Umoja wa Mataifa wapitisha azimio kutaka vita isitishwe, Israel yapinga na yaongeza mapigo Gaza

Kinyume chake taifa la Israel limepinga azimio hilo na katika kipindi cha masaa 24 wameongeza mapigo makali kuzidi ukali wa siku iliyopita.Katika tamko la kupinga azimio hilo Israel imeiambia UN haina uhalali wa kutoa azimio kama hilo.
Wanajua Marekani ipo kuwatetea ndio maana wanaonyesha jeuri.
 
UN ni marekani na marekani ndio anamuunga mkono israel,unadhani hicho kiburi ni cha bure?
 
Kwa sauti moja hapo jana baraza kuu la umoja wa mataifa lilipitisha azimia likitaka vita visitishwe kwa muda ili kutoa fursa ya majadiliano na kuwezesha misaada kuingia Gaza.

Kinyume chake taifa la Israel limepinga azimio hilo na katika kipindi cha masaa 24 wameongeza mapigo makali kuzidi ukali wa siku iliyopita.Katika tamko la kupinga azimio hilo Israel imeiambia UN haina uhalali wa kutoa azimio kama hilo.

Vikosi vya IDF vimeanza kuingia Gaza kwa wingi kwa kutumia vifaru ardhini na ndege za kijeshi angani zikisaidiwa na droni.

Hali ya Gaza imeelezwa na walio ndani kuwa sasa ni balaa tupu,hakuna matumaini tena na hata watu walioko huko ikiwemo waandishi wa habari hawawezi kufikiwa tena. Ndugu walioko nje na ndani kusini na kaskazini hawawezi kujuliana hali tena.
Hamas aliyakoroga, huu uongozi wa sasa wa Israeli ni wa Wayahudi wasioyumba kwenye misimamo yao. Mbaya zaidi dunia ilikuwa inapitia kipindi ambacho hata uonevu ulikuwa na watetezi wa kutosha katika vita vya Urusi na Ukraine. Sababu za Urusi zilikuwa ni kuwa,, Ukraine anakaribisha adui wa Urusi. Kwa Israeli, siyo tu adui kasogea, ila kaua maelfu na kuteka wengine. Wasiwasi wangu ni kuwa, Israeli ataiteka Gaza kwa ujumla wake.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Kwakweli hali inatisha sana huko Gaza!!!
Watoto wadogo wanauwawa wamekosa nini?!!! hii ni laaana kwa Israeli.
Benjamin Netanyahu atawajibika kwa mauaji ya watu wasio na hatia, na anapaswa afikishwe international court
 
Kwa sauti moja hapo jana baraza kuu la umoja wa mataifa lilipitisha azimia likitaka vita visitishwe kwa muda ili kutoa fursa ya majadiliano na kuwezesha misaada kuingia Gaza.

Kinyume chake taifa la Israel limepinga azimio hilo na katika kipindi cha masaa 24 wameongeza mapigo makali kuzidi ukali wa siku iliyopita.Katika tamko la kupinga azimio hilo Israel imeiambia UN haina uhalali wa kutoa azimio kama hilo.

Vikosi vya IDF vimeanza kuingia Gaza kwa wingi kwa kutumia vifaru ardhini na ndege za kijeshi angani zikisaidiwa na droni.

Hali ya Gaza imeelezwa na walio ndani kuwa sasa ni balaa tupu,hakuna matumaini tena na hata watu walioko huko ikiwemo waandishi wa habari hawawezi kufikiwa tena. Ndugu walioko nje na ndani kusini na kaskazini hawawezi kujuliana hali tena.
Dadeki kazi wanayo
 
Back
Top Bottom