Umeshawahi kutana na koboko(black mamba), uliescape vipi maana huyu sio wa mchezo

Nyoka hakivua gamba(ecdysis/moulting) huwa hang ati mwili wake unakuwa soft san na huwa akimbii
 
Sio kweli koboko hawezi kurusha sumu huyo ni swila au cobra
 
Wanafanyaje exactly?

Wanafukuza watu tu wakikutana porini?
Wanavamia boma na kuua Ng'ombe boma zima?
Au anaweza kuvamia mkutano na kuua watu 100?

Hizi ni myth ulizolishwa toka utotoni na ukaamini
Jitahidi kutafuta taarifa sahihi mkuu
Braza tatizo wewe unazungumzia mambo ya kwenye TV na vitabu huku ukibishana na watu walio/wanaouishi uhalisia.

Hakuna sehemu nimetaja mauaji ya watu 100 wala uvamizi wa zizi, ila itoshe tu kusema koboko ni nyoka hatari sana hasa akiwa mkubwa (kama nilivyosema awali nadhani kadri wanavyokua wanaingiwa na kichaa maana wanakuwa wakorofi sana). Kwa ninavyofahamu na nimesoma maandiko kadhaa kuwa koboko hugonga hadi mara 12, sasa hizo 100 labda mnadanganywa huko kwenu.

Kwa experience tu:

Koboko mkubwa aliua familia nzima ya jirani yetu (baba, mama na watoto 8) mwaka 2000. Nikienda Kijiji kile huwa nayakuta makaburi yamepangana hadi yanasisimua.

Tukiwa darasa la 4 classmate mmoja (ke) na kaka zake wawili walikimbizwa zahanati wakafa wote baada ya kugongwa na koboko ambaye aliwindwa na kuuawa kwa mbinde siku kadhaa baadaye.

Kuna wawindaji kule Chato walikuwa wakitoka mawindoni kwenye pori ambalo siku hizi ndo hifadhi inaitwa Burigi-Chato wakakutana na koboko mkubwa karibu tu na barabara akasimama wima. Mwindaji mmoja akajaribu kumzungukia kwa nyuma ampige na gobole huku wenzie wakimzuia na kumsihi watulie nyoka aondoke zake akapuuza. Koboko aligeuka na kumrarua akarest in peace (itambulike pia uwezekano wa koboko kukosea shabaha kwa mbele upo, ila kwa nyuma hakosei na yupo speed zaidi).

Mwezi uliopita nilikuwa kijijini huko Kagera, wanaume wa shoka wa mkoani walipambana kumuua koboko mkubwa aliyeweka kambi shambani kwa mmoja wao karibu na hiyo hifadhi ya Burigi-Chato, nikaenda kushuhudia akiwa kashauawa. Mazingira tu yalionesha shughuli haikuwa ya kitoto.

NB: Hizi ni sehemu tu ya experiences zangu mwenyewe si za kusimuliwa. Misiba niliyoitaja yote niliihudhuria na wali nilikula japo nilikuwa dogo. Japo kama kawaida yetu waafrika, matukio yote hayo ushirikina ulitajwa.
 
My point is..... Koboko ni nyoka mpole sana kwa binadamu na viumbe wengine ambao sio chakula chake as long as you keep the distance, option ya kwanza akikutana na binadamu ni kumkwepa kabla hata hujamuona kwasababu ana sense kali ya kubaini viumbe karibu yake

Koboka ana attack binadamu pale tu anapo sumbuliwa na akabaki na option moja tu ya kujilinda kwa kushambulia....... Hashambulii tu kwakuwa kakuta na binadamu

Kumekua na UONGO mwingi sana kuhusu koboko kuliko UKWELI
Angalia tu Title ya mleta mada alivyochagiza as if ukikutana tu na Koboko you're done.
Hata simulizi zako tu zinaonyesha jinsi myth kuhusu koboko ni uongo.... Eti koboko AKAMRARUA, Koboko only bite(sometimes multiple times) to inject venom sio kurarua

Stori nyingi za koboko ni hearsay tu..... Sijui eti aliua familia nzima as if alikua anafanya msako chumba hadi chumba kuhakikisha kaua wote...... don't get me wrong, Yes anaweza kuua hata watu 100 lakini sio kama mnavyodanganyana

Kaboko hana uadui na biandamu unless umprovoke hapa atajilinda kwa kushambulia.
Nimeishi na kukua mazingira yao toka nimezaliwa hadi naondoka kijiji Singida mpakani na Tabora
Tumeishi nao sana ndani ya nyumba za udongo na tembe na hawakushambulia hata vifaranga wa kuku
 
Koboko (black Mamba) ni nyoka mwepesi katika kujilinda ila ki Msingi nyoka wote wanaogopa wanadamu.

Mara chache Koboko akiwa mkubwa yaani futi 6 na kuendelea anakua Kiburi na anaweza kua na tabia ya kuto ogopa binadamu na viumbe wengine.
Koboko mkubwa hapendi kukaa karibu na maeneo ya watu na inatokea mara chache kushanbulia watu na wanyama.
 
Haya mambo yanakuzwa kwenye maandishi sisi wale tuliotumia sehemu ya maisha yetu maporini tukichunga ng'ombe hawa walikuwa hawatusumbui na kumuua ni rahisi tu. Ukimrushia kitu jiwe anavimba kichwa sehemu ya taya mpaka shingoni sisi tunajua huu ndo wakati sahihi wa kummaliza kabla hajashusha kichwa chuni. Yaani binanadmu unawezaje kuzidiwa mbinu za kupambana na nyoka na kimnyama kama paka? Wanauliwa vizuri tu sema ni elimu na mbinu ya kupambana ndo inakosekana katika maandishi mengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…