Umewahi kuachana na mtu kisa kazidisha mapenzi?

Umewahi kuachana na mtu kisa kazidisha mapenzi?

Namaanisha umewahi kupendwa na mtu sana, wakati wewe sio kiviile.. mpaka ukaogopa.. ukaona kabisa tunakoelekea huyu atakuja kufanya kitu cha ajabu.. au atakuja kuniletea matatizo. Yaani unapendwa hadi inakua kero..!? Kuna muda mapenzi yakizidi aisee inaboa mtu mpaka unaona ni nini hiki Mungu baba?

Kuna binti mmoja nilianzisha naye mahusiano kiutani utani tu.. baada ya muda binti si akakolea? Jamani yule binti alikua ana mapenzi ya kitoto yaani kila dakika anataka kuwa na mimi, nikiwa nae hataki niondoke, nikiondoka ni simu kila dakikaa yani hadi nashindwa kufanya kazi! Na ole wangu atume msg nisijibu.. inakua kesi. Mwisho nilishindwa nikaamua kubwaga manyanga japo demu alikua pisi balaa!

Vipi wewe umewahi kukutana na hali kama hii ukaona inavyokera?
Kuna jamaa muda wote linataka akupigie cm,muongee,mchart....yaan kuandika paragraph linalohusu MAPENZ siyo shida zake,ananikwaza Sanaa hivyo nimeanza kumkwepa simtaki Tena,naona anatumia muda mwingi kuwaza mapenzi badala ya kutafuta fursa,!
Hela huna, unatumia muda mwingi kuongelea mapenzi, mara nakupenda na bra bra nyingi
 
A clingy Person, ana tatizo la emotional over dependancy. Kwenye akili yao wanatafsiri mpenzi wake kama kitu na si mtu, most of them are controling.

Ni watu hatari kuwa nao, maana mambo yakienda tofauti anaweza kuua/kujiua.

Kwenye uwanja wa mapenzi "mbarikiwa" ni yule aliyepata mpenzi muelewa, na anayeweza kucommunicate vizuri, kitu kikitokea anatanguliza neno "tutaliongelea hili" na si kujump kwenye hitimisho lililopo kichwani mwake. Ukienda mahali akwambie "take care" and let me know ukirudi/ukiwa unarudi.

Anyways hayanaga muongozo, ukipata mtu muelewa na wewe si muelewa utahisi hakupendi. 😅
 
Kuna binti mmoja ni mchaga alinipenda sana na alikua anawivu hatari imargine mm sio mtu wakupenda video calls lakin yy atapiga kila mda na hapo usipopokea ni lawama kila siku. Kuna mda anatuma mesej nyingi m najibu kwa meseji moja hapo inakua kesi na napigwa block juu ila uzuri nilikua simtafuti yeye mwenyewe atajishtukia baada ya week tena anaanza mahusiano nilikuja kuachana nae baada ya kuniambia mambo ya ndoa nikasingizia wazazi wangu wamekataa nisioe mchaga.
 
Bila shaka ni kukosa kazi,mtu kama anakaz hawez kuwa fala hvyo
Wengine wana kazi lakini ndio hivyo hivyo. Mi kuna wakati nilijichanganya kwa mfanyakazi mwenzangu nikawa napiga. Yaani yule dada alikua mda wote anaacha kazi zake anakuja kushinda ofisini kwangu! Kuanzia asubuhi, chai anataka twende wote, lunch tuongozane, tukitoka job tutoke wote... mpaka ofisi nzima wakajua kuna kitu kinaendelea pale wakati mi sikutaka ijulikane.. nilijuta sana kumla.
 
Mwanamke akikupenda anakuwa kero
 
Mkuu wanawake wa hivyo ni wakupiga chini, wanawake ni wajanja sana anajifanya kakolea kumbe anakufanyia heart analysis na ole wako upumbazike hakuna rangi utaacha kuona kwenye hii dunia.

Wanawake ni wajanja sana na wanatuonaga sisi wanaume ni wajinga
 
Namaanisha umewahi kupendwa na mtu sana, wakati wewe sio kiviile.. mpaka ukaogopa.. ukaona kabisa tunakoelekea huyu atakuja kufanya kitu cha ajabu.. au atakuja kuniletea matatizo. Yaani unapendwa hadi inakua kero..!? Kuna muda mapenzi yakizidi aisee inaboa mtu mpaka unaona ni nini hiki Mungu baba?

Kuna binti mmoja nilianzisha naye mahusiano kiutani utani tu.. baada ya muda binti si akakolea? Jamani yule binti alikua ana mapenzi ya kitoto yaani kila dakika anataka kuwa na mimi, nikiwa nae hataki niondoke, nikiondoka ni simu kila dakikaa yani hadi nashindwa kufanya kazi! Na ole wangu atume msg nisijibu.. inakua kesi. Mwisho nilishindwa nikaamua kubwaga manyanga japo demu alikua pisi balaa!

Vipi wewe umewahi kukutana na hali kama hii ukaona inavyokera?
Ulimkosea sana muumba mkuu!!

Ipo siku utamkumbuka huyo Binti!

Ungetafuta namna ya ku handle Hali ile sio kubwaga manyanga!!

Ulimkataa mke uliepewa na Mungu mkuu!!

Kwa kawaida upendo wa Binti ukizidi kwako ni dalili kuwa mungu amekupa huyo!!

Kwa kawaida.wanawake wengi Huwa hawapendi kirahisi sisi wanaume!!yaani wengi wapo kimaslahi tu!!

Kwa usalama wako nenda kapige magoti umuombe Mungu msamaha labda anaweza kukusamehe!!

So sad!you handled badly!!
 
Kuna wengine akikuta kama hivyo unachati na wanawake wengine sasa yeye ndio anazidisha mapenzi maradufu akijua kwamba labda kuna mapungufu upande wake ndio maana umetoka nje... Kifupi hapo huchomoki mkuu [emoji1]

Abebe tu msalaba wake asituachie sisi [emoji28]
 
Hiki mnachokijadili humu ndo nachopitia saivi, mpak nawaza ni nin hiki Nimemfanya huyu mwanamke ?

Maan hat kam ningempa Limbwata lakn bado lisingefkia kiwango hiki cha mapenzi yaliyopitiliza anayoonyesha,

kuna muda hadi nliamua kuiacha tu simu hovyo ili aishike akute meseji nazochat na mpenz wangu mwngne ili akasirike tuachane ila cha ajabu amezkuta na ameniambia kanisamehe tuendelee yan kiukweli sielew nachomokaje hap Wakuu.
Nipe namba yake
 
Experience is the best teacher.
Nafikiri ni uzoefu mbaya tunaopitia na kuuamini tu. Wapo waliokuwa hivyo na wakaona sawa tu. Uhusiano bila wivu na controlling hakuna mapenzi hapo.
 
Back
Top Bottom