Umoja wa Israel na Marekani uko sawa na ule wa Ujerumani na Austria 1914

Ni vita dhidi ya ugaidi
Kwa mawazo yako, ila mimi naona ni vita kati ya Israel na Hamas.
Ni mapambano kati ya Al Aqsa Flood na Operation Iron Sword.
Military Operations conducted in the course of an armed conflict can lead to GENOCIDE and WAR CRIMES. This happens when belligerents deliberately target civilians who belong to a particular group with an intention of destroying them as an ethnic, nationality or religious group.

And GENOCIDE is not a concoction of some Jewish hating states, but a long-established international crime inscribed in international conventions, declarations and resolutions.

I hope this way, it's easy to understand.
 
Uchambuzi murua kabisa huu,...
 
Inawezekana huu mwaka utaisha sitosoma andiko kama hili popote, nikakumbuka historia za wanaume kama akina Hitler enzi zile mtu aliyetisha Almanusra shetani aitwe mtakatifu maana siamini kama shetani ana mabaya kumzidi Hitler, cha ajabu alikula kichapo kutoka URUSI hadi akatorokea kusikojulikana.

Nikimtazama Netanyahu alivyo mbishi leo kuna watu wanamzoom tu na wakichoka hatoamini maana atafukuzwa yule
 
Elewa context, katika vita ya Israel na Hamas, nchi ya kwanza kutumia neno Genocide ni South Africa ndo Aljazeera akabebana nalo na kuanza kutumia neno Genocide in Gaza kwenye matangazo yake.

Kinachoendelea Gaza ni vita kati ya Israel na Hamas. Nimeweka wazi kabisa kwamba kinachoendelea ni mapambano ya Al Aqsa Flood(Hamas) dhidi ya Operation Iron Sword(Isreal).

Unaposema kwamba Operation Iron Sword ni Genocide Gaza halafu ukasahau kwamba kuna Al Aqsa Flood amabyo ilimwaga damu zisizo na hatia na huitambui kama Genocide, basi huna la maana uliloliandika ukiacha hizo historia za huko nyuma
 
Je, kile walichofanya Hamas siyo Genocide?
 
Ndugu, nadhani wewe ndiyo unapata shida kuelewa jambo rahisi kabisa.

Uhalali wa SA kutumia neno GENOCIDE umetoka kwenye mkataba wa kimataifa, THE GENOCIDE CONVENTION, ambao Israel na SA ni wanachama. Mkataba unazipa nchi wanachama wajibu wa kuhakikisha zinapambana na GENOCIDAL ACTS COMMITTED BY STATES.

Njia mojawapo ni nchi mlalamika kwenda mahakama ya ICJ na kupeleka ushahidi kuomba mahakama ipime kama kweli kuna GENOCIDAL ACTS, kisha kutoa zuio (Provisional Measures) na baadaye kutoa maamuzi endapo itathibitika kwamba kuna GENOCIDE.

Kwenye kesi ya kwanza ICJ, imesema kwamba "There is a likelihood that Genocidal Acts are committed in GAZA" ndiyo maana ikatoa uamuzi kuzuia Israel isishambulie raia wasiokuwa na hatia kwasababu uwezo huo anao.

Unaposema SA ndiyo kaanzisha ilhali sheria zinasema hivyo na tumeshuhudia mchakato wote wa ICJ unataka sisi tukueleweje labda ???
 
Heshima kwako mkuu,historia hii imenikumbusha tukio la kihistoria la muhimu sana kule ujerumani la "Nuremberg trials"
 
Kwani mchakato wa ICJ ulihitimisha kwamba kuna Genocide au hukumu bado haijatoka ndo Aljazeera na watu kama wewe mkakimbilia kusema Israel inafanya Genocide Gaza?
Yaan cha maana kwenye andiko lako ni historia ambazo umezitumia kuficha kusudi lako. Na wasiojua lengo lako kuu wanakusifia wakati conclusion na lengo lako lilijikita kwenye mihemuko zaidi.
 
Na wasiojua lengo lako kuu wanakusifia
Samahani, tunaomba utupe lengo kuu la mleta mada, mimi naona amejaribu kutoa tahadhari juu ya jambo fulani na amejenga hoja yake kupitia mtiririko fulani!
Mbaya zaidi hajalazimisha tukubaliane na mtazamo wake!
wakati conclusion na lengo lako lilijikita kwenye mihemuko zaidi.
Jaribu kupitia tena halafu uone nani ameendeshwa na hisia, papara, mhemko, jazba n.k kama siyo wewe.
 
Ukweli ni kwamba wewe ndio unaleta mihemko. Na usije ukakimbilia kwenye udini maana MALCOM LUMUMBA sio muislam wala pia sio muarabu, nakuwahi mapema kwa hilo.

Kuna kundi kubwa la Experts lina msimamo kuwa kinachotokea Gaza ni genocide. Na wengine ni waIsraeli mmoja wapo ni Professor Omer Bartov, Professor wa Holocaust and Genocide Studies.

"Professor Bartov is considered one of the world's leading authorities on the subject of genocide." Brown University German Studies

Professor Bartov sasa ana msimamo kuwa kinachotokea Gaza ni genocide. Na mwanzoni alikuwa anaona sio genocide.

Amesema Professor Bartov

"But another part of my apprehension had to do with the fact that my view of what was happening in Gaza had shifted. On 10 November 2023, I wrote in the New York Times: “As a historian of genocide, I believe that there is no proof that genocide is now taking place in Gaza, although it is very likely that war crimes, and even crimes against humanity, are happening. […] We know from history that it is crucial to warn of the potential for genocide before it occurs, rather than belatedly condemn it after it has taken place. I think we still have that time.”

I no longer believe that. By the time I travelled to Israel, I had become convinced that at least since the attack by the IDF on Rafah on 6 May 2024, it was no longer possible to deny that Israel was engaged in systematic war crimes, crimes against humanity and genocidal actions."




Msome maoni yake hapo kama wewe ni miongoni mwa wasomaji.

Na huo ni mfano mmoja tu.

Yangu hayo tu.
 
Nishasema mleta mada lengo lake ni kuongelea kinachoendelea Gaza, hizo stori nyingine kazileta tu ili avute hisia za watu wengi.
 
Ndo maana nimeshasema mimi simezi vitu kama dodoki kisa mtu fulani maarufu kasema.
Kwani hao Expert siyo binadamu?
Usimeze kila kitu kisa kasema fulani.

Ipo wazi kabisa Hamas walitangaza Al Aqsa Flood, Israel wakajibu kupitia Operation Iron Sword kwa hiyo hakuna Genocide.

Kama kuna genocide basi walianza Hamas kwani waliua kila mtu waliyemkuta mbele yao.
Ondoeni unafiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…