Mkuu kujilinda muhimu,nilitemea ungeulizia kuhusu Israel kupora ardhi wa Wasyria pale milima Golan dunia ipo kimya pia kila kukicha Israel inapora ardhi ya waparestina na kujenga makazi dunia kimyaaaa kama hakuna dhulma inayofanyika,wiki ya Jana wamevamia mashamba ya wapalestina wakakata mizeytuni kwa chainsaw dunia kimyaaa wapalestina wangejibu ungeambiwa magaidi na je mpaka unajitambua unajua kuwa Bethlehem ipo palestina?
Sent from my TECNO CA7 using
JamiiForums mobile app
Sasa wapalestina, kama mfano ulioutumia, watajilinda vipi mkuu dhidi ya uonevu wanaofanyiwa!
Hata sisi wengine tutakuja kuwa hivyo hivyo, aah, hapana, ukweli ni kwamba tupo hivyo hivyo hadi sasa. Mkubwa yeyote akiamua kuwa anataka kulinda maslahi yake, awe, mchina, Mmarekani au hata hawa wengine wadogowadogo kama India, Uingereza, Ufaransa, kama maslahi yao hayo yapo hapa kwetu, tuna lipi la kuwazuia?
Tumeona Marekani akiwafurumusha akina Saddam, Gaddafi na wengine, na dunia hakuna ilichoweza kufanya!
Lakini nikirudi nyuma kidogo na kama kujipinga kwa hayo niliyoweka hapo juu. Je, nikuulize mkuu, kwa hali ilivyo sasa, kuna mbabe yeyote anayeweza kurogwa na kuamua kwenda kumpa amri Israel, au Korea Kaskazini?
Kwa upande huo, naweza kusema kwamba kwa nchi kama yetu hii, tunaweza kabisa kusema hatutaki kuchezewa na yeyeote, awe na makombora au vipi, kwa maana akijaribu tu, hata yeye kamasi zitamtoka, pamoja na kwamba anaweza kutumaliza kabisa kama taifa, lakini hata yeye nchini kwake atakuwa na maumivu makubwa sana.
Maana ya hii ni kwamba, wananchi wake hawatamruhusu afanye ujuha wa kutushambulia.
Hili linawezekana tu, kama tunaamua kujilinda sisi wenyewe bila ya kutegemea hiyo dunia.