Umewahi tembea umbali gani mrefu kwa miguu ndani ya jiji la Dar es Salaam?

Kutoka Temeke Mikiroshini ~Kariakoo ~Ubungo ~Temeke Mikiroshini
 
Posta kile kituo wanapaita baridi mpaka Jay Mall, Siku hiyo ndo mara ya kwanza nimepanda daladala sijui kuwa bus haziendi shusha posta mpya zinazunguka pale. Nilaani sana aliyeanzisha ule utaratibu..... Sina hamu mpaka leo.
 
Mawasiliano hadi muhimbili.
Sema tulikua wawili, ila nilichoka ile siku khaaah.
 
Uko vizuri kamanda, lakini mwendo si huwa unapungua kadri unavyokata distance? namaanisha masaa mawili ya mwanzo speed yako haiwezi lingana na baada ya masaa ma5
 
Mzee umesoma Ludewa?
Japo pale ni parefu sana na mapori mengi.
 
Mawasiliano hadi muhimbili.
Sema tulikua wawili, ila nilichoka ile siku khaaah.
Mbona pafupi tu hapo! Mimi nilikuwa nasoma Urafiki na mwamba mmoja. Huyo alikuwa anatoka Kimara go and return kila siku.
Alikuwa anafika darasani ameshajichokea kabisa.
 
Morocco- kimara baruti
Kimara baruti - mnazi mmoja (go & return).
 
Upanga to Mwenge, Mlimani City, Ubungo, Manzese, Magomeni, Kariakoo to Upanga, ni mazoeI tu.
 
Mwaka 1980 nilisindikiza mdundiko toka Kiwalani mpaka Tegeta,
Mwaka 1988 nilitembea toka Chang'ombe hadi Terminal One Ukonga
Mwaka 1995 nilitembea toka Ukonga mpaka corner Bar Ubungo External
 
Segerea to Mwenge hili lilikua ni funzo la kuheshimu pesa........

Nilianza safari saa 11 jioni Nikafika saa 4 na nusu usiku.......
Nilipo fika tabata relini niliwaza nirud nilipo Toka au niendelee na safari ☺️😊😊 turufu ikanambia niendelee na safari......

Mbande/ kisewe to ubungo yaan boda to boda.....kanyaga sana sorry saivi nimekua Bonge mvivu sana kutembea....☺️☺️😊😊

Mikocheni to ubungo tembea mpaka Unapoteza Nuru ☺️☺️☺️😊😊😊

Kariakoo to mbagala kawaida sana yaan ni Tish tashi...muda Sasa miaka mitano Sasa sijawai Rudia kutembea umbali mrefu.....

Maisha yametufundisha MENGI ☺️☺️☺️😊😊😊😊
 
Tulitembea kutoka Titegemee(Mgulani) hadi msasani kisa mwanetu mmoja hakuwa na nauli so tukawa tunampa kampani, yeye aliendelea hadi victorial
 
Tabata to coco beach 2003 hiyo ni go and return kwa mguu
Ila Kwa maisha yangu ya saiv ya kukimbia km 42 marathon etc jiji la dar nalivuruga Sana .....mfano one route nilitoka ubungo to mbezi mwisho ,goba, madale to Tegeta to mbezi beach to mikocheni to sinza.
. etc ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…