Umoja party walalamikia kucheleweshewa usajili, kumgongea hodi Rais Samia

Umoja party walalamikia kucheleweshewa usajili, kumgongea hodi Rais Samia

Chama cha Umoja Party kiliomba usajili wa muda tangu April 2021 na kimeona kuna dalili za kukwamishwa licha ya kufuata taratibu zote ikiwemo kujibu mapingamizi juu ya rangi ya bendera na muonekano wa nembo hivyo kimepanga kwenda kumuona Rais Samia ili kupata haki ya usajili katika ofisi ya msajili wa vyama vya siasa.

Upande wake, naibu msajili wa vyama vya siasa, Sisty Nyahoza amesema maombi ya chama hicho yanashughulikiwa na kuwataka wahusika watulie kwani usajili una taratibu zake ambapo huwezi kuomba leo, kesho ukapata.
Kiherehere chao kimewaponza;
Kweli Mtoto halali na hela😀
 
Mimi naamini CCM wanaogopa chama kimoja tu chadema. Hao wengine Kama Umoja party Ni vichekesho tu. Watapigwa fitna moja wapotee mazima. Tujifunze kwa ACT walikimbia wote wakamuacha zitto pekee yake, baada ya kupigwa fitna na CCM .
 
Hawatasajiliwa
Wanajua jinsi kitakavyoleta ushindani kwa mafisadi

Mi naomba kisajiliwe tuone nguvu yake. Maana kinakuzwa Sana kuliko kilivyo. Wangewauliza ACT waliishia wapi, wote walikimbia mbio wakaacha chama akabaki zitto pekee yake.
 
NA hiyo katiba yao mpya naona ni kama haijawasaidia vile,yaani ni vurugu tupu,ufisadi wa kutisha,pamoja na kuuana,

Imewasaidia sana. Imeleta devolution, maendeleo yameshuka kwa Wananchi, ndio maana inakua kiuchumi. Katiba yao ipo mbali, kule magavana wanaliwa vichwa na impeachement za kutosha. Kule mahakama kufuta matokeo ya urais sio shida wala kazi. Sio huku uchaguzi unaharibika na hakuna Cha kufanyika. Kule makamu wa Rais kumpinga Rais sio issue. Kuanzisha chama Cha siasa hakuna procedures ndefu.
 
Kenya kampeni zinanza Miaka miwili kabla ya uchaguzi walianza mwezi wa nane 2020 uchaguzi mwezi wa nane 2022

Yaani hakuna kinachofanyika Miaka miwili ni kelele tu za uchaguzi na mikutano ya siasa viongozi hawafanyi kazi kuanzia Raisi na makamu na mawaziri na wabunge!

Unapiga kampeni hadi kufilisika kabla ya uchaguzi

Kwa hili Kenya Hawako vizuri. Watu hawataki kwenye viti kufanya kazi wakati mshahara na miposho wanalipwa na Serikali

Acha uongo, Kenya mikutano ya kisiasa ipo sana na sio kampeni. Kampeni zitaanza mwezi wa sita.
 
Acha uongo, Kenya mikutano ya kisiasa ipo sana na sio kampeni. Kampeni zitaanza mwezi wa sita.
Unadanganya nani toka 2020 August kampeni zimepanda

Rutto na Kenyatta wanasubiri kutofautiana mwezi wa sita ? Mjinga wewe
Kenyatta kusema anamuunga mkono Odinga atatangaza mwezi wa sita? Hopeless wewe
 
Hii ni backup ya ccm, wataigiza upinzani ili kuhadaa umma kuwa ni wapinzani, lakini watakuwa wanachukua maelekezo namna ya kufanya siasa za kipinzani. Hiki chama kumeanzishwa na ccm kwa ushirikiano na Tiss 2018. Sababu kadhaa kikachelewa kusajiliwa, lengo ni kupunguza nguvu ya upinzani wa kweli. Vuta subira utaona siasa zake.
Mbowe mwenyewe anasubiri maagizo kutoka CCM,ndio maana Sasahivi anapita mtaani anaomba pesa, baada ya kujenga chama na kufanya mikutano ya kuamsha chama yeye kila siku mtaani kuchukua buku zetu,hajui mtaani wanamchi tumepigika.
 
Kama umepigika usichange maana sio lazima, na kama uliwahi kuchanga na unaona vipi kadai hela yako utarudishiwa.
 
Nitajiunga nao nione, kama watakua strategist kama mimi nitakuwa Committed. Bila hivyo tuendelee kugawana keki ya TAIFA[emoji23][emoji23]
 
Chama cha Umoja Party kiliomba usajili wa muda tangu April 2021 na kimeona kuna dalili za kukwamishwa licha ya kufuata taratibu zote ikiwemo kujibu mapingamizi juu ya rangi ya bendera na muonekano wa nembo hivyo kimepanga kwenda kumuona Rais Samia ili kupata haki ya usajili katika ofisi ya msajili wa vyama vya siasa.

Upande wake, naibu msajili wa vyama vya siasa, Sisty Nyahoza amesema maombi ya chama hicho yanashughulikiwa na kuwataka wahusika watulie kwani usajili una taratibu zake ambapo huwezi kuomba leo, kesho ukapata.
Serikali tunaiomba iache figisu dhidi ya chama chetu cha umoja.
 
Kama umepigika usichange maana sio lazima, na kama uliwahi kuchanga na unaona vipi kadai hela yako utarudishiwa.
Mwambie mbowe ajenge chama kilichoparaganyika sio kuwa ombaomba mtaani,mbowe ni mchaga mambo ya kuombaomba akawachie wagogo.
 
Mwambie mbowe ajenge chama kilichoparaganyika sio kuwa ombaomba mtaani,mbowe ni mchaga mambo ya kuombaomba akawachie wagogo.

Nasema hivi, kama umechanga sana sema ni shilingi ngapi urudishiwe chako ukanywee pombe mbovu.
 
Nasema hivi, kama umechanga sana sema ni shilingi ngapi urudishiwe chako ukanywee pombe mbovu.
Me siwezi changia matapeli wa siasa mkuu,akina Sambodo waliisha changia mamilioni,tuliisha changia ela kibao pale mlimani city, lakini zote ziliishia kwenye tumbo la mbowe hata ofisi ya chama ilimshinda kujenga kwa miaka 15 ya Wenyekiti wake,tokea enzi hizo sichangii matapeli wa siasa tena.
 
Sasa kama huchangii nini kinakuuma wanaume wakichangia hela zao?
 
Back
Top Bottom