Umeshawahi kutana na koboko(black mamba), uliescape vipi maana huyu sio wa mchezo

ndio maana nilisema mimi koboko alipita mbele ya macho yangu na hajafanya kitu ,ila koboko ndio nyoka mshali kuliko wote hilo bush niliokuwepo koboko alimua tu kugonga kuku kibao na mbwa akawaacha wametulia chin na yeye aliuawa maana wahuni walikua wanamuhesabia tu sumu zake maana mbwa wa mwisho aliemgonga hakufa wakajua amefirisika wakampa kichapo hajawah ona
 
Nilikuwa natoka katoro naelekea chato alikuwa anakatisha nikiwa ndani ya hiace. Suka akakaza roho nilisikia kwa nyuma ya gari amegonga na akajifanya kama amekufa suka akadai hajafa pale anasubiri pimbi ajipendekeze amletee mtoa roho
 
Nimeshakutana nae mwaka 2021 nilivyoenda Tabora nlikua na wenyeji karibu nusu ya mwili wake alikua kasimama wima pembeni ya barabara kama mita 30 jamaa wakaniambia tulia tukapita kawaida bila kusitasita tukatokomea kusikikojulikana baada ya kufika mita kama 150 kutoka kwake
 
Hakuna nyoka mshari Duniani mkuu vinginevyo mabalaa yanayotokana na nyoka ingekuwa ni balaa...... Hali hiyo inaweza kutokea bahati mbaya labda nyoka akaanguka na akatua katikati ya mifugo na kusababisha panick, hapo nyoka akikanyagwa au kudonolewa na yeye ata fight back, vinginevyo nyoka hawezi kabisa kuingia mazingira hayo

Kama sio chakula kwake nyoka hanaga muda wa kupoteza kugonga gonga viumbe kisa tu amekasirika........ Snake only bite for selfdefence if it's not a meal

Tumeishi sana na hao nyoka majumbani lakini hawakushambulia hata vifaranga vya kuku kwasababu wanajua varangati la mama kuku litafanya ajulikane anaishi ndani ya nyumba....... Snake are very smart mkuu jaribu tu hata google au Ai utapata majibu
 
Atuongelei nyoka hapa tunaongelea koboko
Huyu kiongoz ni maarafu sababu ni agressive kuliko binamu zake
 
Huyo labda alikuwa anaugua kifaduro
 
Huyo wa pili sijui, ila huyo wa kwanza kuna uwezekano mkubwa hukukutana na black mamba badala yake ulikutana na nduguye mr cobra.

Black mamba si mweusi na ana mwili wa mazoezi na diet hanenepi kizembe zembe, kwa kuongezea anapiga sana cha Arusha kupandisha mori na kujiweka fit.

Nikikutana na nyoka ambaye ni kibonge naweza kumuua hata kwa makofi
 
Duuuuuh angekung'ata kalioooooo
 
kwa upande wangu sikawahi kutana nae ila nisikia ni hatare sana na wanasema sana sana anptkn Tabora, kanda ya ziwa ,Dodoma na Mbeya
Kama ushawahi kutana nae share nasi tujifunze😁
Nilicheza nae kama KGB a.k.a CIA na nilikua kadogo tu miaka kama 10 hiv. Tulikua na brother angu tukamuona kwa mbaali matuta kama 30 -50 hivi, bro akachukua fimbo akamrushia, nyoka aka "dash" fimbo ikapita,kachora "S" kishaakalala chini...
Tukaanza kuulizana vp kakimbia, kapotelea wapi....Lahaula, kitu kikaibuka tuta kama 15 iv kutufkia....🙆🏾‍♂️🙆🏾‍♂️🙆🏾‍♂️bro akarusha fimbo ya pili. Hahahaha si akalala tena chini! Tulichofanya .....tukaanza kudunda kwenye matuta kama( anodi shozi nigga) mbio kurudi usawa wa yeye anakotokea.....yaani yeye akawa anakuja usawa wetu na sie tunarudi anakotoka......tulikimbiaga wewe..... Nadhani yeye mwenyewe alikuja kushangaa hatupo( huyo nyoka). 😅😅😅...na ndala/kandambili tulibebaga mkononi.
Kufika home tunawasimulia wazazi, broo alichezea stiki kinoma noma....akaambiwa alikua ananihatarisha mie kadogo kake😅😅😅
Nb: Yote kwa yote ni Mungu tu ndie alie tuokoa hio siku, na hatukurudi tena huko shamba japokua tulikuaga tumezoea kuenda kila alfajili kutoa Kwale kwenye mitego! Daah! Tulipataka hasara balaa, maana kuja kurudi shamba baada ya wiki tukakuta kwale watatu wameozea kwenye mitego.
 
nimeshawahi muona porini kwenye mifugo nilikua na rafiki yangu wa kimasai aliponionyesha kwanza sikuamini maana alikua kasimama kama cm kadhaa na alikua juu ya jiwe basi nikamwambia tuswage mifugo kushoto akaniambia tulia ile ni hatari japo yeye anaisogelea nilichoshuhudia ni sime ilirushwa ikafyeka kichwa akadansi hapo mpka akakata moto ndipo kumsogelea na kumjifunza ila kuna dawa za wamasai huwa zinaharufu ya kuwakera hivyo nikienda pori lazima niwe nayo kujipaka kuepusha majanga...... si nyoka wa kukaa karibu na makai ila unapomuona we mkwepe tu kujitia ushujaa unaambulia mauti
 
Atuongelei nyoka hapa tunaongelea koboko
Huyu kiongoz ni maarafu sababu ni agressive kuliko binamu zake
DSTV kwenye chaneli ya Net Geo Wild kila siku Jmosi mchana kuna marudio ya Series ya Snake In The City ya wiki nzima
Jamaa na mke wake wanakwenda kukamata nyoka kwenye nyumba za watu, na most of the time wanakua ni Black Mamba....... Ukiangalia namna wanavyo wakamata utajua ninacho maanisha

Black Mamba sio agressive kihivyo ila ni moja ya nyoka wenye sumu kali sana duniani
Na jamaa huwa anasema kabisa Black Mamba unaweza kuishi naye kwenye nyumba ili mradi tu usimbananishe akafikia mhali akaona hatari hapo atashambulia kujihami na sio kuua nyumba nzima kama unavyodhania

Just imagine anamkamata kisha anamuweka kwenye mfuko na akifika porini anamfungua kasimama hapo hapo na nyoka kitu cha kwanza anachofanya ni kukimbilia porini
 
kwa upande wangu sikawahi kutana nae ila nisikia ni hatare sana na wanasema sana sana anptkn Tabora, kanda ya ziwa ,Dodoma na Mbeya
Kama ushawahi kutana nae share nasi tujifunze😁
Ila bora bora hata Koboko....kuna mziki wa "RADI"...asee ule umeme sio! Ukishuhudia matukio yake....huwezi amini.
 
Nmesoma quora ulipoona pia nmesoma uko uko quora kwa watu wanaishi na black mamba zimbabwe mwamba kwa macho yake kaona mtu anakimbizwa na black mamba na anachezea kichapo au uliza wasukuma wa tabora wakuhadithie koboko alievurugwa akiingia kwa kundi la ng'ombe hutenda nini ?
Ila kwa kua umeamua kuwasikiliza Nat Geo endelea tu maana hao hao experts wako walikua wanasema boomslang hana sumu, na baadae wakaja kugundua otherwise ila wanaoishi na hayo majoka hawaaminiki sababu hawana phd
 
Dunia ya leo watu huwa habishani sana kuhusu myth mkuu.
Google it
Uliza Ai
Nenda wekipedia
Angalia Youtube videos
Uliza na Quora
Kisha lete hapa majibu ya unachodai kuhusu Black Mamba kuwa that aggressive

Usilete ngonjera za hearsay hapa
 
Hakika ni cobra, nimechanganya mafaili na mada lengw.
 
Hapo nime kupata maana uongo mwingi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…