UMEWAHI MPAMBANIA MTU HADI AKAPATA KAZI KISHA AKAANZA KUPAMBANA WEWE UONDOLEWE KAZINI!??

UMEWAHI MPAMBANIA MTU HADI AKAPATA KAZI KISHA AKAANZA KUPAMBANA WEWE UONDOLEWE KAZINI!??

Dah umenikumbusha mbali sana!

Nilikuwa mwenyekiti wa kamati ya kuajiri coordinator wa kitengo kwenye taasisi fulani hivi. Tukaishia kuita watu watatu kwenye interview - Mbotswana, Msauzi na Mbongo mwenzangu. Mbongo interview alifanya vizuri ila hakumzidi Msauzi na upepo ulivyokuwa unaelekea Msauzi pengine angepata ile kazi. Hiring committee ilikuwa na memba wanne na mimi mwenyekiti wa 5. Kwenye kupiga kura Mbongo na Msauzi wakapata kura mbili mbili na kura yangu ndiyo ikawa ya kufanyia maamuzi. Basi nikawaambia kuwa candidates wote wawili wako poa na mimi nampigia huyu Mbongo na visababu pale nikatoa. Jamaa akapata kazi...kwa mwezi dola 6,000 + marupurupu na safari/per diem kibao.

Kwani hata miezi mitatu iliisha? Kmmk Mhaya yule alianzisha vita na mimi mpaka nikaona hapa nikizembea atakuja kuniua. Niliamua kuacha kazi na kuhamia sehemu nyingine. Na nilimuaga vizuri tu.

Nilipoondoka tu kumbe alianzisha ligi na jamaa mwingine Mnaijeria. Hapo naona alikwama maana eti walimkuta amefariki nyumbani kwake kwa risasi ya kichwa. Polisi walipochunguza wakaishia kusema kuwa ilikuwa ni suicide japo hakukuwa na suicide note. Ndo ukawa mwisho wa mpuuzi yule.

Baadaye nilipokuja kukutana na yule Mnijeria nikamuuliza bifu lenu na Deodorus liliishaje, akaishia tu kusema kwa lafudhi yao ile nzito " ma braza, it is done!". Hata sijui alimaanisha nini!

Kuanzia hapo simwamini mtu hasa kwenye haya mambo ya ajira!
Bro Watu si wema tena mkuu Wangu... Poleee ndo tunajifunza.... Ndomana Mzee wangu mmoja Alikuwa hataki mazoea na ndugu Wala Rafiki SIJUI Alikuwa anasema Kila mtu ajipambanie ....Sasa NDIO nimejua Alikuwa na maana gani
 
Kawaida sana kibongobongo, mi nishawahi kumleta mfadhili na alikuwa na bajeti ya $5M nikamuunganisha na rafiki yangu muhimu kbs niliyemuamini, lakini akanichafua sana hadi mfadhili mwenyewe akashangaa na akasema nyie watu hampo serious, akakata bajeti hadi $500k na akasema km kitaendelea atafuta mradi na jamaa akakazana hadi mzungu akasema bora nipeleke hii pesa Senegal, akaishia hapo na wote tukabaki makapuku hadi leo, sadly!
 
Poleee mkuu
 
Hawa walikuwa wawili mabinti.
Nilipohamia hapo niliwakuta hawana kazi,walikuwa na desturi mara naomba buku mara jero ikanichosha.
Baba yao akanambia kama kuna kazi huko wataftie na hawa ndugu zako.
Haikupita wiki woote nikawapeleka kwenye hotel moja.
Mwanzo ilikuwa fresh,lakin baada ya muda kama mwezi wakawa hawanisalimii,wananikwepaa😀😀😀
Sikuwahoji lakin walianzisha kampeni Mimi nihame pale home😂😀
Mbaya zaidi Mimi nikapoteza kazi eeeehh nilijutraaaa😂😂
 
Hawa walikuwa wawili mabinti.
Nilipohamia hapo niliwakuta hawana kazi,walikuwa na desturi mara naomba buku mara jero ikanichosha.
Baba yao akanambia kama kuna kazi huko wataftie na hawa ndugu zako.
Haikupita wiki woote nikawapeleka kwenye hotel moja.
Mwanzo ilikuwa fresh,lakin baada ya muda kama mwezi wakawa hawanisalimii,wananikwepaa😀😀😀
Sikuwahoji lakin walianzisha kampeni Mimi nihame pale home😂😀
Mbaya zaidi Mimi nikapoteza kazi eeeehh milijutraaaa😂😂
Duuh poleee kiongozi
 
Hatari sana.. Watu waone tu kwa macho na sura zao zinazotia huruma wakiwa wanatafuta.. Ngoja umpambanie akae ndio utajua sura yake halisi.
 
Back
Top Bottom