Umeumiza watu halafu unataka kuokoka bila kuwaomba msamaha uliowaumiza, hilo haliwezekani!

Mungu angekua katili kama unavyomuelezea hapo, dunia ingekuwa chungu sana kwa wakosefu. Ndo maana tunaambiwa M/Mungu ni mwingi wa Neema na Rehema. Pia M/Mungu ni baba wa wote.
Mungu ni katili sana na hana hata chembe ya huruma.

Mungu aliyeumba dunia iliyojaa uovu, majanga ya asili, njaa, vita, magonjwa n.k ilhali uwezo wa kuumba dunia isiyo na matatizo haya alikuwa nao, Ni mungu mkatili sana aliye ridhia uwepo wa majanga yote haya.
 
{}
 
ulimi uliojaa lawama unaonyesha moyo usio na shukrani. I hope you heal mkuu.
 
Mkuu!
Mkuu rejea mistari miwili hapo chini!
Haijarishi umetenda dhambi za aina gani ukitubu unasamehewa! Ndo kazi ya msalaba! Labda nikupe neno gumu nifungue ufahamu wako! SIKIA: Watu uliowatendea uovu wa aina yoyote, kuna mlango uliofunguliwa (walioufungua wenyewe kwa dhambi au uovu) wakapata uovu huo (Mhubiri 10:8; ... Na yeye abomoaye boma, nyoka atamwuma). Kwahiyo, kilichopelekea kupatwa na yote mabaya kupitia kwako nyuma yako alikuwepo shetani akitimiza neno. Wewe ukiokoka unakuwa umejivua usitumiwe tena na shetani. Hata hivyo kama kuna mali za dhuruma zinazoweza kurejeshwa kama ziko ndani ya uwezo wako inabidi uzirejeshe kama ziko nje ya uwezo wako kuzirejesha basi kazi ya damu ya Yesu msalabani inakusamehe 💯

Luka 3:8
[8]Basi, toeni matunda yapatanayo na toba; ......."


Isaya 1:18
[18]Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
 
Thibitisha kwamba hayupo.
Mungu huyo hawezi kujidhihirisha mwenyewe kwamba yupo wala hawezi kujitetea mwenyewe.

Huu ni uthibitisho tosha kwamba Mungu huyo hayupo.

Kama yupo aje hapa ani prove wrong.

Vinginevyo Mungu huyo mmemuumba vichwani mwenu tu wala hana uhalisia wowote ule.
 
Kama niliemnyang'anya shamba nilimuua nitampata wapi ili kumuomba msamaha?
Mtazamo wako unaangalia watu walio kafibu na wewe tu, na bado wako hai.
Heri hata kama mtu uliyemtenda yupo mbali mfate tuu na umuombee msamahaa kibusara mana kwa simu haileti picha nzuri
 
Kama uliyemkosea hayupo (ulimuua) je bible inasemaje ukitaka kutubu utasamehewa au mpaka nawe ufe ukamuombe huko msamaha?
Haimanishi ivyo cha msingi n kuwa na hali ya kutaka usafisho na kuweza kumshirikisha Mungu huyo mtu alipo akusamehee.Na kweli utasamehewa
 
Kwani Makonda ameamua kuokoka?
 
Uoga upo ila kuna kujisahau kwa sababu sisi sio wakamilifu.
Ni sawa.ila huwa kwa kila mwanadamu huwa kuna roho ya kusita kutenda jambo fulani lisilo jema ila huwa tunapuuzia kuwa liwalo na liwe ambapo huwa tunakosea
 
Kwani Makonda ameamua kuokoka?
Sijui lolote kuhusu huyo Makonda ila hadi uokoke ni mpaka upewe wokovu, anaekupa wokovu hawezi kukubariki ikiwa watu uliowakosea hujawaomba msamaha na kurudisha ulichokichukua.

Kuokoka ni siri ya mtu japo anaweza kuhadaa wengi machoni
 
Ni sawa.ila huwa kwa kila mwanadamu huwa kuna roho ya kusita kutenda jambo fulani lisilo jema ila huwa tunapuuzia kuwa liwalo na liwe ambapo huwa tunakosea
Ndo kutokuwa wakamilifu sasa, ndo maana hata licha ya kusita sita ila bado tunadondokea dhambini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…