Haya mambo ya mahusiano muhimu watu wakae na wenzao kwa machale, wekeza kwa yule anayeonekana akili yake imetulia kwako, usiwekeze kwa mtu mwenye mapepe ambaye anaonesha dalilu zote safari yenu haitabiriki huko mbele.
Hata kama mwanamke/mume ataonekana kuwa pamoja nawe mwanzo, endelea kuwekeza kwake huku unamchunguza, na wala usiogope kumuwekea mutihani ya majaribio ili kupima uthabiti wa mapenzi yake kwako, mpe mitihani mpaka utapojiridhisha yuko sawa huku ukiwekeza kiasi.
Usiwekeze kingi kama vile umeshamuoa, au ameshakuzalia, wekeza kwa akili ukiendelea kumtazama lakini asijue, ili asijue siku nyingine akitaka kitu kama pesa mwambie sina hata kama ipo, ili uione reaction yake kwako, akiwa na tabia ya kuropoka kila mara huyo muache hafai.
Pale utapoona hatabiriki, anza kutafuta chimbo lingine la kuhamia pindi utakapoachana nae, huku ukiendelea kumsindikiza kuisubiri hiyo siku atakayoropoka ukimnyima kitu ndio umbwage rasmi, hapo hutakuwa na lawama.
Sent from my SM-G900H using
JamiiForums mobile app