Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Kwa sauti moja hapo jana baraza kuu la umoja wa mataifa lilipitisha azimia likitaka vita visitishwe kwa muda ili kutoa fursa ya majadiliano na kuwezesha misaada kuingia Gaza.
Kinyume chake taifa la Israel limepinga azimio hilo na katika kipindi cha masaa 24 wameongeza mapigo makali kuzidi ukali wa siku iliyopita.Katika tamko la kupinga azimio hilo Israel imeiambia UN haina uhalali wa kutoa azimio kama hilo.
Vikosi vya IDF vimeanza kuingia Gaza kwa wingi kwa kutumia vifaru ardhini na ndege za kijeshi angani zikisaidiwa na droni.
Hali ya Gaza imeelezwa na walio ndani kuwa sasa ni balaa tupu,hakuna matumaini tena na hata watu walioko huko ikiwemo waandishi wa habari hawawezi kufikiwa tena. Ndugu walioko nje na ndani kusini na kaskazini hawawezi kujuliana hali tena.