Umewahi tembea umbali gani mrefu kwa miguu ndani ya jiji la Dar es Salaam?

Sijaona alietembea humu , sisi tunatembea tumebeba na vyakula kabisa...Yani mnaanza safari jua alijatoka mnafika linazama ,ni usiku.
 
Sinza Mori hadi Sinza Mapambano
 
ila Mbeya nishawahi tembea toka mwanjelwa hadi shuleni (Iyunga) nilikula nauli 200 tu form one hata kuomba kwa konda siwezi sitasahau
 
Palm beach hadi mwenge,kinondon manyanya hadi mwenge hizi nimezipiga sana kila mara yaani nikitoka xul ,ila kubwa kuliko ni kkoo to mwenge
 
Kariakoo - Kinondoni studio.
Buguruni - Mawenzi.
Buguruni - katakana.
Gomzi - Jitegemee.

Ni matunda ya kula nauli, kununua nguo/viatu..,
Hii ya mwisho Ilikua usiku na nikadakwa na wajeda wakati naruka ukuta, ila tulikua wengi.

Hio ya pili Ile nafika tuu nyumbani nahojiwa mbona umechelewa?? ile najibu tuu, nikarudisha chenchi seble nzima.
 

Kumbe na wewe ni wa moro.

Mimi nimekaa moro town miaka 3 na nimejenga kibanda changu hapo.

Mimi na uhaya wangu ila huniambii kitu moro napapenda sana
 
Mbezi beach high school mpaka wazo hill enzi za mgomo wa daladala kipindi cha jakaya hiyoo wazeee nililala siku mbili hom koz ilikuwa ijumaa hivi wakuuu
 
Nilikuwa natembea kutoka tabata shule mpka Ukonga Mombasa maeneo ya relini, nanyoosha mpaka buguruni kwa mnyamani kwa shortcut nakata mpka veta nanyoosha mpka Airport mpka home. kipindi kile nauli ilikuwa 20 Tsh

Nikiwa darasa la 4 na ni kwasababu tulikuwa tunakaa tabata sasa tukahamia kwetu ukonga na darasa la 4 ilikuwa ngumu kuhama kama mtu kasajiliwa mtihani kweny shule husika
 
Yale mabomu ya G/mboto[emoji23]

Kutoka g/mboto rada chuo hadi ubungo but sielewi nilifikaje na sitaki kukumbuka hii kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…