nafasi ya kusepa zake

Koboko huwa hashambulii bila warning labda umkanyage ghafla hapo ata attack bila warning

Kumekua na uongo mwingi kwamba ukikutana naye anakufukuzia hadi akung'ate au anaweza kuua hata mifugo mingi zizini just for fun........ Hii sio kweli
Hili la kurusha sumu pia sio la kweli. Hii ni kwa cobra, tena sio wote, wapo jamii ya "spitting cobra"
 
Mimi nilikutana Naye mbugani akawa anainua kichwa chake.Nikambana na mti kichwa chake na nikamshika mkia wake nikaanza kumzungusha juu Hadi akalegea na kumng'oa meno yake.Nilifanya Hivyo Kwa kutomjua kuwa alikuwa ni black mamba Hadi pale watu wanaojua nyoka wakaja wakamtambua Kwa jina na wanasema nilikuwa nacheza na moto
downloadfile.gif
 
Nyoka anaogopa binadamu kuliko unavyomuogopa wewe, black mamba ana sumu za aina mbili,inayoweza kugandisha damu na inayoweza kuharibu mishipa ya fahamu,, ukimuona achana nae, endelea na shughuli zako,, ukiamua kupambana nae ili kumuua inawezekana lakini ujue hatari ya hiyo vita uliyoanzisha.
Hizo sumu zake zote ni balaa.
 
Back
Top Bottom