Umeumiza watu halafu unataka kuokoka bila kuwaomba msamaha uliowaumiza, hilo haliwezekani!

Mfalme Daudi alimuua Uria ili Daudi aweze kumuoa mke Uria. Kilichotokea ili kulipa hyo dhambi mtoto wake wa kwanza aliyezaa na mke wa Uria alikufa ndo Daudi akapata msamaha wa Mungu.
Mtoto Mchanga alikuwa na Mungu akasema ni sababu Daudi ametenda Dhambi ya kuua watu wengi.

Wakati Dauti anapanda Mlima Molia akitubu dhambi kama alivyoagizwa na Malaika wa Upanga,
Mwenyezi Mungu alimwambia Daudi huwezi kunijengea Nyumba ya Kuabudu kwa dhambi ulizofanya.

Kwa kuwa nilikupa ahadi nasi Nyumba yangu watanijengea wanao. Ndio kuijengwa na Mfalme Suleiman.

Pia Sauli alienda kutela wanyama na mifugo iliyoachwa na W amaleki waliokimbia.

Bwana akamwambia Sauli Kutoa Kutii ni bora kuliko Dhabihu? Na kusikia kuliko Beberu?

Akimwambia lazima aache kwanza Dhambi kuliko kujifanya unaimba nyimbo hadi unalia au kutoa sadaka nyingi.
 
Mungu angekua katili kama unavyomuelezea hapo, dunia ingekuwa chungu sana kwa wakosefu. Ndo maana tunaambiwa M/Mungu ni mwingi wa Neema na Rehema. Pia M/Mungu ni baba wa wote.
Fundisho la mleta mada ni thabiti 100%.

Kiburi cha uzima na uhai ndio kinawafanya wanadamu kuwa wabishi.
 
Yafaa tujifunze ilivyokuwa kwa mtume Paulo ambaye sioalitesa na aliua wakristo tuu, bali pia aliyachoma moto makanisa yao. Lakini Mungu wa huruma na neema alimbadilisha bila masharti yoyote alipokuwa njiani kuelekea Dameski katika kutekeleza harakati zake za madhulumu kwa kanisa(Wakristo). Na aliporudi kujiunga na kanisa watu wengi hawakukubali kuwa huyo ndo yule yule......... Kuna cha kujifunza hapo.
 
Kwani wewe Ndio unaokoa au ni Yesu? Tuanzie hapo
Ndio maana Yesu akasema. Lisilowezekana Kwa mwanadamu Kwa Mungu yote yanawezekana Yakiwemo hayo yote unayoyalalamikia kuwa hayawezekani. Yeye aliifia dhambi ya ulimwengu yeyote unayoijua. Akasema kila ajae Kwangu sitamtupa nje kamwe.
Ni kila ajae kwake Hatamtupa Nje. Kaka mbingu ni ya Mungu si Mali ya mtu
Na kila mtenda mabaya yeyote Ni shetani tu ndani yake. Wewe ni Nani hutaki Mungu amsamehe? Yesu Anasema: Nalikuja kuokoa na kutafuta kile kilichopotea. Nadhani umesaidika
 
Reactions: 511
Tunaokolewa kwa neema tuu na sio kwa matendo!. Isa 1:18 SUV
Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.

Hivyo mtu kuokoka, ukiisha tubu mbele za Bwana, yatosha!.
P
Asante kuni tag.
P
 
Ukiwa kama nani unaniambia hivyo? Wewe ni mdogo wake Mungu?
Sababu nimegundua unakariri biblia badala ya kujifunza biblia,ukishaweza kuchukua mistari tofaut kwenye vitabu mbali mbali na kuunganisha na kupata point moja apo utakuwa umeweza, biblia ni kitabu kilichofungwa seven times ili siyo tu mtu yeyote tu anafungua mihur zake na kukitumia vibaya,ndo maana lazima ujue namna ya kufungua muhur zake,roho mtakatifu awe kazi na practise za kutosha sasa we unategemea umejiandaa kumpinga mungu direct upate kitu uko utasoma tu kama riwaya 🤠🤠🤠
 
Reactions: 511
Mungu angekua katili kama unavyomuelezea hapo, dunia ingekuwa chungu sana kwa wakosefu. Ndo maana tunaambiwa M/Mungu ni mwingi wa Neema na Rehema. Pia M/Mungu ni baba wa wote.
Hakika kabisa....
Kuna msitari katika Biblia unasema, Kama Mungu angehesabu maovu yetu hivi ni nani angesimama?
 
Yaan biblia haijaandikwa kimafumbo imefungwa kabisa kutokujua kama imefungwa,ndo unaonyesha bado unakunywa maziwa
 
Fundisho la mleta mada ni thabiti 100%.

Kiburi cha uzima na uhai ndio kinawafanya wanadamu kuwa wabishi.
Acha tuwe na kiburi tu maana tunajua Neema ya Mungu inatugusa wote na mahali popote na hakuna wa kuizuia ikiwa ya kwamba yeye mwenyewe kashaweka hio neema juu ya watu wake. Kikubwa tumrudie Mungu na kuomba neema yake ituokoe.
 
Watu waovu na wahalifu wengi huwa wanakimbilia kwenye makanisa na kwenye siasa ili kuficha uovu wao.
 
Kuna jambazi mmoja ameiba mali Kenya na kuua watu sasa karudi Tz eti kaokoka na kufungua makanisa na Vitua vya Shell. Huwa namshangaa! Akaombe msamaha kwa aliowauwa Kenya kwanza!
 


Tatizo lako ni kutokujielewa, mtu amaweza mpokea Yes, then akajifunza taratibu akiwa mtii kwa roho mtakatifu kurekebisha njia zake.

Kinachoanza ni maamuzi, then kuwezeshwa kwa kuitembelea hiyo njia katika utii thabiti kwa roho mtakatifu.
 
"Mwenyezi Mungu anachukizwa mno na dhambi"


Mwenyezi Mungu ni mwepesi wa kusamehe
Kama Mungu anachukizwa na dhambi, Alishindwaje kuumba dunia isiyo na dhambi wala uovu?

Mungu huyo hakujua kwamba dunia itakuja kuwa na dhambi adhibiti na kuzuia mapema?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…