Umewahi kutana na Mpenzi kichefuchefu wa namna hii?

Umewahi kutana na Mpenzi kichefuchefu wa namna hii?

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Demu nimekaa naye kwenye uhusiano kama miezi kama 10 hivi. Namsaidia anapokuwa na uhitaji sababu kwa muda sasa hayupo kazini. Namlipia pesa ya chakula, umeme n.k

Juzi juzi kaomba nimpatie pesa aende kwenye harusi ya ndugu yake Kilimanjaro. Nikamwambia sidhani kama ni lazima sana aende maana hayupo kazini na anataka mchango 150,000. Nauli na matumizi 100,000 na 100,000 ya sare.

Nikamwambia hapana sipo vizuri nami mambo yametindinganya kidogo.but nikamkumbusha kuwa nlimwambia atafute biznez ya mtaji wa wastani tu kiasi kisichozidi *********** then nimpe mtaji miezi 4 imekatika hamna majibu.

Akawa mkali. " Usitake kuninyanyasa na vicent vyako. Kukuomba tu pesa umeanza kunichambua, kama hutaki nisaidia basi niache. Nitapambana mwenyewe wala sikulazimishi"

Hii ni kama mara ya 4 anatumia kauli hiyo. Kuwa tuachane kama vipi huwa namwambia tu yaishe tusigombane.

Nikamjibu tu "Sawa" sikuandika kingine nika mblock. Baada ya siku 3 akajifanya amekosea kutuma msg ya kawaida tu sikujibu kitu. Akakosea tena mara ya pili. Sikujibu kitu. Mara ya tatu akapiga simu nikapokea nikamuuliza nani mwenzangu. Akakata simu.

Akaanza kutuma msg kuwa "yaani hatujawasiliana siku mbili umeshatafuta malaya wako. Hukuwa ukinipenda...na nitakuja mvuruga huyo malaya wako mpaka ashindwe kujitambua"

Sikumjibu. Baadaye akapiga this time ametulia na kuanza niuliza nipo wapi akitaka tuonane, nimemwambia tu sina nafasi nipo busy sana kwa sasa. Ameanza tuma msg akilaani nimemchezea tu nimemwacha, Mungu wake atamlipia...hakutegemea n.k.

Mimi ndiyo nimesha move on na ninashukuru zile pesa nlikuwa namtumia sasa nazisave na kuwapa wahitaji wengine na kutumia mimi binafsi. Kuvuja kwa pakacha nafuu kwa mchukuzi.

Nikakumbuka waswahili wanasema "UNATISHIA KUJAMBA WAKATI UNAHARISHA"
 
daah kiukweli sijui mnapataga wapi ujasiri wa kuitolea nje mbususu, na hata haujawahi kuifumania!!,

kiukweli kwangu mimi, kama mbususu ikishatambua makosa yake na ikarudi kinyumenyume kama hiyo yako huwa sinaga ujanja kabisa,kiufupi hua ninakuwa taabani kabisa
 
Malezi ya kuaminisha kuwa mtoto chochote anachotaka akililia atapewa huwa yanakuja kuleta changamoto kubwa sana kitabia kama hizi.

Hako kabinti kana dosari ya kitabia inayoitwa "Narcissism". Kwakifupi hapo hakuna mtu wa maana huyo tabia yake imeshakuwa damaged hadi atakapoamua yeye kuona inafaa kuadabika. Kamekosa adabu sana kiasi kwamba kanahisi kapo entitled kupata kanachotaka.

Sasa wacha kakapewe mimba huko kachakazwe na kakose hata mwanaume wa kukagonga. Shenzi kabisa.
 
Kwa kweli mashuhuri yanamaliza sana pesa.
Ifikie stage tuwe tunawachangia kidogo na hakuna kwenda.
Maana sisi wanawake kuhudhuria sherehe gharama sana sijui kitambaa lace mita moja 25,000 ukiweka na mashono hapo lazima ikatike si chini ya 140,000.
Bado kiatu.
Bado make up.
Bado kucha.
Bado nywele.
Bado nauli.
Bado hujapeleka zawadi.
Sijui kumfuta jasho.
Afu huyo demu wako mpige chini tu.
Maana hana aibu anaombaje hela ya harusi nyingi hizo?
Na mineno ya karaha juu.
Hajui kwamba sasa hivi wanaume wachache sana wanaohudumia wanawake wengi wa wanaume wanapenda mserereko na free k.
Ila mkuu jiandae huyo demu akishapigwa na jua lazima ajute na atakusumbua sana.
 
Back
Top Bottom