Nakumbuka siku moja nikiwa Msasani alitokea kijana mmoja akaniomba nimtembeze kwenye mtumbwi.
Ila kwa bahati nzuri kukawa na boti linaenda Kigamboni siku hiyo, basi bhana nikamuunganisha akaniambia tuende wote mpaka taifa tukaangalie na Mpira kati ya Yanga na Mbeya city.
Alifurahi sana tulipofika Kigamboni tukapanda panton tukavuka posts tukaenda kupanda magari ya rangi tatu, basi bhana tulipofika akaenda kukata ticket kwenye gari akakata ya kwake tu akaniambia nimsubiri, anaenda kutoa hela kwenye simu, nikamuamini poa tu japo nilishashtuka ila nikawa najipa moyo.
Mpaka Mpira unaanza hakutokda ila bidi nianze kupiga ado ado na mguu mpaka msasani.
Kutoka Coco beach hadi kurasini, hiyo siku ilikuwa Boxing day ya Christmass nikiwa na wanangu wa damu tulipiga "pedeli" kutoka Coco beach hadi mitaa ya kurasini baada ya kukosa usafiri ilibidi tufanye maamuzi magumu.
Picha limeanza tumemaliza kuogelea tukasema twende tukachukue gari za kurudi kitaa, bahati mbaya kule ushuani hakuna daladala za kuja kurasini moja kwa moja na zote zilizokuwa zinakuja zilikuwa zinajipangia nauli ambayo mimi na watoto wa mbwa wenzangu tuliona haiko fair (tulikuwa na misimamo ile ya kijamaa).
AZIMIO LA COCO BEACH:
Basi tulikubaliana na wana tupige "pedeli" kutoka Coco beach mpaka posta ambapo kipindi hicho kulikuwa na hiace za Tandika-Posta. Kufika Posta gari hakuna, kumbuka miaka hiyo kuna ile michezo ya watu kukodi gari kuwapeleka beach hivyo ikapelekea uhaba wa usafiri. Kamati ikakaa na kuja na azimio dogo baada ya lile la awali kugonga mwamba.
AZIMIO LA POSTA:
Basi kamati ya Wazalendo ikiongozwa na mimi tukakubaliana tusogee mpaka hapo Stesheni maana kulikuwa na hiace za Temeke-Stesheni kupitia barabara ya kilwa zingetufaa sana kama tukishukia Police ufundi au Jkt basi kurasini sio mbali kabisa.
Tulianza mdogo mdogo kuelekea Stesheni lakini kwa bahati mbaya au nzuri hiyo siku ilipangwa tufanye matembezi ya hisani bila kuwa na ajenda yoyote ile.
Baada ya kufika Stesheni hali ilikuwa ni ile ile tu kama ya Posta ikabidi kamati iende "chemba" kidogo.
AZIMIO LA STESHENI:
Baada ya wataalamu wa kusoma ramani na kutafsiri picha (MAP READING AND PHOTOGRAPH INTERPRETATION) kumaliza kikao kidogo likazaliwa Azimio la Stesheni.
Wataalamu walibaini kuna njia za mkato nyingi ambazo tunaweza kuzitumia kama askari wa miguu kuweza kufikia target bila kuchoma nauli kwa kutumia usafiri usiohitaji nishati ya Mwarabu.
Basi tulianza mdogo mdogo story nyingi sana na kujipa moyo kwamba palipoaki ni padogo sana ukilinganisha na tulipotoka.
Ukizingatia kipindi hicho tulikuwa tumeshaanza kupita Dojo na kupikwa vilivyo huo umbali ulikuwa wa kawaida sana na kuona kama mazoezi tu ya ukakamavu.
Tulifika kurasini kwa wakati kabisa japo kigiza kilikuwa kimeshaanza kuingia lakini hakuna aliyejua kuwa tulipitia changamoto gani siku hiyo.
Ile kamati hakika ilitoa wazalendo wa kweli ambapo kwasasa wanalitumikia Taifa mikoa mbalimbali hapa nchini