Umewahi tembea umbali gani mrefu kwa miguu ndani ya jiji la Dar es Salaam?

42km kwa mkimbiaji nzuri na kimashindano ni masaa 2+
Weweeee 59km kwa masaa 10 ilikuwa n milima gani hiyooo ulipanda mkuu
Alikuwa anatembea huyo, mimi nilitembea mwendo wa kawaida kabisa km 32 kutoka makete wilayani hadi ikonda kwa masaa 6 kasoro. Ina maana km 42 ningezimaliza kwa masaa 7 au 8 kwa kutembea.
 
Safari za Ubungo nhc to kariakoo via makanya street tandale tumezifanya.sana kwenda na kurudi ukiacha zile za Ubungo to Muhimbili
Via morogoro road
Kali kuliko zote ni ile ya mwaka majuzi nipo kibada kigamboni nasubiri daladala za kongowe niunganishe mpaka rangi tatu kukuta daraja
La mto mzinga limejaa maji baada ya mvua kubwa siku hiyo
Dalala za kigamboni kongowe zilikuwa foleni toka kibada mpaka Toa ngoma. Ilibidi kutembea kwa miguu toka kibada mpaka kongowe
Na kongowe Tena tukakuta dalala za kwenda rangi tatu na tandika pia hazitembei kwa foleni ya mto mzinga ikabidi kutembea Tena mpaka stand ya Rangi tatu
Uzuri ilikuwa mafuriko ya watembea kwa miguu kwa hiyo ikawa haichoshi Sana Ila sitosahau hiyo siku
Can u imagine ni kilomita Ngapi nilitembea toka kibada mpaka rangi tatu kupitia kongowe

Sasa humu nikimuona mtu anasema katembea Sana yaani kutoka sinza kwa remmy mpaka magomeni au manzese mpaka kariakoo au keko mpaka cjui kariakoo namshangaa sana
 
Kutoka Chuo Udsm hadi nyumbani mbagala
Sitosahau nilitumia masaa sita kufika nyumbani nilitoka chuo saa sita mchana nikafika hom saa 12 jioni
 
Achana na Dsm

Nilikuwa Mbeya maeneo ya Isanga Tankini, nikapigiwa simu kuna kitu nikifate Nzovwe maeneo ya Iyunga.

Hapo sina nauli

Nikasema sio ishu, nitapiga lwa mbwa haste haste hadi Nzovwe kupitia njia ya hapo Sokomatola, stendi kuu kushuka na kimtetemko cha meta.

Nikafika Nzovwe, mgongoni nilikuwa nimebeba Rasket ambapo ndani yake kulikuwa na vitu vyangu vya muhimu.

Nikatua Rasket nikatoa vitu vilivyokuwa ndani ya Rasket ili niweze kupanga vizuri nipate nafasi ya kuweka hicho kitu nilichokifuata.

Baada ya kukamilisha na kuona kila kitu kipo sawa, nikawaaga nikawa narudi zangu Isanga haste haste.

Nikafika mpaka home huku nikiwa nawatambia wanangu kuwa daladala ni za mademu, mwanaume lazima ukanyage lwa mbwa.

Nikatoa vile vitu kwenye Rasket, katika hali isiyoya kutarajia nikagundua kuna property moja ime miss.

Nikaanza kuvuta kumbukumbu nikagundua ule wakati nikiwa Nzovwe natoa vitu, navyoruishia ndio niliposahau kukirudishia.

Ikabidi kwanza nipige simu Nzovwe ku confirm, wakaniambia kweli nimekisahau.

Kwa hiyo nikawa na root nyingine ya kurudi tena Nzovwe lwa mbwa.
 
TAIFA HADI CHAMAZI, sitosahau malamamae
Unastahili tuzo ya kiatu 🤣 kama Mayele...

Asikwambie mtu Dar hapatembeleki 🤣🤣🤣

fire mpaka mnazi mmoja tu hapo nilimlaani yule mama mno
We ni mvivu kinyama utakuwa bonge sana kwa aina hio ya maisha
 
kutoka Jkt mgulani mpaka kongowe mzinga siku hiyo sitakuja kusahau mvua ilikuwa inanyesha sana foleni ilianzia bandarini mpaka mbagala inabidi tushuke tuanze kutembea mdogo mdogo
Mkiwa wengi haina kwere 🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…