Umoja Party ni chama chenye mlengo upi, kinaamini katika maendeleo au katika Magufuli?

Umoja Party ni chama chenye mlengo upi, kinaamini katika maendeleo au katika Magufuli?

Alafu hii ajenda ya Sukuma gang wenzenu wanaipenda maana inawapa kibali kanda ambayo bila wao huwezi kushinda uchaguzi. Fanya huo utani makabila mengine sio huko.

Ndio maana akina Msukuma ni asset sababu ya ushawishi wao kule! Kule kukiwaka moto ni hatari ambayo CCM hawatamani hata kuiota!

Mnataka kulazimisha ukabila Kama Kenya?. Hata hao wenyewe hayo mawazo hawana mnawalazimisha. Halafu huu uwongo unaenea kwa Kasi. Ninachojua kwa takwimu za uchaguzi wa 2020, chama kilichoungwa mkono Sana Kanda ya ziwa Ni CHADEMA.

Hata matokeo ya ubunge Geita mjini makao makuu ya mkoa ambapo Magufuli anatokea, waliachana kidogo sana mpaka watu wakashangaa. Njoo mwanza Mjini, njoo Musoma, bukoba Mjini, Tarime etc. Kumbuka pamoja na kuutangaza usukuma wa Magufuli mwaka 2015, lakini Magufuli aliambulia asilimia 57 ya kura. Tanzania hakuna ukabila, msitulazimishe Mambo tusiyoyajua.
 
Hoja mfu..UP Kiko n nguvu sana hasa kwa wakulima na wafugaji.

Subiri kianze..hadi watamtaja Alie muua Magufuli

Wewe Seema hoja mfu kana kwamba unajua kila kitu. Chama hakijapata usajili mmeshaanza kelele, hata muanzilishi wake hamumjui. Haya Bwana mtajikaanga kwa mafuta yenu wenyewe.
 
Duh, hii Safi Sana. Baadae wanaungana na chadema, halafu CCM ya Samia chali.

Hii nimeipenda Sana, najua kushinda hawawezi, Ila wakishamiri CCM itabidi 2025 wa rethink watuletee Chuma Kama mzee baba mwenda zake.

Hatutaki watu wasiojulikan tena
 
CCM kimekuwa mchumia belly aka tumbo kinara na kwa hili kimeungana kabisa na Chadema Zitto nae akipiga gitaa matakoni kwa chama mboga. Leteni sera kabla ya 2025 dadeki tuwakomeshe

Hicho chama mpaka kifikie level ya chadema Ni miaka 30 ijayo. Kuna stages za kupitia ambazo chadema kapitia mpaka dola ikapambana naye. Hao umoja party Wana Safari ndefu Sana.
 
Huyo ndiyo anatakiwa na wananchi isipokuwa wewe na wenzako

Wananchi gani walimtaka? 2015 kapata asilimia 57 na 2020 kavuruga uchaguzi. Angepata asilimia 80 Kama Kikwete ningekubali.
 
Mkuu wakiungana watabaki na wababe humu JF na mafisadi ambayo yote yanajulikana kiufupi wataangukia pua matako juu

Ngoma ya watoto haikeshi. Mnawadharau chadema hata usajili wa muda hamjapata bado. Subiria mkiingia site ndio mtanua siasa sio mchezo.
 
Hiki chama kilikuwa kianzishwe na system toka enzi za Magufuli, ila upepo haukukaa sawa. Lengo la chama hiki ni kuipa ccm ahueni wakati wa uchaguzi. Mpango ilikuwa kujitokeze wanaccm watakaojifanya wana mgogoro ndani nya ccm, kisha wavute watu, ila kifanye upinzani unaotakiwa na ccm. Naona sasa hawa sukuma gang ndio wamekabidhiwa huu usanii wa kuanzisha hicho chama. Ila hizi ni mbinu za kizee ile mbaya.

Cc: Msemaji ukweli

Bora umewaambia ukweli.
 
CCM imwogope nani mpaka ifanye hivyo maana hilo li chama lenu la kaskazini lilikufa mwaka 2015 wakati mwenyekiti wenu alipobadili gia angani

Nyie ndio hatuwataki Tanzania mnalazimisha ukabila. Kama chama kilikufa mbona dictator wenu alipata asilimia 57 uchaguzi wa 2015 Kura chache kuliko , na alivuruga uchaguzi wa 2020. Kama chama kimekufa Mbona kamlima risasi Lissu na kumpoteza saanane?.

Halafu huyo Lowassa yupo CCM na mtoto wake mkampa ubunge. Eti chama kimekufa, dictator kazuia siasa miaka sita sasa. Acha uongo
 
Hata ukiacha sawa tu, sasa hivi kina mamilioni ya wanachama. Subiri muda utaongea.

Tafadhali usibebe jeneza bila kujua msiba unatokea wapi. Wanachama milioni, wakati hata usajili wa muda hakijapewa?. Man expectations nyingi bila mahesabu.
 
Kwanini Zitto anakiita ACT Wazalendo? jina sahihi ni ACT Zanzibar / maslahi.

Hi chama ACT kina-act kuleta ulaji kwa maslahi binafsi ya Zitto, hana la zaidi. ACT kingekuwa chama makini cha kitaifa sera zinazowekwa Zanzibar angesisitiza na kupiga kelele ziwekwe na huku Bara pia.

Mfano bei ya vyakula, mafuta, umeme, maji, kodi, tozo wanavyowasaidia Machinga, wafanyabiashara wadogo wangefanya hivyohivyo na huku bara n.k.

Tanzania hatuna chama chochote makini cha upinzani kwa sasa. Angalia mfumuko wa bei, bei za mbolea vifaa vya ujenzi, chakula mafuta, nafaka, usafiri, ajira, mikopo ya hovyo, teuzi, tenguzi huduma za umeme, maji, tozo, kodi zisizo na tija.

Yote hayo vyama vyote viko vya upinzani kimya. Wanasimamia nini kama hivi vitu, majanga haya yote hayawahusu?

Acheni uongo, muwajaze CCM bungeni halafu kelele muwapigishe wapinzani. Hakuna biashara ya hivyo. Walilieni wabunge wa CCM wapaze sauti maana ndio mliowajaza bungeni. Yani kuanzia uenyekiti mpaka udiwani Ni CCM wenye maamuzi, lakini kwa unafiki mnwalaumu upinzani.
 
Watu wanamkubali Mwinyi kutokana na vitendo, kazi zake, utendaji wake. Anawajibika na kuwaajibisha wote kwenye serikali yake. Hana mipasho, ngojera, vijembe, visingizio. Ameiunganisha Zanzibae.Unaweza kuona Zenji inaeelekea wapi chini ya utawala wake.

Huku bara ni visingizio kibao "bei za kila kitu lazima zipande" anasema Rais wa JMT. Sababu anakwambia ni vita vya Ukraine- Urusi, Corona.

Upinzani hawahoji chochote wanataka maendeleo ya watu sio vitu, sera za ukanda, kila tatizo sababu ni Sukuma gangs, JPM, kiongozi wao mkuu baada ya kutoka jela haizunguzii tena.

Sera kuu ya CCM, upinzani ni kumkebehi JPM wanamuita mwendazake na majna mengine mengi ya kebehi sijaona yakitumika kwa kiongozi, mtu mwingine yoyote aliyekufa. Utamaduni wetu TZ tunawaita Hayati, Marehemu.

It will interesting and fun to watch kampeni za uchaguzi CCM na upinzani wa sasa wakiuza sera zao kwa wananchi

Wananchi wakiwauliza kwanini hatuna umeme, maji, tuna kodi, tozo za ajabu, mfumuko wa bei na wao wakijibu sababu ni mwendazake.

Kwanini miradi ya kimkakati inasuasua, tunakopa hovyo, wao wakijibu ni sababu ni mwendazake.

Kwanini masoko yanachomwa moto, ajali zinaongezeka, kwanini hamna sera zenu mpya kulisaidia Taifa, Wao (CCM , upinzani) wataijibu sababu ni mwendazake, Sukuma gang, Wasukuma.

Yoyote atakayehoji, au kutoa maoni mbadala ataambiwa wewe ni Sukuma Gang.

Mnawatukana wapinzani halafu mnaingia upinzani kupambana na CCM. Mmeanza vibaya Sana, ndio maana usajili hamjapewa.
 
Form six kali sana. Ila kuweka picha ya mwenda zake naona wamepatia na wamekosea. Itawasidia na itawapunguzia. Wanasemwa kuathiriwa naye wakiwemo walikosa kazi, ajira hawatakielewa hiki chama. Waitwao si watu wa kuwaamini hata kidogo, wanabadilika sana. Na wote wapo ccm. Hivyo ni shida
 
Back
Top Bottom