Umoja wa Israel na Marekani uko sawa na ule wa Ujerumani na Austria 1914

Naomba uweke hapa hukumu ya kesi ya ICJ ambayo ilionesha kwamba hiyo ni Genocide.
Kama tu ulikuwa hufahamu kama kumekuwa na kesi kubwa ICJ ambayo dunia nzima tumeifuatilia LIVE na kusikiliza pande zote mbili nina wasiwasi hata kama utaisoma hii kesi, zaidi zaidi nahisi napoteza muda.
 

Attachments

Naomba uweke hapa hukumu ya kesi ya ICJ ambayo ilionesha kwamba hiyo ni Genocide.
Samahani, kinachoonekana unataka uonekane mshindi, kama akili yako inafanya kazi vizuri kulikuwa na mabishano huko ICJ kuhusu neno genocide.

Ila ukitumia kichwa chako vizuri pitia hii summary halafu uone siasa ilivyoingia kwenye hii kesi kuhusu neno genocide.

In the Order of 26 January 2024, the Court also found that at least some of the rights claimed by South Africa under the Genocide Convention and for which it was seeking protection were plausible, namely the right of the Palestinians in Gaza to be protected from acts of genocide and related prohibited acts mentioned in Article III.


 

Attachments

Kuna ushahidi gani kwamba intention ya Operation Iron Sword ni kudestroy gazan people?
Mbona unakuwa mbishi kama nyama ya nani hii wewe?? Hebu ruhusu akili yako itumike na kufikiri tu its maximum. Usiwe mtumwa wako mwenyewe. Ondoa hisia za udini na uteule. Kuwa mtu huru then ruhusu akili yako na nafsi yako kuwa ya huru na ya haki.
 
Ni aibu kusema Trump, Putin na Netanyahu hawajaishi madhara ya vita ya pili wala hawajui madhara yake.

Hapa umetekeza
 
Ni aibu kusema Trump, Putin na Netanyahu hawajaishi madhara ya vita ya pili wala hawajui madhara yake.

Hapa umetekeza
Hakuna kiongozi aliyepo hai kati ya hao niliowataja ameshuhudia madhara ya WW2, FIRST HAND. Wote wamezaliwa WW2 imeisha, na baada ya 1945 USA na USSR ndiyo yalikuwa mataifa tajiri zaidi duniani kiushawishi na kijeshi.

Ujana wa Donald Trump, umekuwa wa miaka ya 1970's ambapo Marekani ilikuwa inamiliki 45% ya Uchumi wa dunia. Nchini Marekani peke yake watu walikuwa wanaweza kuwa matajiri kupitia mishahara tu. Hawa kina Netanyahu wamesoma Marekani na kukulia Marekani.

Kule USSR, miaka ya 70's kina Putin ni vijana, kila huduma unayoifahamu wewe ilikuwa inatolewa bure tena kwa kiwango cha juu. Watanzania waliosoma Lomonosov, St Petersburg wanakwambia Urusi kulikuwa na maisha mazuri kupita kiasi.

Ila wanasiasa kama Henry Kissinger, JF Kennedy, George Kenan, Mao Zedong ambao sehemu kubwa ya ujana wao wameshuhudia kipindi kilichopelekea WW2 walikuwa na uelewa mkubwa wa madhara ya vita kuliko kizazi chochote kile kwenye historia. Kuna wanasiasa wengine wa USA na USSR wameishi kipindi cha WW1 na WW2, huwezi kuwafananisha na kizazi cha leo hata kidogo.

Hata ukifuatilia vizuri kilichotokea kwenye THE CUBAN MISSILE CRISIS 1962 utaelewa kwanini Kennedy na Khrushchev waliweza kuzuia vita kubwa vya kinyuklia ambavyo vingeua mabilioni ya watu duniani. Declassified Documents zinaonesha kwamba Kennedy alimwambia Nikita kwamba anaomba aonekane ameshinda ili aweze kuwatuliza wahafidhina wa USA wanaochukia COMMUNISM.

Kiufupi The Cuban Missile Crisis, ingetokea wakati mtu kama Donald Trump na Medvedev wako madarakani kwenye kizazi chetu, leo hii tungekuwa tunazungumza mengine kabisa.

Kama unahisi Donald J Trump au George Bush wanaweza kuwekwa kundi moja na wanasiasa aina ya Henry Kissinger, Richard Nixon, JF Kennedy basi nasema umelala mkuu, amka!

NB: COLD WAR haikugeuka kuwa HOT WAR siyo kwa bahati mbaya!
Hii video hapa chini ni Waziri Mkuu wa Singapore Lee Kuan Yew akizungumzia tatizo la USA kukosa viongozi wenye weledi. Hebu msikilize:

View: https://youtu.be/vNQXLhIcPrc
 
Suala la Astro-hungary ni taifa lililojengeka ktk wazo la kisiasa na kiutawala na kimaslahi baina ya hao Austria na Germany.Na hio Austria haikuwa na mizizi Zaidi ya hio ya kisiasa......... Uhusiano Kati ya marekani na Israel ni tofauti kabisa na Huo WA ujerumani na Austria... Israel ipo mashariki ya Kati na imekutana na marekani njiani.....Katika kusettle kwake Katika nchi yake ya asili ilishikwa mkono na uingereza ña baadhi ya nchi za ulaya.(Ref Balfour treaty) Na baada ishaweka mizizi Katika nchi yake ndipo ikakutana na marekani na mahusiano Yao yakaanzia hapo.....Na ukiangalia utaona Israel inaweza kusurvive pasipo na msaada WA marekani Kwa sababu tayari ana mizizi ktk nchi yake..... Mataifa yote makubwa Kwa Israel yanatekeleza majukumu Yao Tu ya kuhakikisha uwepo WA Israel na yatakapokuwa si mataifa makubwa bado Israel atasurvive.Kwa sababu Bila kutulia Kwa Huyo Israel hakuna yoyote atakaetulià... America ana uhusiano na Israel Kwa sababu ya Eneo alilopo Israel limemsaidia kuzipata misri,, Jordan na Saudi na washirika wake na pia yeye na israel wanashirikiana kwa taarifa na teknolojia...Lakini Israel amejiwekeza kibiashara asia,,ulaya na amerika... Israel anaweza kumudu kuwepo hata marekani akiwa sio super power....Maana kampuni zenye kufanya biashara kwa maslahi ya israel zipo mpaka black market...... Kingine Huyo Austria alijipachika kwenye dini ila Israel ni chanzo cha dini.....dini unayoiona amerika na ulaya na afrikà chemchem yake ni Israel....Mwisho kabisa Marekañi imekuwa super power na kumaintain kutokana na kusoma makosa ya japan,,uingereza,,ujerumani na soviet union kwa hio wanaoisubiri china iwe super power watasubiri sana...Na kuhusu Israel kufutika midle east hio ni day dream au tatizo la halucination...
 
Umoja WA Mataifa uko biased Kwa Israel na umejàa double standard Kwa taifa la Israel kutokana na kuwa na wanachama wengi waliojaa unafki dhidi ya Israel...Kama Israel itajipata kwenye wakati mgumu hutoona kelele,, upuuzi na ujinga kama unaouna Sasa hivi sijui genocide au chochote....Wengi watafurahi...Kwa sababu ule ni Kama mwiba ukitaka kuudhuru,,unakudhuru wewe...Kwa hio wengi wa hao wanafiki mandazi wameshindwa na lile neno dogo kwamba ''If we can't fight him let us join him''' Mwisho wanamuombea ubaya Tu Israel na wakashindwa kujua ziko tarehe zimeunganishwa na Huyo Israel...
 
Kama tu ulikuwa hufahamu kama kumekuwa na kesi kubwa ICJ ambayo dunia nzima tumeifuatilia LIVE na kusikiliza pande zote mbili nina wasiwasi hata kama utaisoma hii kesi, zaidi zaidi nahisi napoteza muda.
Kwenye hii hukumu hakuna mahali ambapo ICJ ilithibitisha kwamba kuna Genocide bali ilikubaliana na hoja za SA kwamba kwa yale yanayofanywa na na Israel huko Gaza yanaweza kuwa yanaenda kinyume ni Genocide Convention.

Kama ulifuatilia, Israel iliamriwa kuhakikisha kwamba inafanya kila linalowezekana kuwalinda raia wa Gaza na kuhakikisha wanapata huduma muhimu kama chakula na usalama.
Kwa kifupi neno Genocide lilibebwa juu juu na AlJazeera na baadhi ya wandamanaji lakini hakuna sehemu ambayo ICJ ilithibitisha kwamba kuna GENOCIDE Gaza kwani kesi ya msingi haijasikilizwa na hiyo order ya mwezi January ilifuatia maombi ya SA ambayo ilitaka Israel isitishe vita.
 
Sitafuti ushindi bali tunaeleweshana. Na muache kuamini na kutumia maneno kimhemuko kisa mtu fulani maarufu kasema kwa utashi wake binafsip

Some vizuri na uelewa maana ya AT LEAST SOME RIGHTS CLAIMED BY SA UNDER GENOCIDE CONVENTION.
Kwa hiyo haimanishi kwamba kulikuwa na genocide. Hata hamas walivunja baadhi ya hizo haki ambazo zipo ndani ya Genocide Convention ila hamsemi walifanya Genocide.
 
Mbona unakuwa mbishi kama nyama ya nani hii wewe?? Hebu ruhusu akili yako itumike na kufikiri tu its maximum. Usiwe mtumwa wako mwenyewe. Ondoa hisia za udini na uteule. Kuwa mtu huru then ruhusu akili yako na nafsi yako kuwa ya huru na ya haki.
Wewe ndo mdini na mtumwa kwa sababu hakuna sehemu ambayo nimetaja dini au dhehebu la mtu.

Kinachoendelea Gaza ni operation iron sword ikijaribu kupambana na Al Aqaa flood. Tusikimbilie kusema genocide wakti kila upande una operation yake.
 
Kwenye hii hukumu hakuna mahali ambapo ICJ ilithibitisha kwamba kuna Genocide bali ilikubaliana na hoja za SA kwamba kwa yale yanayofanywa na na Israel huko Gaza yanaweza kuwa yanaenda kinyume ni Genocide Convention.
Mkuu, tayari umeshaisoma na kuimaliza hukumu yote ya kurasa 29 ???
 
Taasisi ya UNITED NATIONS inakuwaje biased kwa Israel ilhali yenyewe ndiyo imeliunda taifa la Israel mwaka 1948 ???
 
Umeongea mambo mengi sana bila kuweka ushahidi wowote, hili ni kosa. Chanzo chako kikubwa cha haya uliyoyasema hapa ndiyo kile tunaita TRUST ME BRO. Lakini pia umepinga hoja zangu bila kueleza dhahiri hoja yako ni ipi na wewe unasimama wapi (Your Points are Vague, and they lack veracity), japo ntajitahidi kuzijibu kwa ushahidi:

Mosi, taifa la Israel limeundwa mwaka 1948 na UNO kwa msaada mkubwa wa USA, USSR na Great Britain. Unaposema Israel na USA wamekutana njiani sielewi ulikuwa unamaanisha nini.

Pili, unaposema taifa la Israel linaweza kuendelea bila hata msaada wa USA au taifa lolote lile bila kuleta ushahidi wa kuthibitisha hoja yako ni udhaifu mwingine mkubwa wa hoja yako. USA anaisaidia Israel DIPLOMATICALLY, FINANCIALLY, TECHNOLOGICALLY and MILITARILY, na ni mtu mjinga tu ndiyo anaweza kupinga hili. Kila mwaka, USA anaipa Israel msaada wa USD 3.8 Billion kama msaada wa kijeshi.

Tatu, unaposema makampuni ya Israel yanafanya vizuri na yako kwenye Black Market, napata wasiwasi na uelewa wako wako wa uchumi. Hebu nitajie walau makampuni matano makubwa ya Israeli ambayo yanaweza kulinganishwa na yale Top Ten of Fortune 500.

Nne, Israel haijamsaidia USA kupata Misri. Marekani amekuwepo LEVANT hata kabla ya kuundwa Israel 1948. Ukisoma historia utafahamu kwamba, Middle East/Persian Gulf kushawahi toke THE IRAN CRISIS 1946, ambapo USA na USSR walikuwa wanagombania kutawala Iran baada ya WW2 kuisha. Harry Truman walivutana na Joseph Stalin hadi kupelekea USSR kuondoa vikosi vyake kule.

Wewe unaposema Israel ndiyo imemsaidia USA kuzipata nchi za Middle East umeliokota wapi, ilhali tunafahamu kwamba USA amekuwepo eneo hilo hata kabla ya Israel haijawa nchi ???
 
Mkuu imeandika kisomi, afu kinabii zaidi. Kumbe ndo maana kiduku hawamsumbui🙏
 
Kwahyo Ile October 7 haikuwa genocide? Israel ina haki zote za kujilinda kwanamna yoyote ile hata wafe wapalestina au walebanon wangapi, hao watapita ila Israel itabaki
Tatizo ndio huwa linaanzia hapa.......yaani ile tarehe 7 wenyewe wanaona kama kafa kuku mwenye kideli.. yaani waislael walistahili kufa kitu ambacho hata umoja wa mataifa kupitia katibu wake amekaa kimyaa baada ya kuchagua upande........ndio msingi na ndio shida kubwa iliyopo hapa.......wale wanajeshi wa UN wanaona kabisa matukio na shida zote za hawa prox lakin wako tuli hata hawaonyeshi ushirikiano hata tu wa kukemea kwamba msitukalibie sisi sio ninyi .......yenyewe yako kimya kama yako kwenye kufatilia VAR ndio maana nyau nyau kasema wewe katibu wa UN usije tena islael sababu umechagua pa kupendelea.......na hamisha hawa mgambo wako la sivyo watakiona cha mtema kunde.......Israel yuko sawa kujitetea na palestine pia wako sawa kudai kipande chao ila hao prox ndio wanareta udini na kutaka kuiretea vurugu inchi ya Israel........kwa mguu wa dini. ........hitimisho langu ningefanya kama india vunja kira kitu ambacho hawa jamaa wanaamini na kukitumia katika inchi yangu ili nimalizane nao jumla .....mwisho
 
Nimekuelewa, japo hekalu la Zerubabeli nalo huwa tunaliita la Suleimani. Hata hilo la tatu ambalo linapangwa kujengwa nalo litaitwa Hekalu la Suleimani. Sasa turudi kwenye hoja yako ambayo imekaa kidini zaidi na kukacha historia.

Kihistoria na kisayansi, zaidi ya asilimia 50% ya wapalestina ni watoto wa Wayahudi ambao walibadili dini (Jewish Converts) kipindi madola ya kikristo na kiislamu yalipotawala Jerusalem. Hapa ndipo udhaifu wa hoja yako unapokuja.

Labda uniambie, kati ya Wayahudi waliotokea Ulaya (Ashkenazi) ambao huwezi kuwatofautisha na mzungu, na Wayahudi (Sephardim/Palestinians) ambao wengi ni Waislamu ni nani ana haki zaidi ya kuiita Palestina/Israel nyumbani ???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…