Umewahi kupata maumivu kutoka kwa mtu uliyewekeza muda, upendo na imani yako kwake?

Umewahi kupata maumivu kutoka kwa mtu uliyewekeza muda, upendo na imani yako kwake?

Haya mambo ya mahusiano muhimu watu wakae na wenzao kwa machale, wekeza kwa yule anayeonekana akili yake imetulia kwako, usiwekeze kwa mtu mwenye mapepe ambaye anaonesha dalilu zote safari yenu haitabiriki huko mbele.

Hata kama mwanamke/mume ataonekana kuwa pamoja nawe mwanzo, endelea kuwekeza kwake huku unamchunguza, na wala usiogope kumuwekea mutihani ya majaribio ili kupima uthabiti wa mapenzi yake kwako, mpe mitihani mpaka utapojiridhisha yuko sawa huku ukiwekeza kiasi.

Usiwekeze kingi kama vile umeshamuoa, au ameshakuzalia, wekeza kwa akili ukiendelea kumtazama lakini asijue, ili asijue siku nyingine akitaka kitu kama pesa mwambie sina hata kama ipo, ili uione reaction yake kwako, akiwa na tabia ya kuropoka kila mara huyo muache hafai.

Pale utapoona hatabiriki, anza kutafuta chimbo lingine la kuhamia pindi utakapoachana nae, huku ukiendelea kumsindikiza kuisubiri hiyo siku atakayoropoka ukimnyima kitu ndio umbwage rasmi, hapo hutakuwa na lawama.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Kama Betting
 
Hii ni tabia ya kusisitiza maumivu yako wakati ulijitakia mwenyewe ni tabia mbaya kabisa.

Unawekezaje kwa mtu anayeweza kukuumiza? Hujamchunguza kabla ya kujipendekeza kwake?

Unaachiaje mtu mwingine akuumize?

Huoni kwamba hii tabia ya kuacha mtu mwingine aweze kukuumiza na kulialia ni tabia ya kibinafsi sana?

Huoni kwamba, kwa mfano, mtu asipokutaka ana uhuru wa kuendelea na maisha yake, na wewe kudai anakuumiza ni kumlazimisha aendelee kuwa nawe kwa nguvu?

Huoni kuwa hizi habari za kusisitiza sana maumivu yako bila kuangalia wengine wanataka nini ni emotional blackmail?

Muachie mwenzio aende, tafuta mwingine.

Mtu baki kuweza kukuumiza ni kosa lako, umemuachiaje aweze kukuumiza?
Kinachowaumiza vijana ni kudanganywa na sio chengine Mkuu.
 
20231129_150606.jpg
 
Mahusiano hamna.

Niliowakopesha pesa tu ndio bladifakeni.
 
Hii ni tabia ya kusisitiza maumivu yako wakati ulijitakia mwenyewe ni tabia mbaya kabisa.

Unawekezaje kwa mtu anayeweza kukuumiza? Hujamchunguza kabla ya kujipendekeza kwake?

Unaachiaje mtu mwingine akuumize?

Huoni kwamba hii tabia ya kuacha mtu mwingine aweze kukuumiza na kulialia ni tabia ya kibinafsi sana?

Huoni kwamba, kwa mfano, mtu asipokutaka ana uhuru wa kuendelea na maisha yake, na wewe kudai anakuumiza ni kumlazimisha aendelee kuwa nawe kwa nguvu?

Huoni kuwa hizi habari za kusisitiza sana maumivu yako bila kuangalia wengine wanataka nini ni emotional blackmail?

Muachie mwenzio aende, tafuta mwingine.

Mtu baki kuweza kukuumiza ni kosa lako, umemuachiaje aweze kukuumiza?
Hapa umeongelea wale ambao ni marafiki tu hawana familia,ila kwa waliokwisha kuwa na familia( mtoto/watoto) ni ngumu mno
 
Wengi wengi wetu hua tunavipuuzia vitu vidogo vidogo (red flags) wakati tunaanza mahusiano kwa kufubazwa na penzi. Tunashindwa kufanya maamuzi yatakayo athiri maisha yetu in a long run.

Tunakua tumepoteza muda, rasilimali, hisia na tumepoteza watu ambao kwa namna moja au nyingine wangekua na msaada kwetu.

Ni ngumu sana kumshauri mtu na namna pekee ni mtu mwenyewe kuyapitia (learning from exprience).
Umeongea vyema sana,kupuuzia hizi red flags ndo kumetuumiza tulio wengi,mfano unaona kabisa mtu ni muongo,unapuuza,msaliti unapuuza,mbinafsi unapuuza kwa kujipa moyo labda ataach,kumbe ndio asili yake,mwisho wa siku mambo yanaharibika
 
Hapa umeongelea wale ambao ni marafiki tu hawana familia,ila kwa waliokwisha kuwa na familia( mtoto/watoto) ni ngumu mno
Hapo ndipo kuna umuhimu wa kumchunguza vizuri mtu utakayekuja kujenga familia naye na kuwa na watoto.

Pia, watu wametalikiana kwa maelfu ya miaka.

Vinginevyo, kama unathamini sana uhuru wako na unaogopa sana kuumizwa, kukataa ndoa nayo ni option.

Sio kila ukiona mwanamke mwenye matako makubwa tu unatangaza ndoa.
 
Back
Top Bottom