Umewahi kukuta watu wanakula chakula gani ukakishangaa?

Nilikuta watu wanakula aisee nilishangaa.
 
Kuna sista duu wa masaki alikuja home akashangaa nakula ugali maharage akauliza hapa kuna shule ya boarding?

Iringa kuna mboga inaitwa mkalifya,na uroho wangu wote nilichemsha, ni chungu kuliko uchungu wenyewe
Naijua hiyo halafu unakuta mtu anaila anasifia kabisa kuwa ni tamu.
 
Zambia wanakula yale mawashawasha yenye manyoya yanayowasha Yana rangi rangi halafu yanatisha na tukuyu wanakula panya buku.
Yale yenye manyoya hayaliki ni yale yanayopatikana kwenye miembe yanakuwa hayana manyoya yanakuwa makubwa sana.
 
Nyama ya ng'ombe mbichi, yani watu wamebeba sahani wamesimama zizini pale ng'ombe kachinjwa wakapewa nyama wakakaa kula.....nlihisi kichefuchefu
Hii tabia nilikutana nayo Moshi aisee. Kwanza picha linaanza naletewa nyama mbichi nile aisee nikasema nitasubiria ya kuchoma Asante mzee. Nikaletewa damu mbichi nikachomoa, round ya tatu nikaletewa damu imechemshwa na supu ikabidi ninywe tu ili nisije onekana nadharau.

Ila dah aisee
 
Niikuta wameloweka ngozi ya ng'ombe kwenye maji kesho yake mchana ikatolewa ikakwanguliwa manyoya ikakatwa vipande ikapikwa iliwa usiku. Bahati nzuri nina alergy ya nyama nyekundu kwahiyo nikapata excuse ya kutokula ile mboga
Hili suala la Kula ngozi ya ng'ombe watu wengi wanakula ila ukimuuliza kabla hajatambua hujifanya kuwa hawezi Kula na inaliwa sana sana

Kimsingi kongolo kinacholiwa pale ni ngozi ya ng'ombe pekee na ulaji wa kongolo ni mkubwa sana ktk jamii yetu inayoishi mijini
 
Wala 🐌,konokono wote,wala mende wote,wala panya wote,wala nyau wote,wala wou wote nawashangaa na wafananisha na mnyama,🦁(Animals)πŸ€”πŸ€”πŸ€”
 
Wala 🐌,konokono wote,wala mende wote,wala panya wote,wala nyau wote,wala wou wote nawashangaa na wafananisha na mnyama,🦁(Animals)πŸ€”πŸ€”πŸ€”
Hata wewe ni mnyama.sio kufananisha...sisi ni wanyamaaaaaa
 
Watu wana kula utumbo wa kuku na vichwa vya kuku, punda na panya kweli kweli, ni likua nasikia tu ila nilishuhudia mwenyewe......
Niliwahi poteza demu niliye mzima baada ya kuona anakula utumbo wa kuku,na ikawa mwisho wa uhusiano hapo hapoπŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…