Umoja party walalamikia kucheleweshewa usajili, kumgongea hodi Rais Samia

Umoja party walalamikia kucheleweshewa usajili, kumgongea hodi Rais Samia

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Chama cha Umoja Party kiliomba usajili wa muda tangu April 2021 na kimeona kuna dalili za kukwamishwa licha ya kufuata taratibu zote ikiwemo kujibu mapingamizi juu ya rangi ya bendera na muonekano wa nembo hivyo kimepanga kwenda kumuona Rais Samia ili kupata haki ya usajili katika ofisi ya msajili wa vyama vya siasa.

Upande wake, naibu msajili wa vyama vya siasa, Sisty Nyahoza amesema maombi ya chama hicho yanashughulikiwa na kuwataka wahusika watulie kwani usajili una taratibu zake ambapo huwezi kuomba leo, kesho ukapata.
 
Wasajaliwe haraka tuanze kampeni mapema kama Kenya!
Kenya kampeni zinanza Miaka miwili kabla ya uchaguzi walianza mwezi wa nane 2020 uchaguzi mwezi wa nane 2022

Yaani hakuna kinachofanyika Miaka miwili ni kelele tu za uchaguzi na mikutano ya siasa viongozi hawafanyi kazi kuanzia Raisi na makamu na mawaziri na wabunge!

Unapiga kampeni hadi kufilisika kabla ya uchaguzi

Kwa hili Kenya Hawako vizuri. Watu hawataki kwenye viti kufanya kazi wakati mshahara na miposho wanalipwa na Serikali
 
Kenya kampeni zinanza Miaka miwili kabla ya uchaguzi walianza mwezi wa nane 2020 uchaguzi mwezi wa nane 2022
Kampeni zilianza 2020?? Mbona unapotosha.... Kisheria kampeni zinaanza mwezi May/June 2022.

Hayo ya siasa ni mikutano ya siasa tu Wala sio kampeni kama unavyotaka kupotosha.

Then magufuli mbona kila siku alikua barabarani akifanya mikutano ya siasa kwa alichokiita "Kazuiwa na wananchi barabarani"? Au akifanya Rais Inakua sio siasa mpaka afanye mkutano Mbowe??
 
NA hiyo katiba yao mpya naona ni kama haijawasaidia vile,yaani ni vurugu tupu,ufisadi wa kutisha,pamoja na kuuana,
Imewasaidia hauoni mahakama ipo huru na hata mafisadi kama Sonko n.k wamefikishwa mahakamani. Hayo yasingewezekana bila katiba mpya kuipa nguvu mahakama.

Proposal ngapi za Uhuru zimepingwa mahakamani kuanzia BBI, Huduma number n.k hayo bila katiba mpya yangepitishwa na Mabilion yangetumika.

Msitafute Chaka la kujificha, katiba mpya imewafaidisha kuliko kuwapa hasara.
 
Hawa wapuuzi kama wapo serious kui challenge CCM wangejiunga kudai Katiba ambayo ingepunguza nguvu za Serikali (CCM) juu ya kuvibana vyama

Sasa hapo wanamlilia Rais wakati huyo Rais ndio anampa maelekezo huyo msajili awabanie....akili ni kitu adimu sana
 
Mnaikuza tu ila hamna kitu hapo, hao wakipewa kesi ya ugaidi hiko chama kitasambaratika ndani ya wiki.

Ni CHADEMA pekee kimeweza kuwith stand the test of time. ACT kilipitia msuko msuko kidogo tu kikafa, na kama sio Maalim kujiunga huko kingekuwa historia.

So chama Cha siasa sio mihemko wanahitaji miaka 10 ndio walau watapata diwani mmoja.
una fahamu historia ya chadema...?
 
Back
Top Bottom