Umewahi muona paka wa aina hii? Anaitwaje kwa Kiswahili?

Inasikitisha sana watu kuwaua hawa jamaa. Bahati nzuri nchi inasehemu kubwa ya hifadhi vinginevyo wangeisha. Elimu ya kutosha itolewe. Tumekuwa wakatili sana kwa wanyama.
 
wanakuwaga na mikia mirefu kuliko paka wa nyumbani na pia ni warefu zaidi.. macho yao usiku ukiwamulika na tochi yanang'aa zaid ya paka wa nyumbani.
 
Wewe ni mwongo. Huyo mnyama wa porini anazaliwaje nyumbani? Isitoshe ni miongoni mwa wanyama wasioonekana hovyo. MWONGO MKUBWA WEWE.
Mkuu ni elimu tu na kutokujua mambo ndiomaana kaandiKa hivo[emoji1787][emoji23].. jamaa kaandika sirias kabisa kama vile anachokisema ni sahihi[emoji23].

Huyo jamaa anafananisha rangi tu ya paka wa porini na wale paka wenye rangi hiyo ambao hufukuzwa nyumbani
 
Mtaani utotoni alikuwepo mmoja wa hivi. Na kweli aligeuka adui wa binadamu, vyakula na mifugo midogo midogo, alisumbua sana.

Iliundwa kamati ya vijana pamoja na mbwa kadhaa, ile vita ilikuwa balaa sanaa, maana wale mbwa kwanza aliwakalisha vibaya sana, alivimba wote tulisogea pembeni ila mwisho wa siku mwanaharamu yule alipelekwa anapostahili baada ya battle kali sana
 
Usidhani. Hilo ndo jina lake halisi = PAKA SHUME.
 
Anaitwa MONDO.. famous Kwa jina la "wild cat"
Anakula panya kama kawaida, sema anakula adi kuku,kanga Kwa kuwinda..

Apo ni mkubwa...sio kama giant cat wengine yani chui,tiger
 
Kabla ya vita kuanza ni lazima mkazibe matundu ya vichuguu vya karibu. Nilikwaga mwenyekiti wa kamati hii zamani zile. Ikitokea akaingia ndani ya kichuguu,basi matundu mengine yatazibwa,Linabaki 1,unakokwa moto kupitia hilo tundu,pilipili kichaa bila kusahaulika alafu ilo tundu linazibwa pia. Hatorudi tena.
 
Huyo ni paka wa porini anaitwa Serval
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…