Umewahi kukutana ana kwa ana na mnyama gani mkali?

Wakati tupo jkt makuyuni Ile kambi ipo mbuga ya wanyama , tulikua tumedoji fatiki 🤣 🤣 🤣 tumeenda kisima cha chini kwa laiboni (wamasai) tukakutana na nyati live Yesu wangu . Hata sikumbuki tulifikaje kambini
 
Alipita tembo shambani kwetu aisee na huyo alikuwa mtoto that giant ni hatarii anavunja kahawa kama mwanadamu anavyovynja stick za kuchokonolea meno. wanyama wa mwituni ni wakubwa sana.
 
Mimi kuna siku niko na Pikipiki nimetoka site huko nyengedi napanda Milima ya rondo mida ya saa 2 usiku aisee Mara simba huyu hapa nilianguka na Pikipiki nikainyanyua sikugeuka nyuma nilipofika kijijini palepale nilizimia.

Kuna siku tena natoka makangaka naelekea kiranjeranje kupanda basi saa 12 Asbh niko na miguu aisee ghafla naona simba dume na jike huwez amini simba Walikuwa hawana njaa walinisindikiza ila Mimi begi nilitupa na Viatu nilikimbia baadae akaja jamaa wa baiskeli aliokota viatu na begi kauliza nani mwenye begi nikamtajia vitu vilivyopo ndani kitambulisho na nguo akanipa begi.

Kuna siku tena niko speed natoka kinyope nakuja Rutamba pale katikati chui huyu hapa kainua miguu aisee nilinyosha wanguwangu akaruka pembeni.

Siku nyingine tuko na gari Tukaona tembo wanne ruangwa wanapita.

Kiboko ashanikosa kwenye mtumbwi mto ruvuma daraja la mkenda.hakuwa na mtoto alikuwa anaibuka nasikia akiwa na mtoto ndo anakuwa mkali.

Nyoka ndo sana barabarani nishkutana nao zaidi ya Mara tatu ila wadogo wadogo sijawahi kukutana na joka kubwa na kuna siku tumekaa kwenye mti ghafla nyoka kadondoka.

Aisee tunaoishi huku lindi tumepakana karibu sana na pori kubwa la selous yaani tunapocheza Cheza huku njiani tunakutana na viumbe machachari hapa ninahamu tu kuja kukutana na mamba live ndo sijawahi kumuona.
BINADAMU.
 
Siku nakatiza misitu ya Mabwe Pande nikakutana na Mamba wawili wanatiana. Kuniona wakashtuka. Wakaanza nikimbiza. Nilikimbia sana nikapanda juu ya mti mrefu yule dume naye akawa anapanda anile. Nikamtemea mate usoni halafu nikamtoboa jicho moja na kijiti ndo kurudi chini.
 
Hayo majina ya huko unapoishi yanaonesha ni maporini Sasa unashangaa nini,we ndiyo umevamia maeneo ya wanyama pori.Angalia tu usiingie kwenye 18 zao.
 
Siku nakatiza misitu ya Mabwe Pande nikakutana na Mamba wawili wanatiana. Kuniona wakashtuka. Wakaanza nikimbiza. Nilikimbia sana nikapanda juu ya mti mrefu yule dume naye akawa anapanda anile. Nikamtemea mate usoni halafu nikamtoboa jicho moja na kijiti ndo kurudi chini.
kwamba alitaka akule😂😂.

lakini mamba wa mabwepande jau sana.
 
Back
Top Bottom