Umewahi kuachana na mtu kisa kazidisha mapenzi?

Umewahi kuachana na mtu kisa kazidisha mapenzi?

kuna muda hadi nliamua kuiacha tu simu hovyo ili aishike akute meseji nazochat na mpenz wangu mwngne ili akasirike tuachane ila cha ajabu amezkuta na ameniambia kanisamehe tuendelee yan kiukweli sielew nachomokaje hap Wakuu.
Kuna wengine akikuta kama hivyo unachati na wanawake wengine sasa yeye ndio anazidisha mapenzi maradufu akijua kwamba labda kuna mapungufu upande wake ndio maana umetoka nje... Kifupi hapo huchomoki mkuu 😄
 
Inatisha sana Mkuu, inaogopesha sana maan mtu akikupenda sana nayo vibya,

Maan hat akienda kutafuta utajiri wa kichawi huko bas wew ndo unakuwa pendekezo nambari moja la Mizimu maan ndo mtu anayekupenda sana.
 
Asa ukutane na mkaka ndo ana tabia hizo[emoji18][emoji18]
Madhara ya kukosa malezi yenye upendo utotoni, kiufupi hujui mapenzi/ upendo ni nini, unaogopa na kuona kero kwa sababu ubongo wako haujawa trained kuchakata taarifa za upendo.. how can one be afraid to be loved?

Someone to care
Someone to share
Lonely hours
And moments of despair

To be loved to be loved
Oh what a feeling
To be loved

Someone to kiss
Someone to miss
When you're away
To hear from each day

To be loved to be loved (to be loved)
Oh what a feeling
To be loved
 
Sema ukweli usemwe wanawake wenye shobo + kupenda sana huwa ni wale wabovu yaani unakuta hawana demand ya wanaume kuwatongoza hivyo wanaogopa ukimuacha atabaki single. Ni nadra sana ukute pisi kali kakungangania kama ruba. La hasha.

Vivyo hivyo kwa mwanaume masikini
 
Mara nyingi huwa siyo mapenzi bali ni infatuation au obsession wala usije dhani kuwa unapendwa, mimi imewahi nitokea kwa rafiki tu nilikuwa nampenda hadi akawa anakereka anaona huyu naye vipi akawa anashindwa kuniambia ila kuna vitu vilifanya nigundue hilo na sikumlaumu, mwisho wa siku nilikuja kujishitukia na kugundua kuwa ule haukuwa upendo wa kawaida bali umajinuni tu na sasa hivi wala haupo tena namchukulia kawaida tu
 
Namaanisha umewahi kupendwa na mtu sana, wakati wewe sio kiviile.. mpaka ukaogopa.. ukaona kabisa tunakoelekea huyu atakuja kufanya kitu cha ajabu.. au atakuja kuniletea matatizo. Yaani unapendwa hadi inakua kero..!? Kuna muda mapenzi yakizidi aisee inaboa mtu mpaka unaona ni nini hiki Mungu baba?

Kuna binti mmoja nilianzisha naye mahusiano kiutani utani tu.. baada ya muda binti si akakolea? Jamani yule binti alikua ana mapenzi ya kitoto yaani kila dakika anataka kuwa na mimi, nikiwa nae hataki niondoke, nikiondoka ni simu kila dakikaa yani hadi nashindwa kufanya kazi! Na ole wangu atume msg nisijibu.. inakua kesi. Mwisho nilishindwa nikaamua kubwaga manyanga japo demu alikua pisi balaa!

Vipi wewe umewahi kukutana na hali kama hii ukaona inavyokera?
Eeh inakera. Mimi kuna mtu mtu mzma na akili zake kila wakati anapiga piga simu kama vile sina kazi za kufanya. Mtu anapiga simu hadi saa tano usiku.
Hana hata la kuongea ili mradi tu yani anapiga piga simu kila mara imebidi niache kupokea.
 
Labda kweli
Ndivyo ilivyo. Kuna dada mmoja miaka hiyo niliwahi kuingia naye kwenye mahusiano ya kingono, aseeeee sitosahau kadhia ile......

Alikuwa ananisindikiza hadi chooni na analazimisha aingie ndani wakati najisaidia [emoji15], sikuwa serious sana juu ya penzi letu na tangu mwanzo nilimwambia ukweli maake kiuhalisia ni yeye aliyesababisha hadi tukawa wapenzi.

Nililazimika kuhama mtaa kimya kimya nikampotezea mazima. Mama yake alinipigia kuniomba nisimsababishie binti yake kifo maana alitaka kujiua, wakati huo Mimi sikuwa na undani hiiiiivo juu yake.

Nashukuru baadaye nilijinasua ila ilikuwa tafrani kweli kweli
 
Haya mambo yawe kwa kiasi na wote muende kwa wavelength moja. Mmoja akiwa na upendo kupitiliza wakati mwingine anachukulia kawaida ndipo yanapokuja maneno ya namna hii.
Msituumize sisi tunaojua kupenda kwa kubanana
 
Madhara ya kukosa malezi yenye upendo utotoni, kiufupi hujui mapenzi/ upendo ni nini, unaogopa na kuona kero kwa sababu ubongo wako haujawa trained kuchakata taarifa za upendo.. how can one be afraid to be loved?

Someone to care
Someone to share
Lonely hours
And moments of despair

To be loved to be loved
Oh what a feeling
To be loved

Someone to kiss
Someone to miss
When you're away
To hear from each day

To be loved to be loved (to be loved)
Oh what a feeling
To be loved
we jamaa una kipaji cha kutunga mashairi
trust me bro
 
Ndivyo ilivyo. Kuna dada mmoja miaka hiyo niliwahi kuingia naye kwenye mahusiano ya kingono, aseeeee sitosahau kadhia ile......

Alikuwa ananisindikiza hadi chooni na analazimisha aingie ndani wakati najisaidia [emoji15], sikuwa serious sana juu ya penzi letu na tangu mwanzo nilimwambia ukweli maake kiuhalisia ni yeye aliyesababisha hadi tukawa wapenzi.

Nililazimika kuhama mtaa kimya kimya nikampotezea mazima. Mama yake alinipigia kuniomba nisimsababishie binti yake kifo maana alitaka kujiua, wakati huo Mimi sikuwa na undani hiiiiivo juu yake.

Nashukuru baadaye nilijinasua ila ilikuwa tafrani kweli kweli
Maanake alishamweleza hadi mzazi wake kuhusu mapenzi yenu😳😃😃🤔
 
Maanake alishamweleza hadi mzazi wake kuhusu mapenzi yenu[emoji15][emoji2][emoji2][emoji848]
Baada ya kuwa tumeingia kwenye mgogoro (kila wakati anataka tuwe pamoja)mawasiliano kila dakika, nikichelewa kujibu sms taabu, akipiga simu ikawa inatumika taabu, kaniganda kama kupe, nikaanza kumpotezea na kumkwepa mdogo mdogo shida ikaanzia hapo. Tukakorofishana nikamwelezea mapenzi yaishie hapo.....ilikuwa shida sana kwao ikamlazimu amweleze mama yake kila kitu kutuhusu
 
Namaanisha umewahi kupendwa na mtu sana, wakati wewe sio kiviile.. mpaka ukaogopa.. ukaona kabisa tunakoelekea huyu atakuja kufanya kitu cha ajabu.. au atakuja kuniletea matatizo. Yaani unapendwa hadi inakua kero..!? Kuna muda mapenzi yakizidi aisee inaboa mtu mpaka unaona ni nini hiki Mungu baba?

Kuna binti mmoja nilianzisha naye mahusiano kiutani utani tu.. baada ya muda binti si akakolea? Jamani yule binti alikua ana mapenzi ya kitoto yaani kila dakika anataka kuwa na mimi, nikiwa nae hataki niondoke, nikiondoka ni simu kila dakikaa yani hadi nashindwa kufanya kazi! Na ole wangu atume msg nisijibu.. inakua kesi. Mwisho nilishindwa nikaamua kubwaga manyanga japo demu alikua pisi balaa!

Vipi wewe umewahi kukutana na hali kama hii ukaona inavyokera?
Nilikuwa naogopa sana kupendwa sana yaani na ninabahati mbaya sana na hilo yaani wanakuwaga kama wamepandwa na mapepo kwakweli nikiona hivyo nilikuwa najivuta mdogo mdogo mpaka tuachana

Nishavunjiwa Simu nishapigwa makofi wameshazimia yaani upendo na wivu vinakuwa juu hata kusimama na Dada ako tu inakuwa tabu loh
 
Back
Top Bottom